Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 19,675
- 59,775
MIAKA mitatu tangu Rais Samia Suluhu Hassan akabidhiwe kijiti cha kuiongoza Tanzania wadau wa demokrasia wanaielewa falsafa yake ya 4R yaani maridhiano, ustahamilivu, mageuzi na kujenga upya.
Wakati akikabidhiwa kijiti Machi 2021, Rais Samia alisitiza dhamira yake ya kuijenga Tanzania moja yenye ustawi kwa wananchi wote na mara zote wito wake umekuwa kutaka kujenga jamii yenye maelewano, umoja na mshikamano, uzalendo, maridhiano, ustahamilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote.
Rais Samia anasema ataj i tahidi kuf anya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria za uchaguzi ili Tanzania iende na wakati na kutoa fursa zaidi kwa watu wengi kunufaika kiuchumi.
“Tutajitahidi kuijenga Tanzania yenye haki, demokrasia na usawa na mafanikio na ndiyo maana katika kipindi hiki tulikuja na ‘idea’ nne (akimaanisha maridhiano, ustahamilivu, mabadiliko na kujenga upya)…vyama vya siasa tunazungumza, tunaelewana,” anasema Rais Samia.
Katika mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam 4R ilikuwa moja moja ya mada iliyojadiliwa ambapo wadau mbalimbali wa demokrasia wameeleza namna walivyozielewa.