ndugu yangu unayo yasema huyajui, hata huko nje ya nchi uliko sijui ni wapi! mimi kwa sasa niko uholanzi, hawa jamaa ni kidachi kwa kwenda mbele, kingereza kinatumika mara chache saana katika sehem maalum zinazo husisha watu wa mataifa mengine, shule zote ni kidachi, wanashangaa kwa nini sisi tunasoma kwa lugha ya kiingereza!
nimekuwa mwalim najua namna walim wanavyo pata shida kufundisha kwa kiingereza, wanafunzi wanapata shida uelewa kwa sababu wanafikiria kwanza kwa kiswahili wanatafsiri ndo waanze kupata maana, ni kosa kubwa saana tulilotenda kuacha kiswahili kisitumike ktk mashule yetu.
Mara ngapi tumeshindwa kupata tafsiri halisi ya matatizo yetu kwa kikwazo cha lugha!
Halafu kumbuka kiswahili pamoja na kudidimizwa bado ni kati ya lugha kubwa duniani inayotumika tanzania, kenya, uganda, congo, rwanda, burundi, na nchi nyingi za afrika, tunge kithamini kingeweza kutuweka pazuri. Mataifa yote yenye nguvu sasa yanatumia lugha ya kwao!
kuthamini lugha ya kigeni ni ukoloni wa aina fulan kama tutakuwa makini kuchunguza, sisemi kwamba tuache kabisa lugha za kigeni, ni muhim kujifunza kwa sababu ya globalization ila tukumbuke siyo ligha zetu!
kunamsemo unasema "kitaka kumtawala mtu haribu, utamaduni wake" kumbuka lugha ni kiungo muhim saana katika kutunza utamaduni wa mahali, nafikiri wewe pia wa weza kuwa shuhuda kwa sasa Tz tusivyo kuwa na utamaduni wa kueleweka, uzungu si uzungu! uafrika si uafrika! watu kutaka kuishi kiingereza engereza! ndio kuliko badirisha style za watu kuongea, kuvaa, kutembea na tunathamin vyovyote wanavyo fanya wazungu kwa sababu tumedharau vya kwetu! kwa mfano utashangaa dada zetu siku hizi wanalazimisha kuvaa stockings na joto la dar lilivyo!!!!!! huku wenzetu wanavaa hivo kwa sababu ya baridi!!!!!!!!!
Ninasikitika mtu anaposisitiza tujifunze lugha za kigeni kwa gharama ya lugha yetu!
Nakipenda kiswahili lugha ya nchi yangu