Koffi Olomide na Mkewe Cindy Le Couer

Koffi Olomide na Mkewe Cindy Le Couer

Kaanza kuimba na koffi kitambo, angalia wimbo wa Ikea, kipindi hyo kablaa ya 2000s akiwa na akina Suzuki Luvubu
Hapana. Ameanza kuimba na Koffi mwaka 2007. Kabla ya hapo alikuwa akiimba na Mwimbaji wa TPOK Jazz ya Franco aitwaye Carlito Lassa ( Frere Carlyto) ambaye aliimba nyimbo Kama Maya, Affaire Kitikwala, album maarufu ya Mayaula Mayoni ya Don P .....


View: https://youtu.be/Ze6G_JF481w?si=bFKf2LnJrocauT5d
Kidada Kirefu ndiyo Cindy.....

Moja ya nyimbo maarufu za Carlyto aliimba na Mayaula Mayoni.

View: https://youtu.be/r_ZJphVz-sw?si=17mleIuzuiHX2DB6
 
Wajue watu wanaompa Mkongwe KOFFI OLOMIDE Nguvu ya Kudumu kwenye Muziki wa Afrika Takribani Miaka 40 Leo..

Wanasema Penye Mafanikio ya Mtu lazima kuna Connection au Mchakato flani wa kueleweka.

Hawa ndiyo Miamba tegemeo la Koffi Olomide.

1-Mkewe, Cindy le Couer. Huyu ndio kiungo, siyo muhimu Bali ni kiungo wa LAZIMA...

2-George Weah Wakawaka, DJ na Mtayarishaji Wa Muziki kutoka Yaunde Cameroon 🇨🇲.

2-Boss Batuta, Mzee Wa New York. Matamasha mengi ulaya na America Kiungo ni huyu.

3-Jean Baptiste Ilunga AKA Sundiata Keita. Huyu makazi yake Brussels, New York na Paris.. Unaambiwa Jamaa mwaka mzima anazunguka kwenye matamasha kwa wasanii wake anaowasimamia.

4-Tchacho mumbala. AKA Jamal Kashogi, huyu ni P. Funk wao, na pia ni Mpishi wa Mitindo mingi unayoiona na kusikia kwa KOFFI OLOMIDE na Mkewe CINDY.

5-Bestinne Sandra Kazadi. Huyu ni Bilionea wa Kinshasa, na alipata Kuwa Rais wa AS VITA CLUB, mpaka 2023.Ndiyo chimbo la KOFFI OLOMIDE kwenye Mambo ya pesa. Yaani ndiye GSM wake panapohitajika Neno la kipesa.

6-Tonny Muamba. Huyu ni Kiungo mwingne anayehakikisha KOFFI OLOMIDE na CINDY wanakuwa Bora muda wote. Ni mmiliki wa Mahoteli na Kumbi za Starehe Katika miji ya Paris, Marseille, Brussels na New York.

7-Davids Mumbele Matandi. Bilionea mwingne aishiye Paris kipenzi cha Koffi Olomide, huyu ndiye spea tairi ya Kila Shida analohitaji Koffi ikiwa atahitaji. Na ndiye mshauri wa tenda mbali mbali anazoingia Koffi ndani na Nje ya Congo.

8-Adolf Muteba Chilawena. Ni Zambia mwenye asili ya CONGO. Ni Promota mmoja wapo wa Koffi na ukitaka kufanya kazi na Koffi UK I mpaka Muteba akakubali Bali utakuwa umempata Koffi kwa 80%

Na Wengine Wengi, Lakini baadhi Yao ni Jean Marie Mukulasie, Bakari Manyiema, Koko Mongo Simba. Bi Salome Jose kosesa a.k.a (Mourinho).J.J Alinas. Ngaiwa Imboka, Jean Marie Nkubala, Roger bukana, Floyd Masamba, Fading Mamona, Blaise Samba na wengine Florente Ditovelle Mangani Gadi Ramadhani. Na wengine.

Bila kuwasahau watoto wake wapenzi
1-Didi Stone Olomide (Washington)
2-Del Piero Mourinho Olimide
3-Minou Olomide
4-Aristote Olomide
5-Rock Olimide.

GAVANA@2025

Kwanini anaitwa le couer kwani yeye ni moyo na si binadamu?
 
Mkuu hapo mwishoni ..Cindy anamfanya Mzee azidi kupendeza.Hawala hana talaka ...wanasaidia sana kimaisha.

Hakuna wa kumfanya Koffie apendeze, zaidi ya kandarasi zake za mitindo. V12 ana kandarasi (contracts) za kuvishwa mitindo ya nguo, kupambwa na manukato na kampuni za mitindo hapo Paris na anawalipa na nyingine ni Balozi. Kampuni ya Mwanae pia DiDistone inamvisha pia yeye na bendi ya QL. Ndombolo King harudii nguo kwa miaka mingi, anavaa "dressing to kill, dressing to impress".

Yeye na Roga Roga wana kandarasi na LV hapo Paris.
 
Ndio mi mkubwa kwako, 1994 album Maggie inatoka mimi nina akili zangu timamu na Disco naenda.

Koffii ameoa mara tatu, alimuoa Marianne Makosso, wakazaa watoto watatu. Badae Stephanie Godie nae akapata nae watoto wawili, wakatemana.
Badae 1994, akamuoa kwa urasmi kabisa Alliane, mrembo mkali sana mama yake Didistone. Wanasema huyu ndie mwanamke ambae V12 alimpenda zaidi kiasi cha kumtungia nyimbo mbalimbali. Sikiliza "Miss des Miss" toka kwenye Album Noblesse Oblige, 1994. Walidumu miaka kibao wakaachana 2021 juzi tuu hapo.

Huyo Cindy ni hawala/kimada yaani extra marital. Bado mtu mzima hajamwaga wino hapo mzee. Anapiga tuu. 😁
Umeongea ukweli mtupu aisee
 
Kwanini anaitwa le couer kwani yeye ni moyo na si binadamu?

Kumbuka Cindy aliibuliwa na Mokonzi kutoka kanisani akiimba kwaya, na Mopaa ana kipaji hicho cha maono kwa mtu na kumkuza. Bendi ya QL imepita na watu zaidi ya 1,000 wenye vipaji toka kuanzishwa kwake.

Kuhusi Cindy, Mopao ndo wa kumpa Jina hilo la stage, akimananisha "Cyndi mwenye moyo" Cyndi Le Couer. Jina la chumbani, Mopao anamwita Cyndi "Le Couer De la Mer" yaani "Kwenye moyo/shina la bahari". Yeye Mopao ni bahari. Sio umbea sikiliza "Koukoulou" utasikia maneno hayo ya chumbani, wakiitana.

Bila shaka unamkumbuka Sam Tshintu na Suzuki Luzubu kama pivotal figures kwenye kwenye album mbili za mwaka mmoja 1997 ya "Loi" na "ultimatum". 😁

Gone are the days.
 
Mshana Jr nimezidi kukuheshimu baada ya kuandika uzi wa Koffi Mopao Quadra Coraman.
Huyu mzee anastahili heshima ya milele.
Hakuna msanii aliyewahi kutokea duniani anatoa Hit song karibu kila mwaka toka miaka ya 1994 hayupo zaidi ya Koffi olomide master mathematician Genius
 
Cindy siyo poa hata kidogo. Aliingia kwenye kundi kama mwanamuziki wa kawaida! Ila kidogo kidogo akaanza kupanda cheo mpaka kufikia cheo cha juu kabisa cha kuwa Bosslady wa kundi.

Unaambiwa Mzee Baba Koffi humwambii kitu kwa Cindy. Yaani kama mimi tu huniambii kitu kwa babe wangu SweetyCandy!!
Utaniuaga kwa mapenzi babes
 
Kaanza kuimba na koffi kitambo, angalia wimbo wa Ikea, kipindi hyo kablaa ya 2000s akiwa na akina Suzuki Luvubu

Mkuu Cyndi na Ekea ni juzi tuu hapo JK raisi wa nchi hii. Cyndi anajiunga QL miaka 9 badae Suzuki (4×4) kuondoka QL. 1999 Suzuki tayari ana Solo Album "Decompte Final".
Hawa akina Suzuki, Sam Tshintu, Djudju Chet, Petty Chomba, Cyndi ni baba zake.
 
Mshana Jr nimezidi kukuheshimu baada ya kuandika uzi wa Koffi Mopao Quadra Coraman.
Huyu mzee anastahili heshima ya milele.
Hakuna msanii aliyewahi kutokea duniani anatoa Hit song karibu kila mwaka toka miaka ya 1994 hayupo zaidi ya Koffi olomide master mathematician Genius

Mkuu kwa nyongeza ni kwamba, Antoine Agbepa Mumba alias Koffii Olomide, amewahi toa album mbili mwaka mmoja, zikawa gumzo na zikashinda Kora Awards.
Album hizo ni "LOI" (LWAA) yaani sheria, 1997.
"Ultimatum" 1997 yaani kauli ya onyo.
 
Kumbuka Cindy aliibuliwa na Mokonzi kutoka kanisani akiimba kwaya, na Mopaa ana kipaji hicho cha maono kwa mtu na kumkuza. Bendi ya QL imepita na watu zaidi ya 1,000 wenye vipaji toka kuanzishwa kwake.

Kuhusi Cindy, Mopao ndo wa kumpa Jina hilo la stage, akimananisha "Cyndi mwenye moyo" Cyndi Le Couer. Jina la chumbani, Mopao anamwita Cyndi "Le Couer De la Mer" yaani "Kwenye moyo/shina la bahari". Yeye Mopao ni bahari. Sio umbea sikiliza "Koukoulou" utasikia maneno hayo ya chumbani, wakiitana.

Bila shaka unamkumbuka Sam Tshintu na Suzuki Luzubu kama pivotal figures kwenye kwenye album mbili za mwaka mmoja 1997 ya "Loi" na "ultimatum". 😁

Gone are the days.
Mkuu nmependa uchambuzi wako maridhawa...ila nikuulize nmewahi kusikia Cindy alikua anakulwa na fally ipupa kipindi Fulani fally akiwa QL ..
 
Kumekuchaa.. Ukiwa na stress zako usizilete huku tafadhali utadharaulika na mpaka watoto wa jana
Hunaga akili ingawa unadhani unazo. Nimeshangaa umepost uharo bila kujiridhisha na unachopost kama ni sahihi.
Naona kama una chuki binafsi na mshana mbona mada haiitaji hata kua na hasira kujibu hata kama Kuna makosa ya information..tena mada yenyewe ya burudani mziki tena mziki wa Congo...hii haifai hata kidogo,,mambo haya madogo kama ni mtu mzima unaejitambua unamuelewesha mtu bila matusi na fedheha..unakua kama mtoto bwana ..au mwanamke mwenye wivu ..wanaume hatunaga hayo mambo
 
Nimekusoma vizuri sana. Hongera brother.

Ninaweza kusikiliza siku nzima nyimbo za huyo mzee.

Mopao na QL ni urithi wa Congo (Heritage) kama ilivyo kwa Le Grand Maitre Franco Luambo Makiadi na TP Ok Jazz. Mopao ana diplomatic passport kama Balozi wa Utamaduni wa Congo, akipewa na serikali ya Tshisekedi.
 
Mkuu kwa nyongeza ni kwamba, Antoine Agbepa Mumba alias Koffii Olomide, amewahi toa album mbili mwaka mmoja, zikawa gumzo na zikashinda Kora Awards.
Album hizo ni "LOI" (LWAA) yaani sheria, 1997.
"Ultimatum" 1997 yaani kauli ya onyo.
Heshima kubwa kwako Mkuu, naamini hata hilo jina lako Chivundu umelitoa kwenye kibao cha Loi pale kwenye kibwagizo anasema Chiiivunduuuuuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom