Kiswahili kinaliangamiza taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili kinaliangamiza taifa

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Masauni, Aug 5, 2012.

 1. M

  Masauni JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninaomba kuanzisha hii mada baada ya kusikia kwamba kuna mahali walimu wamefukuzwa kwa sababu ya kuongea kiswahili katika mazingira ya shule.
  Niseme tu kwamba naunga mkono jambo hilo kwa asilimia mia. Sababu ni hizi hapa.

  1. Tutambue kuwa kiswahili ni lugha inayozungumzwa sana Tanzania na ukitoka nje ya mipaka ya Tanzania kiswahili chako unaweka mfukoni! Lazima tujufunze lugha za kimataifa(English) ili tulahisishe mawasiliano na mataifa mengine.

  2. Wageni wakija Tanzania wanapata taabu kweli, matangazo ya biashara yameandikwa kwa kiswahili, barabara nazo unakuta vibao vimeandikwa kwa kiswahil mfano PITA KUSHOTO. Sasa jamani wageni wetu ambao wengi wanakuja kwa maswala ya biashara inakuwa ngumu sana.Mgeni kuendesha gari tanzania ni ngumu sana. Mgeni kufanya biashara Tanzania ni ngumu sana!! Kuna jamaa wafanyabiashara wengi sana nawafahamu wanaprefer kwenda Kenya na Uganda kuchukua bidhaa kuliko Tanzania na sababu wanazozitoa ni ugumu wa Lugha.wanasema kwenda Tanzania ni gharama zaidi maana inabidi umtafute mkalimani ambaye utamlipa.

  3. Kenya inatangaza mlima kilimanjaro kwa sababu ya Lugha wanayotumia inaeleweka duniani kote. Sisi tunatangaza mlima kilimanjaro kwa kiswahili wataelewa nini wageni?

  4.Tunawasanii wazuri sana wa muziki, tamthiliya, vichekesho, ambao wangesaidia sana kuitangaza nchi yetu kimataifa na wao pia kufaidika, lakini wamebaki eti wasanii wa BONGO. (Kwa wale mliobahatika kuangalia stand up Zambia kilichorushwa na Africa magic channel mtakubaliana na mimi wale jamaa 3 walioshinda sasa hivi ni comedian wakimataifa wanazunguka nchi mabalimabali sababu ni lugha tu, maana kwa ukweli hawawezi kumfikia Joti, Masanja.

  5.Tuna wachungaji wazuri sana(Pastors) lakini mahubiri yao ni kwa kiswahili. T.B Joshua anajulikana kila mahali kwa sababu mahubiri yake ni ya kiingeraza. Si kwamba Joshua unaupako kuliko wengine.

  6. Mikataba mibovu tunayoingia na wawekezaji ni kwa sababu ya lugha tunashindwa kuilewa vizuri Wawekezaji wanapokuja ilitusionekane ni mbumbumbu wa kiingereza tunabaki kusema YES, YES YES!

  7. Kwa watazamaji wenzangu wa aljazeera kuna kipindi kinaitwa 'Tea cafe (kama sijakosea)kinaongelea maswala mbalimbali yanayohusu nchi husika kipindi hicho kinapofanyika. Kipindi hicho kimefanyika,Kenya, Uganda zambia lakini Tanzania hakuna na hata katika ratiba yao Tanzania haimo simply because hakuna watu kama wanasiasa na baadhi ya watu mahalufu ambao wako tayari kujadili kwa kimombo! Sasa dunia itatuelewa vipi matatizo na mipango yetu ?

  Nchi nyingi sasa hivi zinajifunza Kiingera hata china taifa kubwa wako busy kujifunza kiingereza Sisi masikini wakutupwa tunangangana na kiswahili ambacho mwisho wake ni mipakani tu! Viongozi wetu lazima pia waanalie hiyo watu waanza kufundishwa kiingereza tangu chekechea, maofisini lugha ya kiingereza isisitizwe, mikutano maofisini ifanyike kwa kiingereza. WITHOUT ENGLISH YOU ARE MARGINALIZED YOURSELF
   
 2. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  ndugu yangu!haya unayozungumza umefanyia utafiti kweli?hivi lugha ndio kikwazo cha sisi kuto tambulika au kuto kuwa na maendeleo?naomba nitofautiane na wewe kwa hilo.mimi na amini fikra sahihi huja kwa lugha sahihi inayoeleweka kwa jamii husika.nilisha wahi fika china,kwakweli wale jamaa ni kichina kwa kwenda mbele unaweza shindwa nunua kitu dukani au kwenda mahali fulani kwa kuwa mmeshindwa kuelewena kwa lugha lakini hebu angalia walivyopiga hatua kimaendeleo kwa kila nyanja!hivyo basi usitukuze lugha za kigeni na kuacha za kwako kisa eti hatutaendelea,jaribu kuja na mbinu mbadala ya sisi wapi tumekosea ila hili la lugha hapana!
   
 3. M

  Masauni JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ulifika china miaka gani? Nataka kukuhakikishia kuwa sasa hivi wanajifunza kwa bidii sana! Naomba ulewe hivi unaweza kuwa na ideas nzuri sana very constructive ideas lakini usipoweza kuzielezea hizo ideas kwa watu wakazielewa utamarginalized yourself. Dunia imekuwa ni kama kijiji. Maendeleo katika nchi yanaletwa katika kuwasiliana na si kuwasiliana sisi kwa sisi tu na watu wa nchi nyingine pia. Tukubali tusikubali Kiingereza ndio lugha ya kimataifa lazima tuifahamu kama tunahitaji kupiga hatua katika maendeleo
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,781
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Nenda uchina halafu nioneshe mtaa hata mmoja wenye mabango kwa lugha tofauti na kichina. Mabango na matangazo yote China ni kwa ki-China (Mandarin) kama lugha ya kwanza; pale ambapo ni lazima sana ndipo wanapoweka lugha nyingine. Kama huelewi kichina, tafuta mkalimani na wako hadi ma-profesa wanatembeza watalii na wageni wengine.

  Lugha imesaidia sana kama suluhisho la tatizo la ajira kwa mamilioni ya wachina. Elimu ni pamoja na kutumia "fursa" zilizopo kupambana na umaskini na wachina wamefanikiwa mno katika hili. Tafakari.
   
 5. M

  Masauni JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu mimi nakaa nje ya Tanzania kwa miaka mingi sasa. kabla ya kuondoka Tanzania nilikuwa proud sana na kiswahili lakini baada ya kukaa nje nimegundua viongozi wetu walikosea sana kusisitiza kiswahili na kupuuza kiingereza!! Ndugu yangu narudia tena kwa nchi masikini kama Tanzania, lugha ya kiingereza ni muhimu sana.
   
 6. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 889
  Likes Received: 311
  Trophy Points: 80
  Ulichosema ni ukweli mtupu, ila tegemea kushambuliwa na watu ambao hawako tayari kuukubali hii fact. Tegemewa kuambiwa Wachina, Wajerumani, Wajapani, Wafaransa wanaongea lugha zao na wanaendelea.

  Vile vile subiri kuambia kuwa unawaabudu wazungu.

  Na mwisho kabisa, tegemea kuambiwa kuwa Nyerere aliasisi lugha takatifu ya Kiswahili - kwa hiyo anayekipinga anatenda dhambi kwa Mnyaz Mungu.
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  aah....mi sijui bana.....kingereza tutajua taratibu....kwani haraka ya nini....kuna google translate japo na yenyewe inatranslate kiswahili cha Kenya.....tutakomajeee....
   
 8. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,584
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni nchi maskini bado hivyo tusitegemee lugha yetu kukua kwa haraka labda mtu ajifunze kea ridhaa yake na ili sisi tafanikiwe ktk nyanja mbali mbali tunahitaji kujifunza kingereza kwa namna moja au nyingine kitasaidia kujikwamua ktk hatua kadhaa tunazokutana nazo maishani
   
 9. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160


  Hapo kwenye mstari...ni kweli au urongo???

  Hivi mjerumani(mwenye uchumi unaoongoza barani ulaya) ametumia kiingereza kufika hapo alipo???!!!

  Nadhani maendeleo ni zaidi ya lugha...kama hatusomi, hatufanyi kazi kwa bidii, hatulei na kukuza ubunifu, sifikiri kama lugha pekee itatufikisha kwenye nchi ya kanaani!!!

  Nakumbuka tukiingia sekondari miaka ya mwanzo wa tisini, tulikutana na vijana kutoka Arusha School ambao walikuwa wakisakata kimombo kweli kweli...lakini baada ya muda nasi tukiwa tayari kimombo kimenza kukubali...tulikuwa level moja na hatimaye baadhi yao tukawapiku, siri ikiwa ni kujituma na kusoma kwa bidii.

  Niseme kwamba, tunakihitaji sana kizungu na kwa maneno ya Mh Lowasa, tunakihitaji kichina. Lakini bado bila ya vitu hivyo nimevitaja hapo juu...Lugha si lolote si chochote.
   
 10. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  neo colonialism!
   
 11. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana kwa kiasi fulani na mleta hii mada. Ila asisahau ule msemo 'MKATAA KWAO MTUMWA'
   
 12. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  nakuunga mkono mia kwa mia!! lugha ni vyema kujifunza lakin sio tuseme eti ni chanzo cha umasikini wa tz! nadhan hayo ni mwazo hafifu na ukoloni mambo leo!
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,781
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwanza hongera kwa bahati (au jitihada) ya kipekee kuishi nje ya Tanzania. Pili, sidhani kama kiingereza kinapuuzwa hapa Tanzania na ndio maana kwanza kinafundishwa kama somo ngazi za awali na ndio lugha rasmi ya kufundishia ngazi ya sekondari na kuendelea.

  Pili kulegalega kwa kiingereza isichukuliwe ni kutokana na kupuuzwa kwake kwani hata hicho kiswahili chenyewe wala hakina au hakifundishwi kwa ubora unaotakiwa.

  So, generally, tatizo halipo kwenye kiingereza bali tuna tatizo zaidi ya lugha. Ni almost kila kitu hatukiwezi karibu kila nyanja ya maisha. Kwa mfano, hivi hata kuweka mazingira yetu safi ili tusisumbuliwe na kipindupindu kila wakati tunahitaji kiingereza? Hivi kondakta wa daladala anahitaji kujua kiingereza ili asimnyanyase mwanafunzi? Hivi tunahitaji kujua kiingereza ili tusijisaidie ovyo mitaani? Hivi tunahitaji kujua kiingereza ili tusikwepe kodi au kuiba mali ya umma, ufisadi, n.k?

  Tatizo sio lugha bali mfumo. Na mfumo, nionavyo mimi, unahusisha tabia zetu, desturi zetu, siasa zetu, mila zetu (imani za kishirikina, n.k.), mahusiano yetu, na hata dini zetu. Kama wachina waliweza kwa lugha yao na "sasa hivi" ndio wanajifunza lugha za kigeni kwa nini sisi tushindwe? Ni maoni yangu.
   
 14. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,584
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Naposema mtu ajifunze kwa ridhaa yake namaanisha nje ya tanzania hii maana kwa tz hata usijifunze utajua tu kana watu wanavyojua makabila yao lkn mfumo wa masomo ukianzia awali kwa kingereza utasaidia sana
   
 15. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  We wacha kudanganya watu we!!, English haina mana kama huna maarifa. Tanzania inaheshimika kote kwa kuongea kiswahili fasaha, Kiswahili ndio lugha pekee ya africa inayofundishwa hata ughaibuni. Nyie ndio mnaowapeleka watoto shule ili kujua kiingereza tu halafu mtoto anafeli darasani masomo mengine anabaki kupayukapayuka na kuuza sura. Usiwe mtumwa namna hiyo, boresha chako.
   
 16. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Kiswahili ni lugha pana na yenye kuathiriwa na mazingira ya watu na tamaduni zao...kutokana na hayo kumetokea kitu kinaitwa lahaja.

  Kifupi, lahaja ni lugha kama inavyozungumzwa pahala fulani mathalani, kiswahili cha tanga, ni tofauti na cha mombasa, dar es salaam, mwanza, mbeya, tabora, songea n.k.

  Kwa ufahamu wangu...uongo(uwongo???) na urongo ni maneno mawili yenye kumaanisha kitu kimoja, tofauti ni lahaja.

  Urongo ni neno lenye kutumika katika lahaja za pwani hasa tanga, mombasa na lamu.
   
 17. J

  JeanPrierre Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa, naomba uelewe kuwa Kiswahili ndo utambulisho wa utaifa wako , so u hv to be proud of that. Lugha katika dunia hii ni nyingi sana na huwezi kuzielewa zote. Lakini Kiingereza, ndo kama tunavyofahamu , ni lugha ya kwanza ya kimataifa. Lakini haina maana kuwa bila kuifahamu mambo yako hayataenda vizuri.
  Kiswahili kama lugha siyo kikwazo, hata kidogo. Mifano mingi tu nafikiri ishatolewa. Mie mwenyewe, pamoja na kiswahili changu vilevile naongea Kifaransa na kijerumani. Ulaya kma tunavyofahamu, almost kila nchi ina lugha yake na shughuli zote esp Elimu wanadeliver kwa lugha zao japo unaweza kukuta kuna baadhi ya matangazo yako kwa Kiingereza........, hii ni kutokana na miji mingi kuwa "touristic cities". Ndugu yangu tembelea Ufaransa tu na kiingereza chako, unaweza kutafuta mtu anaeongea kiingereza wiki nzima nausimpate!!!!!!!!!!!.
  Pamoja na kujua lugha nyingine kama Kiingereza, ss ndo wa kukiendeleza au kukiua kiswahili chetu
   
 18. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huwa nachukia sana wanaodharau lugha yao na kutukuza za wengine, huo mimi nauita utumwa.Mleta mada ni mtumwa
   
 19. M

  Mundu JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Enzi za mwalimu katika utumishi wake uliotukuka alisema hivi:

  Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne 1) Watu 2) Ardhi 3) Siasa safi 4) Uongozi bora

  Mimi nadhani kutokuendelea kwetu kunasababishwa na upungufu wa moja wapo ya mambo hayo.

  Sasa ukija na Remix, ukaongeza na lugha, tena ya Kiingereza...hapo inakuwa utata mtupu.
   
 20. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Countries where English is a dejure /official language (List of countries where English is an official language - Wikipedia, the free encyclopedia)
  [TABLE="width: 245"]
  [TR]
  [TD]Country[/TD]
  [TD]Region[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Botswana[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Cameroon[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Eritrea[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ethiopia[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ghana[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Jamaica[/TD]
  [TD]Caribbean[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Kenya[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Lesotho[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Liberia[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Malawi[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Namibia[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Nigeria[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]SierraLeone[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]SolomonIslands[/TD]
  [TD]Oceania[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]SouthAfrica[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]SouthSudan[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Sudan[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Swaziland[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Tanzania[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]TheGambia[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Uganda[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Zambia[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Zimbabwe[/TD]
  [TD]Africa[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Hebu angalieni hizo nchi zinazoongea kiingereza. Wametuzidi nini?
  Kiingereza sio muhimu kiviiile kwa maendeleo yetu. Ili tuendelee tunahitaji Watu, ardhi, sera nzuri (siasa safi), na uongozi makini. Kiingereza is not one of the requirements. In fact, kama (kwa muujiza) Tanzania ingekuwa economically superpower, majirani wote wangekuja tu kutafatua kazi na lazima wangejifunza kiswahili.
  Hebu fikiria, kwa hapa nchini, inasemekana, kilimanjaro wameendelea zaidi kuliko sehemu nyingine. Je wanaongea kiingereza? si wanaongea kichaga na kipare tu?
   
Loading...