mkuu kwasasa kitunguu gunia ni sh ngap,maana mm ndo nimevuna tangu juz,sokoni kupoje,,napatikana Dodoma

grade gani kama ni ya kwanza haitazidi 65 na kama ni sekela haizidi 30. kwa dar nadhani kwa sasa haizidi 90,000
 
ya kwanza na sekela

Mkuu, soko la vitunguu kwa sasa limeyumba sana na kwa kweli kilimo cha vitunguu hakilipi kama huko nyuma pengine kwa sababukuu mbili. Kwanza, uchumi wa mtu mmoja mmoja na wafanya biashara umeyumba. Lakini sababu kuu ni kwamba watu wameshtuka na kwa sasa vitunguu vinalimwa na vinastawi kila mahali, hivyo production imekuwa kubwa na demand iko pale pale. Tulizoea vitunguu vinatoka mang'ora, iringa na singida. Lakini leo hata Bagamoyo vitunguu vinalimwa....!!!

Hivyo kupata bei unayotaka ili angalau ikurudishie gharama zako ni ngumu sana.
 

Asante mkuu,umenena jambo la msingi sana,maana kwa sasa kitunguu sio kama miaka 9 iliyopita,,ntauza rejareja tu,maana debe ni 20-18 hvyo napata faida kwa kila gunia,
 
Kaka Malila na wadau woye humo habari za kazi. Naomba mawasiliano yako Bw. Malila nikuone ili unipe mwanga kwenye Kilimo. Ahsante
 
kaka karibu, kilimo kinataka roho ngumu, bila uvumilivu lazima utoke nduki na jembe begani.
 
I wish wale vijana wenzetu wanaovalia suruali chini ya makalio wangepita huku wakajifunza kitu..tatizo hawafikirii nje ya box.
 
sikulima nyingi. nililima nne....nilipata hasara ya tsh 13,000,000. ndiyo sababu naweka mambo wazi ili kama mtu anaingia ajue anaingia katika mazingira gani. Kama una roho nyepesi unaweza kufa kwa pressure
Mkuu inabidi uwaambie watu ni kwanini Ulipata hasara ili wachague kunyoa ama kusuka. Sababu ni zipi kati ya hizi? 1.ilikuwa ni first time kusema hukujua ABC za kilimo husika? 2. Utunzaji ulikuwa hafifu? 3. Ulilima kilimo cha simu? 4. Kwa kutokujua ABC za kilimo husika kuna magonjwa yaliyotokea kati hukuyatambua mapema? 5. Ulivuna vizuri ila ukakuta mzigo mwingi sokoni hence bei ikakupiga? 6. Ulivuna vizuri ukakutana na mvua ikaharibu mazao yako? Ukala hasara?



Pia wakulima tujifunze kuwa hizo takwimu za "utapata gunia 100-120 kwa heka" kuwa mara nyingi zinatolewa na wauza pembejeo hivyo tuwe makini nazo hiyo ni biashara yao tusitegemee kama watainenea vibaya. Pia sokoni kina pembejeo fake zakutosha tu tuwege makini sana.
 
Kwa hili nakuunga mkono, uko sahihi kabisa.
 

bei imeshuka sana kwa sababu wafanyabiashara wameyumba kwa sababu ya hali ya uchumi.....gharama za utunzaji hazishuki hasa pembejeo...zimepanda. I mean bei za pembejeo hazishuki.
 
 
Asante sana kwa maelezo yako ya kutoa hamasa, mimi ndo napambana kulima heka tatu na ndio naanza sijawah kulima hata siku moja. nalima kilimanjaro maeneo ya miwaleni.
 
Asante sana kwa maelezo yako ya kutoa hamasa, mimi ndo napambana kulima heka tatu na ndio naanza sijawah kulima hata siku moja. nalima kilimanjaro maeneo ya miwaleni.
Hongera sana mkuu, miwaleni ipo wilaya gani?
 
Naomba kuuliza, nataka kulima vitunguu heka moja, nimeambiwa mbolea ya yara milla winner ni nzuri sana. Swali langu je kwa heka moja natakiwa nitumie mifuko mingapi? Na ninatakiwa nirudie kuweka mara ngaoi mpk kuvuna?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…