Ni lini lugha za kikabila zitakuwa somo kama ilivyo kwa Kiarabu, Kiswahili, Kingereza na Kichina?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema Wakuu!

Ni lini lugha mama zetu, nazungumzia lugha zetu za kikabila zitaingizwa kwenye mitaala kama moja ya masomo ya lugha kama ilivyo kichina, kingereza, kiswahili, kiarabu.

Tunampango gani wa kuhifadhi lugha zetu za asili au elimu ya kigeni itafanikiwa kuzifuta Lugha zetu za asili kisha tubakiwe na kiswahili?

Au ndio tunasema lugha za kikabila zitahamasisha ukabila?

Wataalamu wa mambo mje hapa,
Maana naona tumegangamala mara sijui kiarabu, sijui kiingereza, sijui kichina sijui kifaransa lakini tunasahau vilivyovyetu.

Kama lugha zetu za kikabila zitaondoka na kufutika hii inamaanisha hata kiswahili chenyewe karne kadhaa zijazo hakitakuwepo. Kwa sababu kiswahili ni kibantu kwa 64% lakini kadiri siku ziendavyo ninauhakika hakitakuwa kibantu tena. Kwani kama kibantu kitakufa automatically kiswahili tulichonacho nacho kitakufa.

Itabaki kwenye Historia tuu.

Karibuni kwa mjadala
 
Kiswahili kinatosha
Ujifunze kikabila kwa ajili ya nini
 
Tanzania ina makabila 120+.

Mathalani, kila kabila ina lugha yake. Maana yake kutakuwa na lugha zaidi ya 120 za kikabila.

Sasa serikali itawezaje kuzitunza lugha hizo zote? Serikali iamue lugha za makabila makubwa na mahiri kama Kichagga, Kisukuma, Kimasai, Kihaya na Kinyakyusa ziwe masomo mashuleni, unafikiri makabila mengine yataupokeaje?

Kiswahili chetu tu kinatushinda katika kuitunza na kuiendeleza, ije iwe lugha za kikabila? Abadani, haiwezekani.

Lakini pia, lugha ulizotaja wala si lugha za kikabila. Kiarabu si lugha ya kikabila. Ukienda Saudia, kuna lugha zingine kama Mehri, Tagalog na Urdu wanayozungumza sana Wapakistan.

China ndiyo lugha nyingi sana za kikabila. Ila Chinese imetawala.
 
Lugha za kikabila ni za kurithi na kuishi mazingira uliyopo kwa wakati uliopo, huwezi fundishwa hilo.
 
Kwa uelewa wako unadhani hizo kichina sijui kiarabu ni lugha za 'makabila' ya huko?
 
Issue ya makabila nayo kwa TZ imeanza kujichakachua. Na lugha inafuata. Kwa mfano halisi, mimi ni Muhehe, nimekulia kijijini so kihehe nakiongea vyema tu. Nimemuoa Mnyakyusa, ambaye hajakulia Mbeya, so kinyakyusa chake ni cha ena, ndaga fijo na tonunu basi, yaani cha kuungaunga. Watoto wangu basically ni wahehe, japo hawatokifahamu hata kidogo. Nikicheki fasta, classmates wangu roughly wote wa chuo wameoana makabila tofauti. Je huko mbele hicho kizazi kitakuwa na lugha zipi za asili?
 
Kwema Wakuu!

Ni lini lugha mama zetu, nazungumzia lugha zetu za kikabila zitaingizwa kwenye mitaala kama moja ya masomo ya lugha kama ilivyo kichina, kingereza, kiswahili, kiarabu.

Tunampango gani wa kuhifadhi lugha zetu za asili au elimu ya kigeni itafanikiwa kuzifuta Lugha zetu za asili kisha tubakiwe na kiswahili?

Au ndio tunasema lugha za kikabila zitahamasisha ukabila?

Wataalamu wa mambo mje hapa,
Maana naona tumegangamala mara sijui kiarabu, sijui kiingereza, sijui kichina sijui kifaransa lakini tunasahau vilivyovyetu.

Kama lugha zetu za kikabila zitaondoka na kufutika hii inamaanisha hata kiswahili chenyewe karne kadhaa zijazo hakitakuwepo. Kwa sababu kiswahili ni kibantu kwa 64% lakini kadiri siku ziendavyo ninauhakika hakitakuwa kibantu tena. Kwani kama kibantu kitakufa automatically kiswahili tulichonacho nacho kitakufa.

Itabaki kwenye Historia tuu.

Karibuni kwa mjadala
Unataka kwenda China kuongea kimang'ati?
 
Back
Top Bottom