Ninaomba kuanzisha hii mada baada ya kusikia kwamba kuna mahali walimu wamefukuzwa kwa sababu ya kuongea kiswahili katika mazingira ya shule.
Niseme tu kwamba naunga mkono jambo hilo kwa asilimia mia. Sababu ni hizi hapa.
1. Tutambue kuwa kiswahili ni lugha inayozungumzwa sana Tanzania na ukitoka nje ya mipaka ya Tanzania kiswahili chako unaweka mfukoni! Lazima tujufunze lugha za kimataifa(English) ili tulahisishe mawasiliano na mataifa mengine.
Hoja hii umeitoka kwa kukurupuka,hujatuonesha madhara yake. Kwahiyo ina matatizo gani sasa!!! Au ulitaka kumaanisha kuwa ukifika China na hela yako huwezi kununua bidhaa? kwahiyo watanzania wajifunze Lugha zot e za dunia hii kwamba ukitaka kwenda Rwanda, Angola, SA, Brazil, Korea, China.... ujifunze lugha zao kwanza. Au unamaanisha hakuna wakarimani? Ukienda kuomba omba at?
2. Wageni wakija Tanzania wanapata taabu kweli, matangazo ya biashara yameandikwa kwa kiswahili, barabara nazo unakuta vibao vimeandikwa kwa kiswahil mfano PITA KUSHOTO. Sasa jamani wageni wetu ambao wengi wanakuja kwa maswala ya biashara inakuwa ngumu sana.Mgeni kuendesha gari tanzania ni ngumu sana. Mgeni kufanya biashara Tanzania ni ngumu sana!! Kuna jamaa wafanyabiashara wengi sana nawafahamu wanaprefer kwenda Kenya na Uganda kuchukua bidhaa kuliko Tanzania na sababu wanazozitoa ni ugumu wa Lugha.wanasema kwenda Tanzania ni gharama zaidi maana inabidi umtafute mkalimani ambaye utamlipa.
Hoja hii ni kichekesho, kwakifupi hiyo ndo ajira ya watu wetu kufanya kazi ya ukarimani. Nadhani hujui kuwa pengine hawana wakitakacho na kama kingekuwepo basi wataitumia lugha yetu mara moja. Alafu Sasa tukitoka hapo tutakuomba upendekeze tutafsiri ata majina yetu, mitaa yetu..... hii ni hatari, kisa tuwapendezeshe wageni. Wanaenda kenya si kwakuwa kunatumika Kiingereza bali ni sera na taratibu nzuri za uongozi wa Kenya. Huku serikali imelala. Ni ufisai kwenda mbele. na kwa taarifa yako wakija huku wanaenda kwa wamasai na si UDSM mf!
3. Kenya inatangaza mlima kilimanjaro kwa sababu ya Lugha wanayotumia inaeleweka duniani kote. Sisi tunatangaza mlima kilimanjaro kwa kiswahili wataelewa nini wageni?
Hoja hii si ya kweli. Nadhani hujafanya itafiti au umetumwa kuinusuru CCM na ulalaji usingizi na kukosa ubunifu. Hapa bila kuuma uma maneno ni uzembe wa Serikali na idara ya utalii hasa wizara nzima. Hakuna anayewazuia kutangaza kwa lugha zote za dunia hii. Wamelala.
4.Tunawasanii wazuri sana wa muziki, tamthiliya, vichekesho, ambao wangesaidia sana kuitangaza nchi yetu kimataifa na wao pia kufaidika, lakini wamebaki eti wasanii wa BONGO. (Kwa wale mliobahatika kuangalia
stand up Zambia kilichorushwa na Africa magic channel mtakubaliana na mimi wale jamaa 3 walioshinda sasa hivi ni comedian wakimataifa wanazunguka nchi mabalimabali sababu ni lugha tu, maana kwa ukweli hawawezi kumfikia Joti, Masanja.
Ndugu yangu, tatizo hujanijibu maswali yangu ya awali, una mambo mengi huyajui, nakusaidia, Kazi yoyote ni lazima uisomee. kama hujaisomea uifanye kwa kiwango cha kimataifa. Kina masanja wanaifanya kwa kiwango cha Bongo hasa Dar na Uswazi tu. hawa jamaa wamekuja tu toka mtaani na wasanii wetu wengi hawajaona ata ubao! Sasa unataka wafanye maajab gani hapo. Unawajua waswana na mziki wao ambao unapendwa dunia nzima? Wanatumia lugha gani? Wanakijua Kiingereza? Unakumbuka wale Makirikiri walitinga hadi ufunguzi wa kombe la dunia. Unamjua msomi Mr. Bean? Anasaidiwa na Lugha?
5.Tuna wachungaji wazuri sana(Pastors) lakini mahubiri yao ni kwa kiswahili. T.B Joshua anajulikana kila mahali kwa sababu mahubiri yake ni ya kiingeraza. Si kwamba Joshua unaupako kuliko wengine.
Hihi nayo kaili. Sasa Unailinganisha Nigeria na TZ? hawa jamaa wameanza usanii muda mrefu sana. TB Joshua ni msanii alafu promo tu! Ila ni bora ukumbuke Kuwa babu wa loliondo alivuta watu wengi kwa usanii wake bila shaka na si kwa kiingereza. pia mambo ya imani uendana na inani ya watu. Watu wanaenda yesu alipozaliwa na kumalizia maisha yake si kwakiingereza. Au waislam hawaendi Saudia kwakujua lugha. Hoja yako ni dhaifu na niya kitoto.
6. Mikataba mibovu tunayoingia na wawekezaji ni kwa sababu ya lugha tunashindwa kuilewa vizuri Wawekezaji wanapokuja ilitusionekane ni mbumbumbu wa kiingereza tunabaki kusema YES, YES YES.
Si bure wewe umetumwa na magamba, hivi mkuu unasema kweli hapo! Acha hoja za kipuuzi wewe, hapo ni ufisadi tu. Nakuomba uwatake radhi kina Prof. Shivj, Dr. Nshala, Prof. Majamba, kuwa hawajui kusoma mikataba. Tumia kichwa vizuri unapotaka kudanganya au kuwazuga watu. Ebu angalia Ndg. yangu, Karamagi hajui kiingereza? Kwahiyo ukijua kiingereza unaijua sheria tayari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Unachanganya lugha na utaalamu au??????
7. Kwa watazamaji wenzangu wa aljazeera kuna kipindi kinaitwa 'Tea cafe (kama sijakosea)kinaongelea maswala mbalimbali yanayohusu nchi husika kipindi hicho kinapofanyika. Kipindi hicho kimefanyika,Kenya, Uganda zambia lakini Tanzania hakuna na hata katika ratiba yao Tanzania haimo simply because hakuna watu kama wanasiasa na baadhi ya watu mahalufu ambao wako tayari kujadili kwa kimombo! Sasa dunia itatuelewa vipi matatizo na mipango yetu ?