Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau | Page 25 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Safari_ni_Safari, Nov 30, 2010.

 1. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 23,171
  Likes Received: 6,884
  Trophy Points: 280
  KILIMO BORA CHA UFUTA
  Ufuta (sesamum indicum)ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga na ukanda wa chini katika mikoa ya Rukwa na Mbeya. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mbegu za zao hili huwa na wastani wa mafuta kiasi cha asilimia 45.


  MAMBO YA KUZINGATIA WA KATI WA KUZALISHA MBEGU
  - Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na bora, inayovumilia mashambulizi ya magonjwa na wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta mengi.

  - Chagua mbegu inayokomaa kwa pamoja ili kurahisisha uvunaji na pia kuepuka upotevu wa zao shambani.

  - Aina nyeupe ya mbegu ya ufuta hupendelewa zaidi kuliko aina nyeusi.

  MBOLEA
  Ufuta unahitaji rutuba ya kutosha ili kutoa mazao bora. Katika kudumisha rutuba ya udongo, tumia kilimo cha mzunguko wa mazao au weka mbolea za asili pale inapobidi.

  PALIZI
  Dhibiti magugu kwa kupalilia ili kuruhusu ufuta kutumia vizuri unyevu na virutubishi. Magugu mengine huwa ni maficho ya wadudu waharibifu wa zao la ufuta.

  MAGONJWA NA WADUDU
  Ufuta hushambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali ambao huweza kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Hivyo kagua shamba mara kwa mara hasa kwenye maua na mapodo ili kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili zamashambulizi, chukua tahadhari mapema kabla ya uharibifu mkubwa haujatokea.

  MAANDALIZI KABLA YA KUVUNAKAGUA SHAMBA
  - Kagua shamba kuona kama ufuta umekomaa.
  - Ufuta hukomaa, kati ya miezi mitatu na minne tangu kupanda kutegemea aina.
  - Aina ya ufuta usiokuwa na matawi hukomaa mapema kuliko ile yenye matawi.
  - Ni muhimu kuwahi kuvuna ili kuepuka ufuta kupukutikia shambani.

  DALILI ZA KUKOMAA UFUTA SHAMBANI
  - Kwa kawaida majani hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya manjano na hatimaye kudondoka.

  - Mashina hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya kahawia.

  VIFAA VYA KUVUNIA
  - Kamba
  - Siko
  - Panga

  VIFAA VYA KUKAUSHIA
  - Sehemu ya kukaushia yenye Sakafu ya saruji
  - Maturubai
  - Sakafu safi

  USAFIRI

  - Mikokoteni
  - Matela ya matrekta
  - Magari

  KUVUNA
  - Vuna ufuta mapema kabla mapodo kukomaa sana na kuanza kupasuka na kuachia punje.Mapodo ya ufuta yaliyokomaa sana yakiguswa au kutikiswa na upepo hupasuka na kuachia mbegu, hali inayosababisha upotevu mkubwa.

  - Mbegu za ufuta ni ndogo na zikidondoka chini ni vigumu kuziokota. Vilevile mbegu zilizodondoka ni vigumu kuzitenganisha na uchafu.

  - Uvunaji wa ufuta huhusisha ukataji wa mimea yenye mapodo kwa kutumia vyombo vya mkono kama panga kwa kukata mashina.

  - Kwa aina za ufuta zenye mapodo yanayopasuka, uvunaji ufanyike wakati mimea bado ni kijani ili kuepuka upotevu wa mbegu.

  - Aidha uvunaji ufanyike wakati hakuna upepo wala jua kali.

  - Baada ya kukata mashina yafunge katika mizigo midogo na kuweka katika vyombo vya kusafirisha kama vile mikokoteni, matela au magari hadi sehemu ya kukaushia.

  - Panga mizigo midogo kwa kusimamisha katika malundo madogo yasiyozidi mizigo minane kwenye sehemu safi za kukaushia.

  KUKAUSHA
  Mapodo ya ufuta hukaushwa yakiwa yamefungwa katika vitita. Vitita huwekwa kwa kuegeshwa kwenye fremu ya kukaushia kwa muda wa wiki mbili hadi tatu kutegemea hali ya hewa. Fremu hii huwekwa juu ya turubai au sakafu ili kuzuia upotevu wa punje kutokana na kupasuka kwa mapodo.

  KUPURA
  Upuraji hufanyika kwenye turubai, mkeka au kwenye sakafu safi.

  - Vitita hupigwa taratibu kwa kutumia mti au hutikiswa vikiwa vimegeuzwa vichwa chini ili kuruhusu punje za ufuta kudondoka kwenye sakafu safi au turubai.

  KUPEPETA NA KUPEMBUA
  Kupepeta na kupembua hufanywa ili kuondoa takataka kama vile mawe, vipande vya mapodo,vijiti na vumbi.Njia bora ya kupepeta na kupembua ni kwa kutumia mikono.

  - Ufuta huwekwa kwenye vyombo kama vile ungo kwa kiasi cha kilo mbili hadi tatu. Ufuta hurushwa hewani kwa kasi ndogo na takataka nyepesi huchukuliwa na upepo. Zile nzito huondolewa kwa mikono.

  KUFUNGASHA
  Mbegu za ufuta zilizo safi huwekwa kwenye vifungashio kama vile magunia madogo ya aina ya juti ya ujazo wa kilo 50.

  - Fungasha mbegu za ufuta kwenye magunia yenye uzito usiozidi kilo 50. Kabla ya kufungasha hakikisha mbegu zimekauka hadi kufikia unyevu wa asilimia 10.

  KUHIFADHI
  - Panga magunia ya ufuta juu ya chaga.
  - Panga kwa kupishanisha ili kuruhusu mzunguko wa hewa kati ya magunia.

  KUSINDIKA MBEGU ZA UFUTA

  Ufuta husindikwa kupata bidhaa ya mafuta ambayo hutumika katika mapishi mbalimbali. Mafuta hukamuliwa kwa kutumia njia za asili na kwa kutumia mashine.

  Njia za asili zina ufanisi mdogo ukilinganisha na zile za kukamua kwa mashine, hivyo ni vyema kutumia mashine. Kuna mashine za aina mbili zinazotumika kukamua mafuta; mashine za mkono na zile zinazoendeshwa kwa injini au mota ya umeme. Mashine za mikono zinazotumika zaidi hapa nchini ni za aina ya daraja (Bridge press) na Ram.

  KUKAMUA KWA MASHINE YA DARAJA
  Mashine ya daraja ni moja ya mashine za kisasa zinazoweza kukamua mafuta ya ufuta. Mashine hizi huendeshwa kwa mikono na zina uwezo wa kukamua mafuta kwa asilimia 68 hadi 72.

  Inaweza kukamua kilo 25 za ufuta kwa saa moja. Ili kupata ufanisi mzuri wa mashine hii, ni muhimu ufuta uwe na unyevu wa kati ya asilimia 11 na 13. Iwapo unyevu utakuwa chini ya kiwango hicho inashauriwa kunyunyizi maji kwenye ufuta kabla ya kukamua.

  VIFAA VYA KUKAMULIA MAFUTA
  - Mashine ya daraja
  - Sufuria - Vifungashio
  - Mifuko midogo ya nguo au viroba vyenye upana wa sentimita 20 na urefu wa sentimita 20.
  - Chombo cha kukinga mafuta.
  - Chujio safi
  - Lebo
  - Lakiri Malighafi
  - Mbegu za ufuta safi
  - Maji safi

  UKAMUAJI MAFUTA
  - Nyunyuzia maji kidogo kwenye ufuta ili kuongeza unyevu kufikia asilimia 11 hadi 13. Mafuta hutoka vizuri kwenye kiwango hicho cha unyevu.

  - Jaza ufuta kwenye vifuko vya nguo au viroba

  - Vipange vifuko hivyo kwenye silinda na kuanza kuzungusha mhimili hadi mafuta yaanze kutoka kupitia matundu ya silinda.

  - Acha kwa muda mafuta yaendelee kutoka kisha endelea kuzungusha mhimili hadi mafuta yaishe. Mhimili ukiacha kuzunguka ni dalili kuwa mafuta yamekwisha.

  - Kusanya mafuta, chuja na fungasha kwenye chupa safi zilizochemshwa. Hakikisha chupa ni kavu na zina mifuniko.

  - Weka lebo na lakiri
  - Hifadhi mahali pakavu na pasipo na mwanga mkali.

  MASHINE YA RAM
  Mashine ya Ram ina uwezo wa kusindika kilo 7 za mbegu za ufuta kwa ufanisi wa asilimia 57%.Aina ya Ram (BP-30) ina uwezo wa kukamua lita 20 za mafuta kwa siku.

  VIFAA
  - Ndoo
  - Mashine ya Ram
  - Kichujio au kitmbaa safi
  - Vifungashio safi

  UKAMUAJI
  - Anika mbegu za ufuta juani kwa kuzitandaza kwenye mabati ili zipate joto la kutosha.

  - Lengo la kuanika mbegu juani ni kurahisisha ukamuaji wa mafuta.

  - Jaza mbegu za ufuta kwenye mpare wa kulishia

  - Funga wenzozuia (HANDLE)ili mbegu za ufuta zisitoke.

  - Nyanyua wenzozuia mpaka juu ili kuruhusu mbegu za ufuta kuingia kwenye silinda.

  - Shusha wenzozuia chini ili kuruhusu pistoni kusukuma mbegu za ufuta ziingie ndani ya eneo la shindilio

  . - Nyanyua tena wenzozuia mpaka juu na kushusha na wakati huohuo ukiendelea kujaza mbegu za ufuta kwenye mpare wa kulishia. Wenzoinua ukiwa mzito ni dalili kuwa msukumo wa kutosha umejengeka. Msukumo huo utasababisha mafuta kutoka.

  - Mafuta yanapoanza kutoka legeza wenzozuia ili kuruhusu mashudu kutoka.

  - Chuja na hifadhi mafuta kwenye vyombo safi vyenye mifuniko vilivyochemshwa.

  MATUMIZI
  Mafuta ya ufuta hutumika katika mapishi mbalimbali ili kuongeza ladha. Pia husaidia kuleta nguvu na joto mwilini. Mbegu za ufuta huchanganywa na vyakula mbali mbali kama mikate, keki, mboga na kadhalika.

  Kwa hisani ya mdau MITIKI -KILIMO KWANZA: KILIMO BORA CHA UFUTA

   
 2. Jcoder

  Jcoder JF-Expert Member

  #481
  Jul 27, 2016
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 496
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Pwani,morogoro pia ni mikoa unaweza lima ufuta. Tatizo ambalo naliona ni wanunuz wa huo ufuta kuwa na bei ya ajabu. Mnunuz mkubwa naye mjua ni MO ila yy this tme alikua ananunua kwa1600Tsh kwa kg 1 ya ufuta.
   
 3. p

  primaquin Senior Member

  #482
  Jul 27, 2016
  Joined: Apr 27, 2014
  Messages: 114
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Asanteni na vipi gharama za kulima ekari moja?
   
 4. Freedom tommorrow

  Freedom tommorrow JF-Expert Member

  #483
  Jul 27, 2016
  Joined: Jan 31, 2015
  Messages: 1,708
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  kilimo cha ufuta hakina gharama kama una eneo tayari. unaweza sema kulima ekari moja ni 50,000/= kutegemea na mahala, mbegu 10,000/= hivi kutegemea na mahala, dawa ya kupulizia 16,000/= ambayo unaweza kupulizia mara 2 kwa vipindi tofauti kwani ufuta huwa unashambuliwa sana na wadudu, unaweza kukodi mpuliziaji 10,000/= palizi 25,000/=.... lakini mkuu hesabu hiyo kwa wakulima wa huku Rufiji sijui sehemu nyingine.... Rufiji ufuta unastawi lakini kutegemea na eneo ila kwa kilwa huwa wanavuna ufuta mwingi sana kulinganisha na huku
   
 5. f

  frank255 Member

  #484
  Jul 27, 2016
  Joined: Jul 17, 2016
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mkuu ufuta unastawi ukanda wote wa pwani na maeneo ya karibu nayo, Wilaya zinazoongoza ni Liwale, Kilwa, Nachingwea, Luangwa, Masasi, Tunduru, Songea pia Ifakara, Tanga kiufupi ni maeneo mengi sana mpaka Mbeya ufuta unalimwa. Kuhusu gharama ni za kawaida kama mchangiaji alivobainisha hapo juu na bei kwa miaka mitatu hii (tangu 2014) umekua ukiuzwa Tshs 1500-2000. Na bei zinatofautiana kutokana na maeneo. Mfano maeneo ya Kilwa mpaka Tunduru wanunuzi wananunua kupitia vyama vya ushirika hivyo kuna ushuru kadha wa kadha lazima walipe ndio maana bei yao huwa chini tofauti na mikoa wanayouza magulioni ambako gharama za mnunuzi zinakua ndogo mpaka bei huonekana kubwa. Asante.
   
 6. p

  primaquin Senior Member

  #485
  Jul 27, 2016
  Joined: Apr 27, 2014
  Messages: 114
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Asante mkuu
   
 7. s

  stweka JF-Expert Member

  #486
  Jul 27, 2016
  Joined: Jun 9, 2016
  Messages: 422
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
  Ufuta una gharama sana,kupalilia hatua kumi kwa kumi buku 1,kupanda kwa kutwa moja buku5,kwa mpandaji na mchimbaji mashimo buku7,hapo hujanunua dawa za kupulizia magugu na za kupulizia wadudu,kukata kutwa buku 5 kiufupi ukitaka kulipa ufuta jipange
   
 8. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #487
  Aug 1, 2016
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  jf ni kila kitu nimepata hili wazo la kilimo cha ufuta nika google moja kwa moja ikanileta jf,michango yenu mizuri sana nimepata ,na nimeridhika na michango niliokuwa nahitaji, .
   
 9. Mr.genius

  Mr.genius JF-Expert Member

  #488
  Aug 1, 2016
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 80
  Karibu sana mkuu kwenye ulimwengu wa Great Thinkers

  Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
   
 10. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #489
  Aug 5, 2016
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  tuko pamoja humu ahsante sana genius
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #490
  Sep 28, 2016
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,663
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Msimu wa mwaka huu bei ya ufuta ilikuwa kiasi gani /kg?
   
 12. F

  FORWARD JF-Expert Member

  #491
  Oct 3, 2016
  Joined: Feb 17, 2014
  Messages: 703
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Nimeanza na kuchoma kichaka ekari 5 ili nianze upandaji katikati ya mwezi wa 12 maeneo ya mwaya, moro.
   
 13. ELIAS MICHAEL MORRIS

  ELIAS MICHAEL MORRIS JF-Expert Member

  #492
  Oct 3, 2016
  Joined: Sep 26, 2016
  Messages: 368
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 80
  mimi ndugu zangu nataka nijalibu kilimo cha mpunga, nimetafuta mashamba ya kukodi maeneo ya tuliani morogoro wanataka laki 1 kwa kila heka hivyo nimeona bola nikachukue heka 5 japo nilitamani sana heka 10 sema ndo ivyo nina laki 5 tu ya kukodishia shamba, ivi ndugu zangu soko la mpunga likoje na aina gani ya mbegu ni nzuri ni inaweza toa gunia ngapi kwa heka?
   
 14. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #493
  Oct 12, 2016
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,663
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Wakuu naomba jibu la swali hili tafadhali
   
 15. M

  Markomx JF-Expert Member

  #494
  Oct 14, 2016
  Joined: Apr 23, 2016
  Messages: 708
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 180
  ilianza 2000 1 kg ikashuka hadi 1500,
  mwaka huu bei ilikua chini sana,ila mwaka huu nazan itakua juu kwani wakulima wengi wamekata tamaa na bei ya ufuta,hivyo wengi watabadilisha mazao
   
 16. O

  Omerta JF-Expert Member

  #495
  Dec 10, 2016
  Joined: Jan 3, 2016
  Messages: 3,194
  Likes Received: 2,459
  Trophy Points: 280
  Mkuu nielekeze nitakapoweza kuuza huu ufuta nina kama kg 400-600 maeneo ya morogoro
   
 17. M

  Mzee Kijana JF-Expert Member

  #496
  Jan 3, 2017
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 763
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 80
  Wadau vipi kuhusu Dar na maeneo ya karibu kama vile Mkuranga na Kisiju ufuta unakubali?
   
 18. Teacher J

  Teacher J Member

  #497
  Apr 4, 2017
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Naomba kwa anayefahamu changamoto za zao la ufuta nipate msaada

  shambani kwangu ufuta unabadilika rangi rangi kuwa njano then kukauka wakati ndio unaelekea kutoa maua[​IMG][​IMG][​IMG]
   
 19. Bigbon

  Bigbon JF-Expert Member

  #498
  Apr 23, 2017
  Joined: May 21, 2016
  Messages: 595
  Likes Received: 694
  Trophy Points: 180
  Mkuu endapo ufuta umekomaa halafu mvua inanyesha unafanyaje ili ukate ama ukiukata utunze sehemu gani ili ubaki ubora wake.kwa mwaka huu 2017 maeneo ya Mkoa wa pwani ufuta umekoma lakini bado mvua zinaendelea kunyesha tu
   
 20. T

  Tunkamanin JF-Expert Member

  #499
  Jun 7, 2017
  Joined: Feb 27, 2015
  Messages: 558
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 180
  The same thing inatokea kwangu. Please tunaomba majibu nataka nianze kukata 15-06-2017 ila ndio hivyo Lindi huku.
   
 21. GEBA2013

  GEBA2013 JF-Expert Member

  #500
  Jul 6, 2017
  Joined: Feb 22, 2014
  Messages: 3,217
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Sh Ngapi Kilo Moja Ya Ufuta
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...