Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau | Page 26 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Safari_ni_Safari, Nov 30, 2010.

 1. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 23,171
  Likes Received: 6,884
  Trophy Points: 280
  KILIMO BORA CHA UFUTA
  Ufuta (sesamum indicum)ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga na ukanda wa chini katika mikoa ya Rukwa na Mbeya. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mbegu za zao hili huwa na wastani wa mafuta kiasi cha asilimia 45.


  MAMBO YA KUZINGATIA WA KATI WA KUZALISHA MBEGU
  - Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na bora, inayovumilia mashambulizi ya magonjwa na wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta mengi.

  - Chagua mbegu inayokomaa kwa pamoja ili kurahisisha uvunaji na pia kuepuka upotevu wa zao shambani.

  - Aina nyeupe ya mbegu ya ufuta hupendelewa zaidi kuliko aina nyeusi.

  MBOLEA
  Ufuta unahitaji rutuba ya kutosha ili kutoa mazao bora. Katika kudumisha rutuba ya udongo, tumia kilimo cha mzunguko wa mazao au weka mbolea za asili pale inapobidi.

  PALIZI
  Dhibiti magugu kwa kupalilia ili kuruhusu ufuta kutumia vizuri unyevu na virutubishi. Magugu mengine huwa ni maficho ya wadudu waharibifu wa zao la ufuta.

  MAGONJWA NA WADUDU
  Ufuta hushambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali ambao huweza kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Hivyo kagua shamba mara kwa mara hasa kwenye maua na mapodo ili kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili zamashambulizi, chukua tahadhari mapema kabla ya uharibifu mkubwa haujatokea.

  MAANDALIZI KABLA YA KUVUNAKAGUA SHAMBA
  - Kagua shamba kuona kama ufuta umekomaa.
  - Ufuta hukomaa, kati ya miezi mitatu na minne tangu kupanda kutegemea aina.
  - Aina ya ufuta usiokuwa na matawi hukomaa mapema kuliko ile yenye matawi.
  - Ni muhimu kuwahi kuvuna ili kuepuka ufuta kupukutikia shambani.

  DALILI ZA KUKOMAA UFUTA SHAMBANI
  - Kwa kawaida majani hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya manjano na hatimaye kudondoka.

  - Mashina hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya kahawia.

  VIFAA VYA KUVUNIA
  - Kamba
  - Siko
  - Panga

  VIFAA VYA KUKAUSHIA
  - Sehemu ya kukaushia yenye Sakafu ya saruji
  - Maturubai
  - Sakafu safi

  USAFIRI

  - Mikokoteni
  - Matela ya matrekta
  - Magari

  KUVUNA
  - Vuna ufuta mapema kabla mapodo kukomaa sana na kuanza kupasuka na kuachia punje.Mapodo ya ufuta yaliyokomaa sana yakiguswa au kutikiswa na upepo hupasuka na kuachia mbegu, hali inayosababisha upotevu mkubwa.

  - Mbegu za ufuta ni ndogo na zikidondoka chini ni vigumu kuziokota. Vilevile mbegu zilizodondoka ni vigumu kuzitenganisha na uchafu.

  - Uvunaji wa ufuta huhusisha ukataji wa mimea yenye mapodo kwa kutumia vyombo vya mkono kama panga kwa kukata mashina.

  - Kwa aina za ufuta zenye mapodo yanayopasuka, uvunaji ufanyike wakati mimea bado ni kijani ili kuepuka upotevu wa mbegu.

  - Aidha uvunaji ufanyike wakati hakuna upepo wala jua kali.

  - Baada ya kukata mashina yafunge katika mizigo midogo na kuweka katika vyombo vya kusafirisha kama vile mikokoteni, matela au magari hadi sehemu ya kukaushia.

  - Panga mizigo midogo kwa kusimamisha katika malundo madogo yasiyozidi mizigo minane kwenye sehemu safi za kukaushia.

  KUKAUSHA
  Mapodo ya ufuta hukaushwa yakiwa yamefungwa katika vitita. Vitita huwekwa kwa kuegeshwa kwenye fremu ya kukaushia kwa muda wa wiki mbili hadi tatu kutegemea hali ya hewa. Fremu hii huwekwa juu ya turubai au sakafu ili kuzuia upotevu wa punje kutokana na kupasuka kwa mapodo.

  KUPURA
  Upuraji hufanyika kwenye turubai, mkeka au kwenye sakafu safi.

  - Vitita hupigwa taratibu kwa kutumia mti au hutikiswa vikiwa vimegeuzwa vichwa chini ili kuruhusu punje za ufuta kudondoka kwenye sakafu safi au turubai.

  KUPEPETA NA KUPEMBUA
  Kupepeta na kupembua hufanywa ili kuondoa takataka kama vile mawe, vipande vya mapodo,vijiti na vumbi.Njia bora ya kupepeta na kupembua ni kwa kutumia mikono.

  - Ufuta huwekwa kwenye vyombo kama vile ungo kwa kiasi cha kilo mbili hadi tatu. Ufuta hurushwa hewani kwa kasi ndogo na takataka nyepesi huchukuliwa na upepo. Zile nzito huondolewa kwa mikono.

  KUFUNGASHA
  Mbegu za ufuta zilizo safi huwekwa kwenye vifungashio kama vile magunia madogo ya aina ya juti ya ujazo wa kilo 50.

  - Fungasha mbegu za ufuta kwenye magunia yenye uzito usiozidi kilo 50. Kabla ya kufungasha hakikisha mbegu zimekauka hadi kufikia unyevu wa asilimia 10.

  KUHIFADHI
  - Panga magunia ya ufuta juu ya chaga.
  - Panga kwa kupishanisha ili kuruhusu mzunguko wa hewa kati ya magunia.

  KUSINDIKA MBEGU ZA UFUTA

  Ufuta husindikwa kupata bidhaa ya mafuta ambayo hutumika katika mapishi mbalimbali. Mafuta hukamuliwa kwa kutumia njia za asili na kwa kutumia mashine.

  Njia za asili zina ufanisi mdogo ukilinganisha na zile za kukamua kwa mashine, hivyo ni vyema kutumia mashine. Kuna mashine za aina mbili zinazotumika kukamua mafuta; mashine za mkono na zile zinazoendeshwa kwa injini au mota ya umeme. Mashine za mikono zinazotumika zaidi hapa nchini ni za aina ya daraja (Bridge press) na Ram.

  KUKAMUA KWA MASHINE YA DARAJA
  Mashine ya daraja ni moja ya mashine za kisasa zinazoweza kukamua mafuta ya ufuta. Mashine hizi huendeshwa kwa mikono na zina uwezo wa kukamua mafuta kwa asilimia 68 hadi 72.

  Inaweza kukamua kilo 25 za ufuta kwa saa moja. Ili kupata ufanisi mzuri wa mashine hii, ni muhimu ufuta uwe na unyevu wa kati ya asilimia 11 na 13. Iwapo unyevu utakuwa chini ya kiwango hicho inashauriwa kunyunyizi maji kwenye ufuta kabla ya kukamua.

  VIFAA VYA KUKAMULIA MAFUTA
  - Mashine ya daraja
  - Sufuria - Vifungashio
  - Mifuko midogo ya nguo au viroba vyenye upana wa sentimita 20 na urefu wa sentimita 20.
  - Chombo cha kukinga mafuta.
  - Chujio safi
  - Lebo
  - Lakiri Malighafi
  - Mbegu za ufuta safi
  - Maji safi

  UKAMUAJI MAFUTA
  - Nyunyuzia maji kidogo kwenye ufuta ili kuongeza unyevu kufikia asilimia 11 hadi 13. Mafuta hutoka vizuri kwenye kiwango hicho cha unyevu.

  - Jaza ufuta kwenye vifuko vya nguo au viroba

  - Vipange vifuko hivyo kwenye silinda na kuanza kuzungusha mhimili hadi mafuta yaanze kutoka kupitia matundu ya silinda.

  - Acha kwa muda mafuta yaendelee kutoka kisha endelea kuzungusha mhimili hadi mafuta yaishe. Mhimili ukiacha kuzunguka ni dalili kuwa mafuta yamekwisha.

  - Kusanya mafuta, chuja na fungasha kwenye chupa safi zilizochemshwa. Hakikisha chupa ni kavu na zina mifuniko.

  - Weka lebo na lakiri
  - Hifadhi mahali pakavu na pasipo na mwanga mkali.

  MASHINE YA RAM
  Mashine ya Ram ina uwezo wa kusindika kilo 7 za mbegu za ufuta kwa ufanisi wa asilimia 57%.Aina ya Ram (BP-30) ina uwezo wa kukamua lita 20 za mafuta kwa siku.

  VIFAA
  - Ndoo
  - Mashine ya Ram
  - Kichujio au kitmbaa safi
  - Vifungashio safi

  UKAMUAJI
  - Anika mbegu za ufuta juani kwa kuzitandaza kwenye mabati ili zipate joto la kutosha.

  - Lengo la kuanika mbegu juani ni kurahisisha ukamuaji wa mafuta.

  - Jaza mbegu za ufuta kwenye mpare wa kulishia

  - Funga wenzozuia (HANDLE)ili mbegu za ufuta zisitoke.

  - Nyanyua wenzozuia mpaka juu ili kuruhusu mbegu za ufuta kuingia kwenye silinda.

  - Shusha wenzozuia chini ili kuruhusu pistoni kusukuma mbegu za ufuta ziingie ndani ya eneo la shindilio

  . - Nyanyua tena wenzozuia mpaka juu na kushusha na wakati huohuo ukiendelea kujaza mbegu za ufuta kwenye mpare wa kulishia. Wenzoinua ukiwa mzito ni dalili kuwa msukumo wa kutosha umejengeka. Msukumo huo utasababisha mafuta kutoka.

  - Mafuta yanapoanza kutoka legeza wenzozuia ili kuruhusu mashudu kutoka.

  - Chuja na hifadhi mafuta kwenye vyombo safi vyenye mifuniko vilivyochemshwa.

  MATUMIZI
  Mafuta ya ufuta hutumika katika mapishi mbalimbali ili kuongeza ladha. Pia husaidia kuleta nguvu na joto mwilini. Mbegu za ufuta huchanganywa na vyakula mbali mbali kama mikate, keki, mboga na kadhalika.

  Kwa hisani ya mdau MITIKI -KILIMO KWANZA: KILIMO BORA CHA UFUTA

   
 2. N

  NewtonPierre New Member

  #501
  Jul 8, 2017
  Joined: Jul 7, 2017
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Guys natafuta buyers wa ufuta kwa Dar, bei zikoje, contacts zao
   
 3. NGOSWE2

  NGOSWE2 JF-Expert Member

  #502
  Jul 8, 2017
  Joined: Dec 19, 2013
  Messages: 419
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60
  Wewe unauzaje kwa kilo moja?
   
 4. emmanuel mhecha

  emmanuel mhecha JF-Expert Member

  #503
  Jul 8, 2017
  Joined: Jun 21, 2015
  Messages: 943
  Likes Received: 530
  Trophy Points: 180
  Wonderfull
   
 5. emmanuel mhecha

  emmanuel mhecha JF-Expert Member

  #504
  Jul 8, 2017
  Joined: Jun 21, 2015
  Messages: 943
  Likes Received: 530
  Trophy Points: 180
  Noted
   
 6. j

  jjason john New Member

  #505
  Jul 27, 2017
  Joined: Jul 25, 2017
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  naomba tufahamiane kaka najua utakuwa unauwelewa juu ya hili zao na mm ndio natataka kuanza
   
 7. c

  chino009 New Member

  #506
  Oct 8, 2017
  Joined: Mar 26, 2017
  Messages: 1
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Mwenye ujuzi na kilimo cha ufuta naomba kujua gharama kuanzia uandalizi wa shamba mpaka kuvuna makadirio yawe kwa acre
   
 8. Komba the Great

  Komba the Great Member

  #507
  Jan 1, 2018
  Joined: Apr 25, 2016
  Messages: 70
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  Habari wadau, Kuna mbegu ya ufuta inaitwa Lindi 202, wazoefu wanasema inakomaa haraka na pia ina kiwango kikubwa cha mafuta, naomba kuuliza mwenye kuweza kunisaidia pakuipata hiyo mbegu, nataka jaribu kuipanda na mimi.
   
 9. Mr.Junior

  Mr.Junior JF-Expert Member

  #508
  Jan 4, 2018
  Joined: Sep 8, 2013
  Messages: 8,978
  Likes Received: 4,579
  Trophy Points: 280
  Upo wapi wewe?
   
 10. w

  wise-comedian JF-Expert Member

  #509
  Jan 4, 2018
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,757
  Likes Received: 2,946
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama uko Dar,pwani au Lindi unaweza kuipata kwa gharama ya 5000 kwa kilo.
   
 11. Komba the Great

  Komba the Great Member

  #510
  Jan 5, 2018
  Joined: Apr 25, 2016
  Messages: 70
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  Niko Dar es Salaaam
   
 12. Komba the Great

  Komba the Great Member

  #511
  Jan 5, 2018
  Joined: Apr 25, 2016
  Messages: 70
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  Niko Dar es Salaam Mkuu
   
 13. Mr.Junior

  Mr.Junior JF-Expert Member

  #512
  Jan 5, 2018
  Joined: Sep 8, 2013
  Messages: 8,978
  Likes Received: 4,579
  Trophy Points: 280
  Mimi najua inapatikana Nachingwea kituo cha utafiti mkuu kama una mtu huko mwagize akutumie kwa basi.
   
 14. Komba the Great

  Komba the Great Member

  #513
  Jan 5, 2018
  Joined: Apr 25, 2016
  Messages: 70
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  Asante, Ngoja nijaribu kuona uwezekano huo
   
 15. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #514
  Jan 8, 2018
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 7,953
  Likes Received: 4,090
  Trophy Points: 280
  Nenda Morogoro kwenye kiwanda cha mbegu kinaitwa ASA (Agricultural Seed Agency). Ukiwa unatoka Msamvu stand panda daladala za kwenda mjini shukia Komoa, uliza studio za Abood Radio zilipo fuata hiyo barabara ukishavuka hiyo studio mbele kidogo kama mita 500 hivi utakuwa umefika!! Waambie nimeelekezwa na Kaka Job K kwamba hapa nitapata mbegu ya ufuta aina ya Lindi 202?
   
 16. Komba the Great

  Komba the Great Member

  #515
  Jan 9, 2018
  Joined: Apr 25, 2016
  Messages: 70
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25

  Shukrani Kaka Job K, Nikipata wasaha nitakwenda huko, na haya maelekezo nita ya piga picha na kuyahifadhi katika simu yangu ya kiganjani ili nisipotee. Ila hawa jamaa hawawezi kuwa na wakala wa usambazaji hizo mbegu Jijini Dar es Salaam?
   
 17. Ngatiani

  Ngatiani JF-Expert Member

  #516
  May 21, 2018
  Joined: Apr 6, 2017
  Messages: 331
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 80
  Habari! Napenda kupata taarifa zaidi kuhusu kilimo cha maua. Naomba msaada.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...