Koffi Olomide na Mkewe Cindy Le Couer

Koffi Olomide na Mkewe Cindy Le Couer

Wajue watu wanaompa Mkongwe KOFFI OLOMIDE Nguvu ya Kudumu kwenye Muziki wa Afrika Takribani Miaka 40 Leo..

Wanasema Penye Mafanikio ya Mtu lazima kuna Connection au Mchakato flani wa kueleweka.

Hawa ndiyo Miamba tegemeo la Koffi Olomide.

1-Mkewe, Cindy le Couer. Huyu ndio kiungo, siyo muhimu Bali ni kiungo wa LAZIMA...

2-George Weah Wakawaka, DJ na Mtayarishaji Wa Muziki kutoka Yaunde Cameroon 🇨🇲.

2-Boss Batuta, Mzee Wa New York. Matamasha mengi ulaya na America Kiungo ni huyu.

3-Jean Baptiste Ilunga AKA Sundiata Keita. Huyu makazi yake Brussels, New York na Paris.. Unaambiwa Jamaa mwaka mzima anazunguka kwenye matamasha kwa wasanii wake anaowasimamia.

4-Tchacho mumbala. AKA Jamal Kashogi, huyu ni P. Funk wao, na pia ni Mpishi wa Mitindo mingi unayoiona na kusikia kwa KOFFI OLOMIDE na Mkewe CINDY.

5-Bestinne Sandra Kazadi. Huyu ni Bilionea wa Kinshasa, na alipata Kuwa Rais wa AS VITA CLUB, mpaka 2023.Ndiyo chimbo la KOFFI OLOMIDE kwenye Mambo ya pesa. Yaani ndiye GSM wake panapohitajika Neno la kipesa.

6-Tonny Muamba. Huyu ni Kiungo mwingne anayehakikisha KOFFI OLOMIDE na CINDY wanakuwa Bora muda wote. Ni mmiliki wa Mahoteli na Kumbi za Starehe Katika miji ya Paris, Marseille, Brussels na New York.

7-Davids Mumbele Matandi. Bilionea mwingne aishiye Paris kipenzi cha Koffi Olomide, huyu ndiye spea tairi ya Kila Shida analohitaji Koffi ikiwa atahitaji. Na ndiye mshauri wa tenda mbali mbali anazoingia Koffi ndani na Nje ya Congo.

8-Adolf Muteba Chilawena. Ni Zambia mwenye asili ya CONGO. Ni Promota mmoja wapo wa Koffi na ukitaka kufanya kazi na Koffi UK I mpaka Muteba akakubali Bali utakuwa umempata Koffi kwa 80%

Na Wengine Wengi, Lakini baadhi Yao ni Jean Marie Mukulasie, Bakari Manyiema, Koko Mongo Simba. Bi Salome Jose kosesa a.k.a (Mourinho).J.J Alinas. Ngaiwa Imboka, Jean Marie Nkubala, Roger bukana, Floyd Masamba, Fading Mamona, Blaise Samba na wengine Florente Ditovelle Mangani Gadi Ramadhani. Na wengine.

Bila kuwasahau watoto wake wapenzi
1-Didi Stone Olomide (Washington)
2-Del Piero Mourinho Olimide
3-Minou Olomide
4-Aristote Olomide
5-Rock Olimide.

GAVANA@2025

Mwongo mkubwa wewe. Kama kitu hujui uwe unauliza. Mambo mengi umeandika uongo mtupu kama stori za vijiweni.

1. George Weah anayetajwa na Koffi ni huyu mchezaji na rais wa zamani wa Liberia. Koffi hajawahi na hana Mtayarishaji wa muziki mwenye hilo jina.

2. Tatcho Mbala ni mjasiriamali na mfanyabishara wa DRC na sio music producer.

3. Bestine Kazadi ni waziri huko DRC na Sandra Kazadi ni mpwa wa Koffi. Hawamfadhili pesa Koffi.
 
kumekucha
 
Cindy siyo poa hata kidogo. Aliingia kwenye kundi kama mwanamuziki wa kawaida! Ila kidogo kidogo akaanza kupanda cheo mpaka kufikia cheo cha juu kabisa cha kuwa Bosslady wa kundi.

Unaambiwa Mzee Baba Koffi humwambii kitu kwa Cindy. Yaani kama mimi tu huniambii kitu kwa babe wangu SweetyCandy!!
Yaan toka niijue hii story imebidi nirudi kusikiliza tena kile kibao aseeh. Kumbe sio Diamond na Zuchu peke yao hata Koffi na Cindy ndio mambo yao
 
Ni sahihi mkuu, japo umemsahau Marehemu AHMED BAKAYOKO aliyekuwa PM Ivory Coast. Mapenzi yangu kwa Muziki wa Koffii ni makubwa sana. I grew up listening to his music.
Tunaweza kuzungumza kila albam ya Koffie kwa miaka yote 40 ya carrier yake, tusiache kitu. 😁
Ninapousikiliza wimbo wake “Loi” kuna kipande anasema “Tshivundu” nakua nakumbuka ID yako.. au nikiona ID yako nakumbuka hicho kipande kwenye huo wimbo😅
 
Mwongo mkubwa wewe. Kama kitu hujui uwe unauliza. Mambo mengi umeandika uongo mtupu kama stori za vijiweni.

1. George Weah anayetajwa na Koffi ni huyu mchezaji na rais wa zamani wa Liberia. Koffi hajawahi na hana Mtayarishaji wa muziki mwenye hilo jina.

2. Tatcho Mbala ni mjasiriamali na mfanyabishara wa DRC na sio music producer.

3. Bestine Kazadi ni waziri huko DRC na Sandra Kazadi ni mpwa wa Koffi. Hawamfadhili pesa Koffi.
Umeandika kishari sana.Be easy!
 
Mafanikio ya mtu ni mtu mwenyewe na umimwengu wa roho aliojiunga nao basi. Hao wengine hufuata tu bila ya kujua ni nini kilichonyuma.
 
Mwongo mkubwa wewe. Kama kitu hujui uwe unauliza. Mambo mengi umeandika uongo mtupu kama stori za vijiweni.

1. George Weah anayetajwa na Koffi ni huyu mchezaji na rais wa zamani wa Liberia. Koffi hajawahi na hana Mtayarishaji wa muziki mwenye hilo jina.

2. Tatcho Mbala ni mjasiriamali na mfanyabishara wa DRC na sio music producer.

3. Bestine Kazadi ni waziri huko DRC na Sandra Kazadi ni mpwa wa Koffi. Hawamfadhili pesa Koffi.
Sometimes unakuwa kama demu aliyepigwa kibuti au ambaye yuko kwenye siku zake😂😂🤣
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom