Kubadili matokeo IV 2012: Prof. Mukandala aivimbia serikali!

Kama kweli, hongereni sana na endelezeni uzalendo huu Prof. Mukandala Dr. Ndalichako. Safi
 
Mukandara sio mtu mwenye msimamo thabiti kwa mambo ya msingi na hasa inapokuwa serikali ya Kikwete inahusika; Kikwete ndio aliyemzawadia hicho cheo cha UVC hapo UDSM hivyo hana ubavu wa kumpinga!!! Siamini kabisa kuwa Mukandara anaweza kupinga maamuzi ya serikali. Udhaifu wa uongozi wake pale UDSM ndio chanzo cha kuanguka kwa hadhi ya chuo hicho na hata ahao ALUMNI anaosema watasaidia kukipatia chuo msaada ,wengi wao naamini hawatakisaidia chuo kwa sababu ya uongozi mbovu wa Mukandara!!!
 
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Kama ni kweli, basi upepo wa mabdiliko hauzuiliki, hadi Mukandala?
 
Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Heko! Hii ndio professionalism!

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo! VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

I love it!
 
Serikali ijiwajibishe yenyewe, usitegemee upande bangi uote mpunga, haya matokeo ya litarajiwa na bado tusubiri kiama cha matokeo mabovu kwa mtindo huu tuendao. Mungu ibariki Tanzania na kizazi hiki cha utawala usio na muelekeo thabiti.
 
mukandara huyu ndo bhajiuzulu? ngoja tuone, maana elimu bongo bora liende, tangia enzi za mungai elimu yetu ilianza kuyumba.
 
Nakushauri pia kapitie mitaala ya kufundishia pamoja na quality ya walimu tulionao hapa Tanzania, halafu rudi tujadili vizuri. Sababu ziko nyingi ila nilizotaja hapo ni kidogo sana. Ninachokikataa na kukiona cha kipuuzi zaidi ni suala la kusema wana-standardize matokeo, hapa wanafanya standardization kwa faida ya nani? Kujifariji kuwa waliofaulu ni wengi wakati ukweli unajulikana? Huoni kuwa kwa kufanya hivyo tuna haribu quality ya wasomi wajao?

ok,kwahiyo tatizo la mitaala pamoja na quality ya walim tulionao limeanza mwaka jana tu kiasi kwamba kupelekea anguko la 60%?????nnachofaham mm miaka yote tunatumia walim hao hao ambao ww umewaita ni poor quality pamoja na mitaala hiyohyo mibov(km ipo) lakni hatujawahi kuona anguko la ghafla kiasi hiki!!!

Kuhusu hoja yako ya tunastandadize kwa faida ya nani??jib ni kwa faida ya watoto wa wakulima ambao walijitahid kadri ya uwezo wao,na wengine kupeleka watoto wao private schools km st mathews,st anthony nk wakijua kua watoto watafaulu lakin pia wamepata zero!!

Hivyo,tunastandadize ili kupunguza wavuta bangi na waporaji ambao inasemekana NECTA ndio iliwasababishia anguko hilo kwa kupandisha madaraja ya ufaulu bila kuwapa habari ili kuweza kuyapokea mabadiliko hayo!
 
Uelewa wa watu juu ya jambo hili n mdogo sana. Tunapozungumzia kubadili matokeo tuna maana gani? Maana maagizo ni kuwa viwango vya ufaulu vibaki vya mwaka 2011.

Maana yake mstari wa wastani wa ufaulu kwa kila somo wa chini unashuka toka alama 35 hadi 21, ikiwa na maana waliokuwa na alama juu ya 35 hawaathiriki kwa hli.

Huku ndio kunaitwa kubadili matokeo?
 
Which minister specifically, or just any minister. The directive was from the PM and this guy doesn't deal with education (in its specificity).
Maagizo/maelekezo ni lazima yatatolewa kupitia waraka ambao most likely utasainiwa na waziri mwenye dhamana ya elimu (kama sheria inavyotaka).
 
Mi Nadhani Sio sahihi kuwaongezea Grades hao watoto waliofeli,ni kama kufunika Kombe huko mbeleni itakuwaje ?Na waliochora Zombe watapewa Grade gani

Nadhani Kama wangekua na nia ya kuwasaidi wangewaandalia mchakato wa kurudia masomo Kama alivyofanya Tibaijuka jimboni kwake sio kupitisha Mambumbumbu.
 
walichofanya waliangalia matarajio ya wapiga kura wao ili wapate kura. Kuporomoka kwa elimu "its none of their business" hivi kwani watoto wao wamesoma katika mfumo wa NECTA, vyeti vya watoto wao hata baadae haviwezi hathirika kokote kutokana na ilhili la kuchakachua matokeo. Bora liende, funika kombe mwana haramu apite. Nani hatakayethamini vyeti vya Tanzania? Wengi watayajua haya wakikua. ukweli ni kwamba kuna tatizo katika mfumo wa Elimu na sio kuchakata matokeo na kudanganya watu
 
ni bora PROF NA DR NDALICHAKO
WALINDE HESHIMA YAO prof mukandala ni msomi mzuri ila ana tabia ya
kuyumbishwa na wanasiasa na kama atalisimamia msimamo wake basi itakuwa
ushindi ata kwa wanafunzi wa UDSM pia Dr JOYCE NDALICHAKO bingwa wa
mathematics mwenye msimamo na asiyeyumbishwa ata kidogo anaweza
akajiuzulu kama serikali itaendelea na msimamo wao cha msingi WAWE NA
MSIMAMO MOJA ILA NAMWOFIA PROF ANAWEZA AKALEGEZA MSIMAMO.

hawawezi kujiuzulu hao maana hawana pa kwenda kibarua wakikiotesha nyasi! ni kawaida ya ccm kuwatumia wajuzi kama kondom na kuwamwaga kiaina
 
..hii kama ni kweli ingeonyesha angalao kuna watu huko juu wenye kupinga ile theory ya "akili ndogo kuongozwa na akili kubwa".....maana wamekutana kisiasa watawala na overnight wakaamua matokeo yabadilishwe....kwa malengo yao ya kisiasa....Kama kweli kuna dhamira ya dhati ya kuinua elimu kwanini matokeo yote ya tume ya Pinda hayajawekwa wazi???...kwanini wamechukua uamuzi huo mmoja bila kuweka wazi matokeo yote ya tume??.....kama si sababu za kisiasa ni vipi mtu anaweza kuelezea uamuzi huu wa watawala???......
 
Mwenyekiti wa Baraza
la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari
kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.

Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya
kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo
hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi
tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.

Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na
kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.

Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji
Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia
uamuzi wake huo.

Mengi yatafuata. Kaeni chonjo!
VUTA-NKUVUTE
aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

hapa hatupendi Tetesi wewe,Bado sijaelewa chanzo chako vizuri
 
Back
Top Bottom