Kiswahili kinaliangamiza taifa

Kiingereza ni lugha ya kimataifa, kiswahili ni kitanzania. Kwa uhuru wa kuuelewa utandawazi kwa mapana yake, tusijidanganye, kiingereza kinahitajika mno.
Si kweli, Kiswahili ni lugha ya kimataifa. Hata umoja wa nchi za kiafrika, AU, wanatambua hilo. Hapo hakuna ubishi! Tatizo letu ni kasumba za kikoloni. Bado mawazo ya kuabudu wazungu yametutawala kiasi cha kwamba kila chetu tunakiona duni.
 
Ulichosema ni ukweli mtupu, ila tegemea kushambuliwa na watu ambao hawako tayari kuukubali hii fact. Tegemewa kuambiwa Wachina, Wajerumani, Wajapani, Wafaransa wanaongea lugha zao na wanaendelea.

Vile vile subiri kuambia kuwa unawaabudu wazungu.

Na mwisho kabisa, tegemea kuambiwa kuwa Nyerere aliasisi lugha takatifu ya Kiswahili - kwa hiyo anayekipinga anatenda dhambi kwa Mnyaz Mungu.
Mbona unajishtukia?
 
Ndugu yangu mimi nakaa nje ya Tanzania kwa miaka mingi sasa. kabla ya kuondoka Tanzania nilikuwa proud sana na kiswahili lakini baada ya kukaa nje nimegundua viongozi wetu walikosea sana kusisitiza kiswahili na kupuuza kiingereza...
Hapa nashindwa kukuelewa. Nami nipo nje ya Tanzania kwa miaka zaidi ya thelathini sasa lakini ndio ninazidi kukithamini Kiswahili, zaidi ya vile nilivyokuwa ninakithamini nilipokuwa TZ! Kwanza sio nchi zote za Ulaya zinazungumza kiingereza na bado zimeendelea, kwa hiyo acha kupotosha kwa sababu za kutokujiamini.
 
Tatizo tulonalo hasa nchi za kiafrika ni mawazo ya kiutumwa ambayo bado hayajatutoka.Tunaona kuiga mambo ya wazungu ata kama ni mazuri eti utumwa. Nani anakwambia kujifunza na kuongea kiingereza ni UTUMWA?
 
Si kweli, Kiswahili ni lugha ya kimataifa. Hata umoja wa nchi za kiafrika, AU, wanatambua hilo. Hapo hakuna ubishi! Tatizo letu ni kasumba za kikoloni. Bado mawazo ya kuabudu wazungu yametutawala kiasi cha kwamba kila chetu tunakiona duni.

Acha uongo, nani amekwambia kiswahili ni lugha ya kimataifa.Wewe ndo unamawazo duni ya kitumwa hutaki kuiga mambo mazuri ya wengine kisa unawaza utumwa!
 
Ninaomba kuanzisha hii mada baada ya kusikia kwamba kuna mahali walimu wamefukuzwa kwa sababu ya kuongea kiswahili katika mazingira ya shule.
Niseme tu kwamba naunga mkono jambo hilo kwa asilimia mia. Sababu ni hizi hapa.

1. Tutambue kuwa kiswahili ni lugha inayozungumzwa sana Tanzania na ukitoka nje ya mipaka ya Tanzania kiswahili chako unaweka mfukoni! Lazima tujufunze lugha za kimataifa(English) ili tulahisishe mawasiliano na mataifa mengine.

2. Wageni wakija Tanzania wanapata taabu kweli, matangazo ya biashara yameandikwa kwa kiswahili, barabara nazo unakuta vibao vimeandikwa kwa kiswahil mfano PITA KUSHOTO. Sasa jamani wageni wetu ambao wengi wanakuja kwa maswala ya biashara inakuwa ngumu sana.Mgeni kuendesha gari tanzania ni ngumu sana. Mgeni kufanya biashara Tanzania ni ngumu sana!! Kuna jamaa wafanyabiashara wengi sana nawafahamu wanaprefer kwenda Kenya na Uganda kuchukua bidhaa kuliko Tanzania na sababu wanazozitoa ni ugumu wa Lugha.wanasema kwenda Tanzania ni gharama zaidi maana inabidi umtafute mkalimani ambaye utamlipa.

3. Kenya inatangaza mlima kilimanjaro kwa sababu ya Lugha wanayotumia inaeleweka duniani kote. Sisi tunatangaza mlima kilimanjaro kwa kiswahili wataelewa nini wageni?

4.Tunawasanii wazuri sana wa muziki, tamthiliya, vichekesho, ambao wangesaidia sana kuitangaza nchi yetu kimataifa na wao pia kufaidika, lakini wamebaki eti wasanii wa BONGO. (Kwa wale mliobahatika kuangalia stand up Zambia kilichorushwa na Africa magic channel mtakubaliana na mimi wale jamaa 3 walioshinda sasa hivi ni comedian wakimataifa wanazunguka nchi mabalimabali sababu ni lugha tu, maana kwa ukweli hawawezi kumfikia Joti, Masanja.

5.Tuna wachungaji wazuri sana(Pastors) lakini mahubiri yao ni kwa kiswahili. T.B Joshua anajulikana kila mahali kwa sababu mahubiri yake ni ya kiingeraza. Si kwamba Joshua unaupako kuliko wengine.

6. Mikataba mibovu tunayoingia na wawekezaji ni kwa sababu ya lugha tunashindwa kuilewa vizuri Wawekezaji wanapokuja ilitusionekane ni mbumbumbu wa kiingereza tunabaki kusema YES, YES YES!

7. Kwa watazamaji wenzangu wa aljazeera kuna kipindi kinaitwa 'Tea cafe (kama sijakosea)kinaongelea maswala mbalimbali yanayohusu nchi husika kipindi hicho kinapofanyika. Kipindi hicho kimefanyika,Kenya, Uganda zambia lakini Tanzania hakuna na hata katika ratiba yao Tanzania haimo simply because hakuna watu kama wanasiasa na baadhi ya watu mahalufu ambao wako tayari kujadili kwa kimombo! Sasa dunia itatuelewa vipi matatizo na mipango yetu ?

Nchi nyingi sasa hivi zinajifunza Kiingera hata china taifa kubwa wako busy kujifunza kiingereza Sisi masikini wakutupwa tunangangana na kiswahili ambacho mwisho wake ni mipakani tu! Viongozi wetu lazima pia waanalie hiyo watu waanza kufundishwa kiingereza tangu chekechea, maofisini lugha ya kiingereza isisitizwe, mikutano maofisini ifanyike kwa kiingereza. WITHOUT ENGLISH YOU ARE MARGINALIZED YOURSELF

Unajua ni kama vile kijana aliyeshindwa na maisha na kuanza kumlaumu baba yake kwamba ni chanzo cha yeye kuwa na maisha magumu, kwa hiyo mimi nafikikiri wewe maisha huko uliko yamekupiga sasa unatafuta wa kulaumu naona umepata mnyonge wako kiswahili.

Fanya kazi jitume acha kupigania na kupoteza muda kwa vitu ambavyo hata ufanye nini huwezi kubadilisha Kiswahili kina zaidi ya miaka 1000 hapa kwetu, kimepitia mengi, sio wewe wa kwanza kuanza kukipinga na wala hautakuwa wa mwisho, watu walikuwa mpaka wanavishwa kengele mgongoni kwa kwamba your stupid kwa maana umeongea kiswahili, nchi zimetumia mabilioni ya fedha kukipinga kisisambae, unajua matokeo yake nini, Kiswahili kinazidi kukua, kukua na KUKUA, leo hii kila nikienda kijijini watoto wadogo wa chekechea ambao zamani walikuwa wakicheza kwa kuongea kilugha leo wanacheza kwa kiswahili, hiyo inamaanisha nini? kuna mtu anashindwa vita!

Fanya kazi utafanikiwa acha kulaumu!

Mimi sijakipinga kiswahili. ninachopinga ni mfumo huu wa kiswahili. tuige wenzetu wakenya ,waganda,wamalawi, zimbabwe, south africa n.k. Nchi hizi pamoja kwamba zinalugha zao lakini pia wanazungumza kiingereza sababu wametambua umuhimu wa lugha hii ya kiingereza na ndio maana communication inakuwa rahisi na mataifa mengine hivyo kuongeza kasi ya maendeleo. Sisi ni kiswahili tu, hivyo tunapunguza kasi ya maendeleo sababu mawasiliano yanakuwa magumu. Tujifunze mambo mazuri ya wenzetu ili nasi tusiachwe nyuma sana
 
Acha uongo, nani amekwambia kiswahili ni lugha ya kimataifa.Wewe ndo unamawazo duni ya kitumwa hutaki kuiga mambo mazuri ya wengine kisa unawaza utumwa!
Duh, bado una safari ndefu. Kwa wewe kimataifa inamaanisha nini? Kiswahili kinaongelewa kwenye zadi ya mataifa kumi barani Afrika na kinafundishwa katika vyuo vya mataifa mbali mbali duniani. Umoja wa Afrika (AU) wameshapitisha Kiswahili kuwa ni lugha rasmi ya umoja huo. Nadhani wewe bado una mawazo duni sana na itachukua muda mrefu kujikwamua. Pole. Siwezi kukusaidia!
 
Tatizo tulonalo hasa nchi za kiafrika ni mawazo ya kiutumwa ambayo bado hayajatutoka.Tunaona kuiga mambo ya wazungu ata kama ni mazuri eti utumwa. Nani anakwambia kujifunza na kuongea kiingereza ni UTUMWA?
Ni wapi nimeongelea utumwa, au ni wewe ndio una mawazo ya kitumwa kwa hiyo ndio maana unajistukia haraka kabla watu hawajakuambia?
 
Mimi sijakipinga kiswahili. ninachopinga ni mfumo huu wa kiswahili. tuige wenzetu wakenya ,waganda,wamalawi, zimbabwe, south africa n.k. Nchi hizi pamoja kwamba zinalugha zao lakini pia wanazungumza kiingereza sababu wametambua umuhimu wa lugha hii ya kiingereza na ndio maana communication inakuwa rahisi na mataifa mengine hivyo kuongeza kasi ya maendeleo. Sisi ni kiswahili tu, hivyo tunapunguza kasi ya maendeleo sababu mawasiliano yanakuwa magumu. Tujifunze mambo mazuri ya wenzetu ili nasi tusiachwe nyuma sana

Mimi mbona sikuelewi tatizo lako hasa ni nini? Kama swala ni mawasiliano mbona wageni wengi tu Tz na wanaishi, sehemu kubwa ya watz sasa hivi hapa tz wanafanya kazi makampuni ya kigeni na wanatumia kiingereza, sasa ulitakaje zaidi ya hapo?
Hivi ulishasikia kampuni kubwa Duniani imegoma kuja kuwekeza Tz kwa sababu watu hawajui kiingereza? Kama hawaji au kama wapo na wameamua kuondoka ni kwa sababu nyingine kabisa na hazihusiani na kiingereza au Kiswahili!

Na hapo kwenye mawasiliano bahati nzuri hizo nchi zote ulizozitaja nimebahatika kufika na nazijua vizuri isipokuwa labda Zimbabwe na ninakuhahakishia hata huko mawasiliano bado ni tatizo tena kubwa zaidi kuliko hapa kwetu kwa maana kwa maana Tz ukijua Kiswahili uko safe na unaweza kuzunguka karibu nchi nzima na kufanikisha kazi zako, hizo nchi nyingine wanaojua kiingereza ni wachache sana (usiangalie miji mikuu) na waliobaki wote wanaongea lugha nyingine kwa hiyo ina maana kama wewe ni Mganda au sijui Mzambia akitaka kwenda wilayani huko ni lazima upate mkalimani ingawaje yumo ndani ya nchi yake! Sasa sijui nani ana afadhali hapo kati yetu sisi na wao!

Kwa kwa kifupi hali hapa kwetu sio mbaya sana kama unavyofikiri kuwa tu na amani endelea kupiga kazi na tujenge Tanzania yetu inawezekana tukiamua!

Kutoa nafasi ya Kiswahili na kuleta Kiingereza au Lugha nyingine hapa Tz haiwezekani na haitowezekani kamwe kwa sababu za kihistoria, kumbuka wazungu walijaribu sana wakashindwa wakaamua tu kukikubali kiswahili na kukichukulia kama kilivyo leo hii watz wengi wanafaidika nacho wengine wanafanya kazi mara BBC, wengine radio Japan, wengine radio china, wengine VOA Marekani wengine wanafundisha Kiswahili vyuo vikubwa mbalimbali Duniani na huwezi jua labda na wewe siku kitakuja kukusaidia mahali kama sio wewe basi labda ndugu ama jamaa yako!
 
Naomba nikuulize maswali yafuatayo:
Je, ni lugha gani kati ya kiingereza na kiswahili, inamchango mkubwa katika maendeleo ? na ni kwa nini?
 
Naomba nikuulize maswali yafuatayo:
Je, ni lugha gani kati ya kiingereza na kiswahili, inamchango mkubwa katika maendeleo ? na ni kwa nini?
Mimi naona hatuelewani na tunaongea vitu viwili au labda 3 tofauti, sasa umetoka kwenye Lugha unakuja kwenye mambo ya maendeleo hiyo nayo ni topic inayojitosheleza na ni ndefu sana, tukubali kutofautiana na tuendelee kujenga Tanzania yetu!
 
Uyu jamaa Masauni naona sasa kachanganyikiwa!
 
Acha uongo, nani amekwambia kiswahili ni lugha ya kimataifa.Wewe ndo unamawazo duni ya kitumwa hutaki kuiga mambo mazuri ya wengine kisa unawaza utumwa!

Masauni
Kiswahili ni lugha ya kimataifa.

Vipi lugha inakuwa ni lugha ya kimataifa? Au nini kinafanya lugha iwe ni lugha ya kimataifa?

Kuna hii link ukipitia basi utashawishika kuwa Kiswahili tayari ni lugha ya kimataifa na inasambaa kwa kasi.

6 KISWAHILI AS AN INTERNATIONAL LANGUAGES: RECENT DEVELOPMENTS
On the international level, Kiswahili has scored more marks than was thought possible twenty years ago. Kiswahili is now spoken or understood by about 80-100 million people in the following countries:.......

Education
Kiswahili is taught as a language in more than 100 (my estimate) universities and higher education institutions in worldwide. This estimate does not include the many African-American black schools in the U.S.A that teach Kiswahili as a second language to black students. Most of the universities teaching Kiswahili are in the U.S.A, but there are also famous schools of Kiswahili in U.K. (SOAS), Germany (sevaral universities), Russia (St Petersburg and Moscow State University), France, Belgium (Gent and Antwerp), Italy (Naples), Switzerland, Austria, Netherlands, Poland, Norway, Sweden and Finland, China, Japan, Oman and Mexico. Within Africa, Kiswahili is taught in more than 10 universities in Tanzania, Kenya, Uganda, DRC, Madagascar, Ghana, Sudan, Nigeria and Libya. Though it is not possible at this point to
give an estimate of the number of students, it is safe to assume that Kiswahili is the most widely taught African language in the world.

The media and publishing
Kiswahili is used in more than 100 radio and TV broadcasting stations worldwide. About ten of these are in Tanzania and Kenya. Other African countries that broadcast in Kiswahili include DRC, Rwanda, Burundi, Egypt, Iran, Sudan, Uganda, South Africa. Many Asian and European countries also broadcast in Kiswahili. In America, apart from the Voice of America, there are many black FM radio stations that have Kiswahili programs. The Swahili services of the BBC, Deutsche Welle and Voice of America appear to have the widest reach. In book publishing, Kiswahili has been the favourite target language of translations from different world literatures. In the nineteenth and early twentieth
centuries, numerous books from English, French and Arabic were translated into Kiswahili. At the height of communism, many books from China, North Korea and the Soviet Union were also made available in Kiswahili.

Link H-Net Discussion Networks - Kiswahili as a National and International Language=

Pia hapa :link http://www.njas.helsinki.fi/pdf-files/vol15num2/mukuthuria.pdf
The development of Kiswahili language from a minority language in the 18 th. C. to an international language can be attributed to many factors. These include ...
 
Mimi naona hatuelewani na tunaongea vitu viwili au labda 3 tofauti, sasa umetoka kwenye Lugha unakuja kwenye mambo ya maendeleo hiyo nayo ni topic inayojitosheleza na ni ndefu sana, tukubali kutofautiana na tuendelee kujenga Tanzania yetu!
Ni kweli naona hatutaelewana maana tunatofautiana ufahamu. Unashindwa kuelewa usiano uliopo kati ya lugha na maendeleo and that is my argument from the beginning. Lugha as a means of communication inamchango katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja, society, taifa na kimataifa. Ndio maana nimekuuliza kama unakubaliana na mimi kwamba lugha inamchango katika maendeleo, nambie kati ya kiingereza na kiswahili kipi kimechangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo iwe ya mtu mmoja mmoja, kikundi au taifa. (Kama hujui kulink lugha na maendeleo basi usijibu)
 
Kiswahili hakiangamizi taifa. Tatizo ni mfumo wa elimu hata kiswahili kina matatizo ya kielimu angalia makosa hata kwenye hii JF. Tuweke mfumo ambao tutajifunza kiswahili na kiingereza sanifu kwa wakati mmoja kuanzia shule za awali mpaka chuo kukuu. Tena tukifanya hivyo watu wetu watafaidi sana kwa sababu watoto ni rahisi sana kujifunza lugha zaidi ya moja bila shida. Lugha ya taifa muhimu jamani.
 
Masauni,

..umesema ukweli 100%.

..mbona Nyerere alikuwa anazungumza Kingereza vizuri mno?

..kuna dhambi gani na sisi kukimudu Kiingereza kama Baba wa Taifa?

..we r really limiting and isolating ourselves by not learning and mastering english.

..wenetu wanakosa kazi kwa kutokujua kiingereza.

..Uchumi wa India umeibuka na kupaa kutokana na matumizi ya lugha ya Kiingereza na utaalamu wa IT.

.
 
Last edited by a moderator:
Nenda uchina halafu nioneshe mtaa hata mmoja wenye mabango kwa lugha tofauti na kichina. Mabango na matangazo yote China ni kwa ki-China (Mandarin) kama lugha ya kwanza; pale ambapo ni lazima sana ndipo wanapoweka lugha nyingine. Kama huelewi kichina, tafuta mkalimani na wako hadi ma-profesa wanatembeza watalii na wageni wengine.

Lugha imesaidia sana kama suluhisho la tatizo la ajira kwa mamilioni ya wachina. Elimu ni pamoja na kutumia "fursa" zilizopo kupambana na umaskini na wachina wamefanikiwa mno katika hili. Tafakari.

Kulinganisha China na Tanzania si sawa.

China ilinganishwe na bara zima la Afrika, si Tanzania.

Kiuchumi, wingi wa watu etc, China inaipita Afrika nzima kwa ujumla, sasa wewe unaona sawa kulinganisha China na Tanzania?
 
Kiswahili ni Muhimu sana, Lakini Kiingereza ni muhimu zaidi Hasa kwa nchi changa na masikini kama Tanzania ambayo inategemea kila kitu kutoka Nje (Tofauti na zilivyo hizo developed countries zinazodumisha lugha zao zaidi).Maandalizi ya kutumia zaid lugha ya kiswahili pekeyake yanahitaji gharama kubwa na maandalizi ya muda mrefu sana.
Kuna mahusiano makubwa ya matumizi ya Lugha za Kigeni (mfano kiingereza) kutokana na utegemezi wetu kwa haya mataifa makubwa kwenye nyanja kama Elimu zetu, Utaalamu, Biashara za kimataifa,Mahusiano ya kimataifa, Utalii, Uwekezazi na Utandawazi.
 
Mkuu mbona unaleta story za kusadikika? weka reference. Ndugu yangu tembea uone!! inawezekana wewe umezaliwa Dar, umesoma Dar, Umepata kazi dar, umeoa ukiwa dar. Ulimwengu unaoufahamu ni Dar es salaam tu!! Katika karne hii ya Science na teknolojia, tunahitaji lugha ya kimataifa. Ninawafahamu wasomi wazuri sana wa kitanzania ambao walishindwa kuiwakilisha Tanzania katika nyanja za utafiti na sayansi nje ya nchi kwa sababu ya lugha ya kiingereza lakini mkiwa mnajadili kwa kiswahili ni vichwa si mchezo.

Leo katika jumuia ya africa mashariki tunawaogopa sana wakenya na waganda(pamoja na sababu zingine lakini pia Lugha inachangia tuwaogope tukijua kwamba kupata kazi katika nchi hizo bila umombo ni ngumu)
Lugha ya kiiingereza ni pana sana na ndio maana inakuwa rahisi kufundishia kuliko kiswahili amabacho si kipana.
Sasa naanza kuwa na mashaka na upeo wako wa elimu. Ukiona vyaelea ujue vimeundwa, hivyoni pia katika lugha. Ukiiona inachanua ujue wapowatu waliofanya juhudi za ziada kuijenga na kuifanya unavyoiona. Wewe unataka "Ready Made" kuanzia kitambaa cha kufutia jasho hadi lugha! Nashangaa sana na mawazo yako yenye tafakuri finyu kabisa. Mimi sikukulia Dar kama unavyodhani na nimezunguka zaidi ya nchi 15 na hadi sasa niko nje ya Tanzania na huku ndiyo nimeona athari za kukumbatia vya watu! Ingekuwa kujua kiingereza ndiyo ufunguo pekee wa maendeleo wataaliano, wa Hungary, wa Romania, wa -Giriki, wa- Taliano woote wangekuwa wakitumia Kiingereza kama lugha zao rasmi! lakini sivyo kila mmoja anajivunia lugha yake na kuendeleza juhudi za kuiboresha. Lakini wewe umebweteka na kusubiri uendelee kwa kufanya juhudi za kukijua kiingereza pekee! Shame on you!
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom