Kinachokwenda kufanyika kwenye miamala ya simu, ni Serikali kuuchukua tena uchumi sadifu wa kati kwa walala hoi kwamba hawastahili kuwa nao

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,622
2,459
Sijui ni kivipi mtu anapofika kwenye level fulani ya maisha hutaka kuilazimisha akili yake kuwa na wengine wote wako kama yeye

Badala ya kurudisha akili zake kule alikotoka ili ayapime maisha aliyopitia na hatimaye aone pia wale ambao bado wako huko wanapitia ugumu uleule aliowahi kuupitia yeye kabla hajafika hapo alipo, hata akichaguliwa/bahatika kuwa katika nafasi Fulani ya uongozi, Aumize kichwa chake jinsi ya kuisaidia jamii masikini,

Kusaidia Jamii kama kiongozi, hauhitaji utoe pesa mfukoni mwako

Ni kuweka sera wezeshi ambazo zitaifanya jamii hii masikini kufikia uwalau maisha ya kufurahia uwepo wao hapa duniani

Jamii yetu bado masikini sana, bahati mbaya kabisa, tunao baadhi ya viongozi ambao tangu kuzaliwa hawaijui shida, na ndiyo maana imekuwa ni rahisi kwa viongozi kama hao kupiga makofi kwenye mijadara mingine inayoumiza walala hoi, Lakini Kuzaliwa kwetu katika jamii ambayo haikuwahi kuona shida, isitufanye kutotambua kwamba masikini wa masikini wapo, na shida zipo

Kinacho kwenda kufanyika sasa kwenye sera ya makato ya miamala ya simu, ni kwenda kuzidisha ukali wa maisha kwa jamii kubwa ya watu wa maisha ya chini na kuathiri uchumi wao mdogo unaotegemea jasho jingi ili mtu apate mlo wa siku

Naishauri serikali, Kwa sababu tunajamii kubwa ambayo inaishi kwa kutegemea maisha ya kubangaiza, na kwa sababu tozo hiyo ya miamala na laini ya simu ni mpango wa serikari ipate kodi ili kuendeleza miradi na ujenzi wa barabara vijini

Badala ya kodi hiyo kuingizwa kwenye huduma hizi mhimu na kuifanya huduma hii iwe na makato makubwa kiasi cha kufanya wazee wetu kule vijini wakose msaada kutoka kwa vijana wao wanaowatumia vijisenti vya kujipatia mahitaji yao

Kodi hii ihamishiwe upande wa abiria wanaosafiri kwa mabasi kwenda mikoani, usafiri wa Treni, meli, na ndege, na kodi yake iwe ni kila abilia atakatwa kodi ya sh 1,000 tu kwa kila abiria anayetumia usafiri wa basi kwenda mkoani,

Serikali itafute namna ya kulipa hiyo kodi, ni au iunganishwe kwenye tiketi, msafiri badala ya kulipa 10,000 alie 11000,

Itawaokoa wengi ambao hata hawajui ni lini watapanda basi, ndege, meli wala treni kwa maana hawana huo uwezo, lakini wanasimu na hawapigi simu wao, zaidi husubiri wapigiwe tu na kutumiwa pesa kidogo
 
Watalamu waliona pazuri kukamua kwenye simu,wewe umesomea kodi?
 
Watalamu waliona pazuri kukamua kwenye simu,wewe umesomea kodi?
Mkuu haya ndiyo matatizo nilosema kwenye bandiko hili, Ukibahatika kuwa na maisha fulani hivi, usisahau pia kuwa kuna mtu hajafikia hayo maisha, bahati mbaya hii kodi inaenda kukusanywa kwa kiwango kilekile cha mtu wa chiiini zaidi, wa kati na wa juu kwa kiwango kilekile,

Kwa nini kodi hizi zisielekezwe kwa wasafiri wa ndege, meli, mabasi ya mikoa n.k?
 
Mkuu haya ndiyo matatizo nilosema kwenye bandiko hili, Ukibahatika kuwa na maisha fulani hivi, usisahau pia kuwa kuna mtu hajafikia hayo maisha, bahati mbaya hii kodi inaenda kukusanywa kwa kiwango kilekile cha mtu wa chiiini zaidi, wa kati na wa juu kwa kiwango kilekile,

Kwa nini kodi hizi zisielekezwe kwa wasafiri wa ndege, meli, mabasi ya mikoa n.k?
Hao watu wa chini unaowasema ndio chanzo cha Serikali kutowajibika kwa wananchi. Hawa ndiyo wanakuwa watu wa kwanza kuunga mkono Serikali kwa kila kiti, hata inapowaonea watu.

Hili rungu likae hapo hapo, limbonde kila mtu kichwani, ili akili iliyolala iamke. Wasipopata maumivu hao unaowaita watu wa chini, siku zote wataendelea kuwa kikwazo cha mabadiliko yanayohitajika ili kuwa na uongozi unaowajibika kwa umma.

Hata wakati marehemu, kwa udikteta tu, alipoamua kuwaonea wenye pesa, akawa anawabambikia kesi, anawateka, anawapoteza, kundi kubwa la waliokuwa wakifurahia, ni hilo kundi la watu maskini.
 
Mimi kwa mtazamo wangu wale watu ambao wanaona hii issue ni ngumu kwao warudi tu kwenye Yale maisha ya zamani kabla issue ya simu ama miamala kuja. Maana sidhani Kama Kuna ulazima wa kutumia simu kwenye Jambo lolote.

Ambao hawataki wafungie simu zao makabatini na wenye kutaka wakubaliane na hali halisi. Muhimu hapa ni hii Kodi tunayokatwa itumike Kama ilivyokusudiwa. Bunge na mamlaka husika ziifuatilie kwa ukaribu Sana. Sio tukatwe kodi halafu ziishie kufaidisha watu binafsi kwa kuzidokoa.
 
Mimi kwa mtazamo wangu wale watu ambao wanaona hii issue ni ngumu kwao warudi tu kwenye Yale maisha ya zamani kabla issue ya simu ama miamala kuja. Maana sidhani Kama Kuna ulazima wa kutumia simu kwenye Jambo lolote..
Ni taifa la kujitolea kwa kila khali, lakini kwa bahati mbaya kabisa utasikia, Fedha zimepotea, fedha bilioni ngapi zimeibiwa sjui na nani, sijui taasisi fulani inajilipa posho ngapi kwa siku

Hii ndio inayoliza walipa kodi
 
Sijui ni kivipi mtu anapofika kwenye level fulani ya maisha hutaka kuilazimisha akili yake kuwa na wengine wote wako kama yeye

Badala ya kurudisha akili zake kule alikotoka ili ayapime maisha aliyopitia na hatimaye aone pia wale ambao bado wako huko wanapitia ugumu uleule aliowahi kuupitia yeye kabla hajafika hapo alipo, hata akichaguliwa/bahatika kuwa katika nafasi Fulani ya uongozi, Aumize kichwa chake jinsi ya kuisaidia jamii masikin...
Posho za wabunge zitozwe kodi, hii itaonyesha uzalendo wao
 
Sijui ni kivipi mtu anapofika kwenye level fulani ya maisha hutaka kuilazimisha akili yake kuwa na wengine wote wako kama yeye

Badala ya kurudisha akili zake kule alikotoka ili ayapime maisha aliyopitia na hatimaye aone pia wale ambao bado wako huko wanapitia ugumu uleule aliowahi kuupitia yeye kabla hajafika hapo alipo, hata akichaguliwa/bahatika kuwa katika nafasi Fulani ya uongozi, Aumize kichwa chake jinsi ya kuisaidia jamii masikini
Inahitaji akili ndogo tu kutambua kusudio la Serikali ya Awamu ya Sita.

Serikali ya Awamu ya Tano ilianzisha miradi ya kimkakati, yenye lengo ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini, kwa kutumia fedha za ndani. Fedha hii ilipatikana kwa kuziba mianya ya ufisadi, ubadhirifu wa mali ya umma, kulinda utajiri wa nchi hii (ardhi, chini ya ardhi, majini, na angani) na ilikusanya kodi kwa wenye nacho (wafanya biashara wakubwa).

Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mama, inabidi ikamilishe miradi hiyo kuthibitisha kuwa mama naye ana uwezo. Kwa silika ya wanawake, Mama Rais hana ubavu na uthubutu wa kutumia njia ambazo aliyemtangulia (mwanaume jembe) kupata fedha ya kukamilisha hiyo miradi ya kimkakati na kuanzisha mipya.

Kwa kauli zake mwenyewe anatarajia kupata hiyo fedha kutoka kwa wafadhili, wafanya biashara na wawekezaji, hasa hasa wa nje. Kwa sababu hiyo amewalegezea masharti ya kuwekeza na kufanya biashara lakini wakati huo huo akiwaongezea wasio nacho mzigo, kupitia kodi, kwa kigezo cha kila mwananchi kuchangia maendeleo ya nchi.

Ukweli utabaki kuwa kodi mpya, km ya miamala, itabebwa zaidi na wasio nacho kwa njia ya bei za bidhaa ambazo zitaongezwa kufidia ongezeko la gharama za uzalishaji kutokana na kodi mpya.

YAJAYO YANAFURAHISHA lakini YANAFIKIRISHA
 
Mimi kwa mtazamo wangu wale watu ambao wanaona hii issue ni ngumu kwao warudi tu kwenye Yale maisha ya zamani kabla issue ya simu ama miamala kuja. Maana sidhani Kama Kuna ulazima wa kutumia simu kwenye Jambo lolote...
Ungelikuwa karibu na mimi ningekuchapa kibao kimoja matata sana cha uso najua akili zingerudi.

Unamaamisha kweli watu waache kutumia simu kalne hii.

Na hayo matumizi ya serikali ni yepi?
 
Sera za kodi kwa nchi mbalimbali hua ni ama uwatoze zaidi matajiri maskini wawe na nafuu au uwatoze zaidi maskini ili matajiri wawe na nafuu. Sijui kwetu ni ipi inatumika kati ya sera hizo juu.
 
Ungelikuwa karibu na mimi ningekuchapa kibao kimoja matata sana cha uso najua akili zingerudi
Unamaamisha kweli watu waache kutumia simu kalne hii
Na hayo matumizi ya serikali ni yepi?
Na Mimi ningekuchapa bakora ili uache kulalamika hovyo. Mtoto wa kiume unalalamika kuchangia kodi kwa ajili ya maendeleo yako.

Nyie ndio wale huku mtaani tukisema tuchange Ela kwa ajili ya kukarabati barabara iliyoharibika kutokana na mvua mnapinga na kusema wachange wenye magari tu. Ila wake zenu wakiumwa mnakodisha magari na kuyapitisha kwenye barabara hizohizo kwenda hospital.
 
Sera za kodi kwa nchi mbalimbali hua ni ama uwatoze zaidi matajiri maskini wawe na nafuu au uwatoze zaidi maskini ili matajiri wawe na nafuu. Sijui kwetu ni ipi inatumika kati ya sera hizo juu.
Nadhani kwetu inatumika ya kuwatoza zaidi masikini ili matajiri waendelee kuwa nacho zaidi

Na hii ni mbaya zaidi kwa sababu, Serikali inayofanya masikini waishi kwa machozi ya uchungu, huwa ni kama laana fulani, kwa maana serikali inalazimisha kuwanyang'anya hata hicho kidogo walichonacho kwa nia ya kuogopa wawekezaji wasiondoke!!
 
Na Mimi ningekuchapa bakora ili uache kulalamika hovyo. Mtoto wa kiume unalalamika kuchangia kodi kwa ajili ya maendeleo yako.
Nyie ndio wale huku mtaani tukisema tuchange Ela kwa ajili ya kukarabati barabara iliyoharibika kutokana na mvua mnapinga na kusema wachange wenye magari tu. Ila wake zenu wakiumwa mnakodisha magari na kuyapitisha kwenye barabara hizohizo kwenda hospital.
Mkuu, mawazo yako ni mazuri sana, lakini kumbuka kwamba, hii kodi haijazingatia mwenye nacho na asiyenacho

kuna mtu huko kijijini, hajui kuwa na vocha zaidi tu ya yeye kusubiri kupigiwa na kutumiwa vijisenti vya kumsaidia leo ili mkono uingie kinywani naye yumo kwenye kodi hii

Kwa nini hizi kodi zisingelekezwa kwa wasafiri wa ndege, mabasi ya mikoani, treni na meli?

Kwa siku wasafiri wa vyombo hivyo, ni wangapi, na wakati huohuo ikaboreshwa ikawa ni kama mtu analipia bima ya afya, ili kama ikitokea ajali, atibiwe bule kwa kutumia kodi hiyo!
 
Mimi kwa mtazamo wangu wale watu ambao wanaona hii issue ni ngumu kwao warudi tu kwenye Yale maisha ya zamani kabla issue ya simu ama miamala kuja. Maana sidhani Kama Kuna ulazima wa kutumia simu kwenye Jambo lolote...
Ndugu yangu pesa lazima ipigwe kwasababu watekelezaji wa mipango ndio hawa watumishi wa imma ambao hawajapandishwa mishahara kwa miaka 5, na pia mishahara yao midogo
 
Back
Top Bottom