Kishindo cha DP WORLD: Tozo na Kodi mbalimbali kufutwa au kupunguzwa mwaka wa fedha 2023/2024. Tutarajie mazuri zaidi miaka ijayo ya fedha

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Kwenye mapendekezo ya bajeti Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 baadhi ya tozo kama ile tozo ya kwenye miamala ambayo ni kilio Cha wanyonge wengi na Ile Kodi ya 'store' iliyopelekea mgomo Kariakoo zitaondolewa kabisa. Ukiachana na hizo Kodi, tozo na ushuru mbalimbali wa bidhaa zitapungua kabisa.

Kodi ni muhimu sana na Kwa vyovyote zisingeweza kuondolewa ikiwa mbadala wake haujajulikana ila Kwa kuwa mbadala umepatikana basi Serikali sikivu ya mama Samia imetupatia unafuu.

Tusipepese macho, mbadala wa tozo hizo ni matokeo na faida za uwekezaji zitakazopatikan katika bandari Kwa ushirikiano na DP WORLD. Makubaliano na DP WORLD yatakuja na fursa lukuki ikiwepo kuongezeka Kwa mchango wa mapato yanayochangiwa na bandari mpaka 67% kutoka 37% ya Sasa.

Hizi ni faida za mwaka wa kwanza tu, Sasa tufikirie mbali Zaidi faida zitakazokuwepo mwaka wa fedha 2024/2025-2025/2050. Naamini zitakuwa za kufurahisha.

Wanaopinga makubaliano haya watuambie kama hili sio jambo jema Kwa wananchi?

Je, Kuna mwananchi wa kawaida anayepinga makubaliano ikiwa yanampa faida za Moja Kwa Moja kama hizi?

Rai yangu, tumwache mama afanye kazi ,mipango na mikakati yake Kwa Taifa ni mikubwa Zaidi ya tunavyowaza au kufikiria.
 
Ogopa matapeli, bandari yetu haiuzwi.
 
Kodi ni muhimu na zinawekwa Kwa mujibu wa Sheria na hata kuondolewa kwake haziondolewi kienyeji tu
Kodi za wizi kwa wananchi. Unaende kununua v8 matumizi ya hovyo honyo ,mwisho wa siku wanauza bandari zetu mpaka bandari ya mto ruvu
 
Hoja ya kijinga kabisa. Kabla ya Serikali hji kulikuwa na tozo kwenye miala?

Kabla ya serikali hii kulikuwa na tozo kwenye mafuta?

Wakati ambao tozo hizo hazikuwepo, DP ndiye aliyefanya zisiwepo?

Watetezi wa mkataba wa hovyo wa bandari, wote ni wajinga wasio hata na kumbukumbu.
 
  • Usijiondoe ufahanu kuwa wameongeza gharama kwenye mafuta na cement! Wajinga ni wengi!
  • Bandari mpaka za kwenye viziwa zimetekwa hivyo, ni marufuku kukuta mtu hata anaota jua bila idhini ya DP.
  • Akina Mkwawa wangefufuka leo wangeanzisha farangati za kufa mtu kuliko hata walivyofanya kwa Wajerumani
 
Hoja ya kijinga kabisa. Kabla ya Serikali hji kulikuwa na tozo kwenye miala?

Kabla ya serikali hii kulikuwa na tozo kwenye mafuta?

Wakati ambao tozo hizo hazikuwepo, DP ndiye aliyefanya zisiwepo?

Watetezi wa mkataba wa hovyo wa bandari, wote ni wajinga wasio hata na kumbukumbu.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Rais kawapungunzia mzigo wanyonge kwenye tozo mbalimbali.

Hizo tozo kwenye petrol ni tozo kwenye luxury ,kadri unavyotaka luxury ndio utalipa Zaidi. Tuseme inakuwa ni tozo katika kulinda na kuhifadhi barabara na hapo watumiaji wa barabara ndio wanalipa.
 
Back
Top Bottom