Tena aliniacha kinyama Sana,
Kuna simu yake fulani iliharibika kioo,
ikabidi anipe nimbadilishie kioo,
Baada ya simu kupona, nikagunduwa madudu mengi Sana kwake kupitia phone's sms ambazo zilibaki kwenye simu yake.
Baby mbona Jana nimekuwekea chakula lakini umesusa ?
Najuwa hunipendi Ila mimi nakupenda Sana kuliko mwanaume yeyote..
Hakika wewe ndy chaguo langu.
Moja Kati ya sms zake niliizozikuta kwenye simu yake ,
Kwa kwl niliumia sn..
Nikiangalia hata pesa ya Kodi ya chumba anapoishi nalipa Mimi.
Baada ya kucopy namba ya yule jamaa mlengwa ,,
nikaamua kumpigia simu,
Jamaa akafunguka kwamba hana mipango na yule demu zaidi ya kugegeda tu.
Nikarudi kwa yule mrembo wa chuo kumpigia simu.
Nikamuuliza kuhusu SMS na nimempigia jamaa amekiri kuwa na mahusiano.
Kabla hajakaa simu yangu
Akaniambiya ,,
Sasa Mimi nikusaidiaje kwa Mfano?
Ndy mwisho wa mapenzi yetu hadi sasa mwaka wa 11 sijawahi kumuona hata kwa bahati mbaya.