Wabongo tunachanganya mambo ndio maana tupo nyuma kwa kila kitu

shadrackAmri

Member
Oct 27, 2023
5
3,144
Unakuta mataifa mengine yalioendelea jinsi wanavyojadili mambo yao kwenye mitandao ya kijamii unafurahi.

Mfano wachina mtu akiweka video yake ya kuelezea kitu fulani Kwa lugha ya kichina wanaokuja kutoa maoni yao(wachina)wanatumia zaidi lugha ya kichina.

Hivyohivyo kwa wakorea wanatumia lugha yao kutoa ujumbe/maoni kwenye mitandao wanapojadili kitu.

Wabongo sasa mfano bongozozo na wazungu wengine wanaopenda kuongea Kiswahili kwenye mitandao hasa TikTok unakuta kaweka video yake ambayo kaongea Kiswahili mwanzo mwisho wabongo wanakuja kutoa maoni yao kwa kiingereza😁😁😁mzungu anajitahidi kumjibu kwakiswahili mbongo hastuki anaandika tena ujumbe kwakingereza

Unakuta jumbe nyingi sana kwenye hio video nizakiingereza wakati alieweka video katumia kiswahili na nimzungu ámbae kingereza anakijua vuzuri sana ila kakiacha akaamua kutumia kiswahili

Sasa wabongo wenzangu nawafundisha ukiona sehemu imetumika kingereza tumia kingereza ukiona kimetumika kiswahili tumia kiswahili ukiona kimetumika kichina tumia kichina sawa?

Acheni kuchanganya mambo
 
Kwa wanaume wenzangu: Nimeingia Google kucheki maana ya TikTok, ni mtandao wa kijamii ambao watumiaji wana share video mbalimbali na wengine wana comment like etc. Najua wengi hamuujui.
 
Back
Top Bottom