Hadi sasa hivi hujatoa tafsiri ya maneno ambayo umeyaandika na tayari nimeshakwambia lakini umekimbia kutoa tafsiri
Umeandika unavyojua wewe maneno ulikoyatoa.
Umesema niwe specific nime quote tena na tena comment yako lakin umekaa kimya kuhusu hilo
Kiranga hajawahi kukimbia changamoto wala swali.
Kama hajui jibu atakwambia tu hajui.
Sio kamaMshana, unamwambia ajibu akili ni nini, anajibu akili ni akili, bwahahaha.
Nakujibu hivi.
Naweka maneno nilivyoyaandika Kiingereza, halafu natafsiri Kiswahili chini.
Usije kuomba tafsiri ya lugha ya kabila yenu tu hapa.
Kiingereza
By convergence, the mathematics needed to resolve the nature and beginning of the universe in the singularity at the big bang, according to the best known current theories, can be narrowed down to reconciling Einstein's Relativity, which deals with the science of the very big/heavy and quantum theory, which deals with the very small.
This is because, at the singularity, all the matter of the universe is condensed into an infinitesimally small space -the primordial beginning of our spacetime, necessitating a conundrum of the very dense/ large mass (Einstein's Relativity)in an infinitesimally small space (Quantum Physics).
Without coming up with the mathematics of reconciling Relativity and Quantum Physics, which has not been done todate, the beginning of the universe will remain unknown.
Tafsiri ya Kiswahili
Kwa kujongea kwenye kukutana, hisabati zinazohitajika kutatua asili na mwanzo wa ulimwengu katika ajabu la mwanzo wa ulimwengu lililotokea kwenye Mshindo Mkubwa, kwa mujibu wa nadharia nzuri kabisa zinazojulikana sasa, zinaweza kubanwa zaidi ndani ya maafikiano kati ya nadharia ya Einstein ya Uwiano, ambayo inafanya kazi na sayansi ya vitu vikubwa sana/ vizito sana, na Nadharia ya Kwanta, ambayo inahusika na vitu vidogo sana.
Hii ni kwa sababu, kwenye maajabu ya mwanzo wa ulimwengu, mada yote ya ulimwengu ilibanwa katika eneo dogo isivyomithilika - mwanzo wa sili wa eneomuda wetu, kusababisha kizungumkuti cha mada iliyo ngumu/ kubwa (Uwiano wa Einstein unahusika hapo) iwe kwenye eneo dogo sana (Fizikia ya Kwanta inahusika)
Bila ya kupata hisabati zitakazotatua kitendawaili cha kuunganisha Uwiano wa Einstein na Fizikia ya Kwanta, kitu ambacho bado hakijawezekana kufanyika mpaka leo, mwanzo wa ulimwengu utabaki haujulikani