Mkuu kwanza hongera kwa bahati (au jitihada) ya kipekee kuishi nje ya Tanzania. Pili, sidhani kama kiingereza kinapuuzwa hapa Tanzania na ndio maana kwanza kinafundishwa kama somo ngazi za awali na ndio lugha rasmi ya kufundishia ngazi ya sekondari na kuendelea.
Pili kulegalega kwa kiingereza isichukuliwe ni kutokana na kupuuzwa kwake kwani hata hicho kiswahili chenyewe wala hakina au hakifundishwi kwa ubora unaotakiwa.
So, generally, tatizo halipo kwenye kiingereza bali tuna tatizo zaidi ya lugha. Ni almost kila kitu hatukiwezi karibu kila nyanja ya maisha. Kwa mfano, hivi hata kuweka mazingira yetu safi ili tusisumbuliwe na kipindupindu kila wakati tunahitaji kiingereza? Hivi kondakta wa daladala anahitaji kujua kiingereza ili asimnyanyase mwanafunzi? Hivi tunahitaji kujua kiingereza ili tusijisaidie ovyo mitaani? Hivi tunahitaji kujua kiingereza ili tusikwepe kodi au kuiba mali ya umma, ufisadi, n.k?
Tatizo sio lugha bali mfumo. Na mfumo, nionavyo mimi, unahusisha tabia zetu, desturi zetu, siasa zetu, mila zetu (imani za kishirikina, n.k.), mahusiano yetu, na hata dini zetu. Kama wachina waliweza kwa lugha yao na "sasa hivi" ndio wanajifunza lugha za kigeni kwa nini sisi tushindwe? Ni maoni yangu.