Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Mkuu nna kiswali kingine kidogo..
Unaamini kuna kitu kinaitwa dark energy?
Darker enegry...

Darker matter.....



namsubiri vizuri ssna hapa make quantum physics katika kuulezea how nature is imebase kwenye vitu hivi,,na ukiangalia logo yake [profile picture] kaweka fibonacci golden ratio signs ambayo inaonesha original of life under fibonancci sequence,,,,,manake anabelive kwenye quantum physics from explaining reality of the universe,,
 
namini namsubiri hapa hapa ajichanganye aseme anaijua vizuri ndo nimkaange vizuri na quantum physics yak,,,,anadhani wengine watujui kuhusu quantum tecnlogy that tries to explani about the core of everything....nimemsubiri ajibu hiyo artice watu wafunguke vuzuri kama hatajikana leo sijui
Nasubiri jibu pia
Cc kiranga
 
Wapi nimesema nadhani ana majibu zaidi ya hayo?

Unanisoma? Sijaandika hapa kwamba hawezi kujibu kwa sababu hata yeye hajui anachotaka kuuliza ni nini?

Hujaona nilipoandika hilo?
Si kila kitu ukiseme moja kwa moja ndipo umanishe unataka nini!!
Kitendo cha kukataa jibu lake na kutaka jibu jingine au kutokuridhika na jibu lake ni wazi kwamba unataka jibu jingine.

Kutaka jibu jingine ni kudhani ana majibu zaidi ya la mwanzo.

Wewe umekataa hilo jibu, unasisitiza kupewa jibu jingine, unataka ujibiwe vp?
 
Nikikuonesha unaniruhusu nikuite jina gani?
Bado nasubiri uniite jina ulilochagua kuniita na nikakuruhusu,endapo tu utaonesha post ambayo mtu kasema akili ni uwezo wa kutambua uwepo wa mungu.

Nasubiri.
 
Sieleweki wapi?

Kujua aina za akili kivipi wakati nataka kujua akili ni nini...

Nataka maelezo ktk kujua anachouliza ili nimjibu kuwa akili hapo kwa maelezo ninazo au sina.
Unataka maelezo ya nini wakati ameuliza una akili?

Eleza hasa ambacho kinachanganya hapo hadi kihitaji maelezo,ukishindwa kueleza naye hatoweza kuelezea ikiwa kweli kuna ulazima huo.

Neno akili linajitaji maelezo gani?
 
Iko hivi
Kwanza wale wasio waamini katika Mungu mmoja wamekwepa sana sana kujibu hili swali kwakuwa wanajitambua wazi kuwa wanazo akili lakini kimbembe ni kuthibitisha! Na kamwe hawawezi kukwambia hawana akili... Hivyo hivyo ni sawa na uwepo wa Mungu! Yupo lakini huwezi kumthibitisha kimwili kama usivyoweza kuthibitisha akili ulizonazo japo zipo
Dunia ina pande mbili giza na nuru, juu na chini, kushoto na kulia
VINAVYOONEKANA na VISIVYOONEKA...

Tunahisi, njaa kiu ama hamu ya kitu lakini hatuwezi kuvionyesha vikaonekana... Ila vinatulizwa na vitu VINAVYOONEKANA yaani chakula, maji nk
Kama tunakubali kuwa kila kitu duniani kina pande mbili basi tutakuwa wajinga tukibisha kama kuna upande wa pili wa dunia usioonekana na huu ndio

ulimwengu wa roho, ulimwengu wa Kimungu usio na ithibati za kisayansi lakini upo
Wewe utakuwa na matatizo makubwa sana.Na hii ni kwa sababu Mungu mwenye uwezo wote,upendo wote naujuzi wote unayesema kakuumba,hayupo.

Kiranga ktk maelezo yake yote hakuna aliposema haamini uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani.Anasema haamini kwa sababu dhana ya uwepo wake inajipinga yenyewe.Ni sawa na wewe uzaliwe bila kumjua baba yako.Na baada ya kufikisha umri wa miaka let say arobaini anatokea jamaa mwenye umri wa miaka 39 anadai yeye ndiye baba mzazi wako.Hivi kwa mazingira haya unahitaji mpaka mama mzazi wako(aliyefanya tendo na baba yako ukapatikana) awepo ili kujua kwamba kwa umri wako wa miaka 40 haiwezekani baba mzazi wako awe huyu wa miaka 39?

Hatuamini uwepo wa Mungu mjuzi wa yote,upendo wote na uwezo wote si kwa sababu haonekani bali hatuamini kupitia dhana ya uwepo wake ambayo imejipinga yenyewe hata kabla ya kupingwa na Kiranga.

Vipo vitu vingi tu visivyoonekana ila nakiri vipo.Na ni kwa sababu uwepo wake hauna contradictions.Mfano mtu kusema neno "kesho".
 
Acha niende moja kwa moja. Mtu akikuuliza una akili au hauna unamjibu nini? Au utasema Mshana Jr hajajibu?
Ni simple tu namuuliza kwanza akili ni nini!!

Maana wengine wanasema akili ni nywele,sasa Mimi mwenye kipara itakuwaje!?
Si itabidi niseme sina akili!.

Wengine wanasema akili ni uwezo wa kuchakata taarifa na mambo mengine kichwani.Hapa itabidi niseme ninazo.

Sasa ya nini kujitabisha kote huku wakati mtoa hoja angesema tu maana anayoikusudia ili nimjibu kama nina akili ama sina!?
 
Msaidie kujibu kwanza swali kongwe! Hivi na maarifa yenu yote mnayojivunia kuwa nayo (kama ni kweli) mpaka leo hii mmeshindwa kabisa kujibu kama mna akili ama hamna? HILI LAWEZA KUWA AJABU KUU NANE LA DUNIA....
Nijibu wewe kama una AKILI ama huna nitakupa ushahidi Adam kuwa binadamu wa kwanza!
Nimeulizwa AKILI ninini nimejibu ni AKILI.. Kama hili sio jibu sahihi naomba nipewe jibu sahihi... Hapa pia hakuna kitu!
Akili ina tafsiri tofauti tofauti mkuu. Ndo maana anataka kujuwa unamaanisha nini. Hivi mtu asiye na akili unamtafsiri vipi?
 
Wewe utakuwa na matatizo makubwa sana.Na hii ni kwa sababu Mungu mwenye uwezo wote,upendo wote naujuzi wote unayesema kakuumba,hayupo.

Kiranga ktk maelezo yake yote hakuna aliposema haamini uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani.Anasema haamini kwa sababu dhana ya uwepo wake inajipinga yenyewe.Ni sawa na wewe uzaliwe bila kumjua baba yako.Na baada ya kufikisha umri wa miaka let say arobaini anatokea jamaa mwenye umri wa miaka 39 anadai yeye ndiye baba mzazi wako.Hivi kwa mazingira haya unahitaji mpaka mama mzazi wako(aliyefanya tendo na baba yako ukapatikana) awepo ili kujua kwamba kwa umri wako wa miaka 40 haiwezekani baba mzazi wako awe huyu wa miaka 39?

Hatuamini uwepo wa Mungu mjuzi wa yote,upendo wote na uwezo wote kwa sababu haonekani bali tunapinga kupitia dhana ya uwepo wake ambayo imejipinga yenyewe hata kabla ya kupingwa na Kiranga.

Vipo vitu vingi tu visivyoonekana ila nakiri vipo.Na ni kwa sababu uwepo wake hauna contradictions.Mfano mtu kusema neno "kesho".
..'Emmanuel'..
Maana yake ni Mungu pamoja nasi..
Hahahahhahh...

Walikosea sana kukuita hivyo mkuu
 
Akili ni uwezo wa kuelewa, kujifunza na kuchambua mambo mbalimbali katika mazingira yetu na kuweza kupata ujuzi na maarifa ya kutuwezesha kuishi kwa ufanisi.

Ikumbukwe ni dhana pana, hiyo ni mojawapo.
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri.

Sasa toka uanze kuzisoma post/comments za Kiranga wewe unamuweka wapi kwenye hilo!?

Je,ana huo uwezo wa kuchakata mambo ama hana!?

Kama jibu lako ni ndiyo maana yake ana akili.Na kama huo uwezo hana maana yake si hana akili!!.

Mjadala unakuwa umeishia hapo na tuendelee na hoja zingine.

Ila siku nyingine nyinyi wafuasi wa Mshana Jr muache kuwa mnauliza maswali ambayo majibu yake yapo clear.Kama ni kuendelea kumtolea sadaka jamaa yenu ili afaidishe familia yake huku nyinyi waumini wake mkishindia mlo mmoja endeleeni.Na maandiko yenu yamewaambiwa kabisa kuwa mnaangamia kwa kukosa maarifa!!
 
Akili ina tafsiri tofauti tofauti mkuu. Ndo maana anataka kujuwa unamaanisha nini. Hivi mtu asiye na akili unamtafsiri vipi?
Mushi angejibu kwa tafsiri yake. Mbona sijamuwekea... Limitations? Mbona mimi sikuwa na masharti? Nimeulizwa AKILI ninini nikajibu kuwa ni AKILI! Bila kujali jibu langu ni sahihi ama la lakini nilijibu
Sasa hebu nisaidie wewe msaidie kujibu! Utakuwa umefanya jambo moja kubwa sana... Swali lilikuwa linasema una AKILI ama huna AKILI?
 
..'Emmanuel'..
Maana yake ni Mungu pamoja nasi..
Hahahahhahh...

Walikosea sana kukuita hivyo mkuu
Hawakukosea maana inategemea na Mungu yupi anazungumziwa.

Mwanamziki Beyonce Knowles amenunua kanisa kule Marekani na amejitambulisha kuwa yeye ndiye Mungu wa kanisa/dini/dhehebu hilo.
Na sifa za Mungu huyu (Beyonce) ni kuwa yeye ni mwanamziki na ameolewa na Jay-zee.

Na kwa kuwa hizi sifa za Mungu Beyonce hazina contradictions za uwepo wake(Kweli ni mwanamziki na mumewe ni Jay-zee),ni rahisi zaidi kuamini umungu wake kuliko huyu wa kwenye vitabu anayesemwa ana uwezo wote,upendo wote na ujuzi wote halafu akamuumba eti shetani ili kuwaharibu wanae.

Mungu wa namna hiyo hayupo,ni stori tu za vijiweni za kujipatia fedha kwa mgongo wa sadaka na zaka huku waumini wakizidi kuwa mafukara.
 
Back
Top Bottom