mkuu kwasasa kitunguu gunia ni sh ngap,maana mm ndo nimevuna tangu juz,sokoni kupoje,,napatikana Dodoma

grade gani kama ni ya kwanza haitazidi 65 na kama ni sekela haizidi 30. kwa dar nadhani kwa sasa haizidi 90,000
 
ya kwanza na sekela

Mkuu, soko la vitunguu kwa sasa limeyumba sana na kwa kweli kilimo cha vitunguu hakilipi kama huko nyuma pengine kwa sababukuu mbili. Kwanza, uchumi wa mtu mmoja mmoja na wafanya biashara umeyumba. Lakini sababu kuu ni kwamba watu wameshtuka na kwa sasa vitunguu vinalimwa na vinastawi kila mahali, hivyo production imekuwa kubwa na demand iko pale pale. Tulizoea vitunguu vinatoka mang'ora, iringa na singida. Lakini leo hata Bagamoyo vitunguu vinalimwa....!!!

Hivyo kupata bei unayotaka ili angalau ikurudishie gharama zako ni ngumu sana.
 
Asante mkuu,umenena jambo la msingi sana,maana kwa sasa kitunguu sio kama miaka 9 iliyopita,,ntauza rejareja tu,maana debe ni 20-18 hvyo napata faida kwa kila gunia,
 
Kaka Malila na wadau woye humo habari za kazi. Naomba mawasiliano yako Bw. Malila nikuone ili unipe mwanga kwenye Kilimo. Ahsante
 
kaka karibu, kilimo kinataka roho ngumu, bila uvumilivu lazima utoke nduki na jembe begani.
 
I wish wale vijana wenzetu wanaovalia suruali chini ya makalio wangepita huku wakajifunza kitu..tatizo hawafikirii nje ya box.
 
sikulima nyingi. nililima nne....nilipata hasara ya tsh 13,000,000. ndiyo sababu naweka mambo wazi ili kama mtu anaingia ajue anaingia katika mazingira gani. Kama una roho nyepesi unaweza kufa kwa pressure
Mkuu inabidi uwaambie watu ni kwanini Ulipata hasara ili wachague kunyoa ama kusuka. Sababu ni zipi kati ya hizi? 1.ilikuwa ni first time kusema hukujua ABC za kilimo husika? 2. Utunzaji ulikuwa hafifu? 3. Ulilima kilimo cha simu? 4. Kwa kutokujua ABC za kilimo husika kuna magonjwa yaliyotokea kati hukuyatambua mapema? 5. Ulivuna vizuri ila ukakuta mzigo mwingi sokoni hence bei ikakupiga? 6. Ulivuna vizuri ukakutana na mvua ikaharibu mazao yako? Ukala hasara?

Pia wakulima tujifunze kuwa hizo takwimu za "utapata gunia 100-120 kwa heka" kuwa mara nyingi zinatolewa na wauza pembejeo hivyo tuwe makini nazo hiyo ni biashara yao tusitegemee kama watainenea vibaya. Pia sokoni kina pembejeo fake zakutosha tu tuwege makini sana.
 
Mkuu, soko la vitunguu kwa sasa limeyumba sana na kwa kweli kilimo cha vitunguu hakilipi kama huko nyuma pengine kwa sababukuu mbili. Kwanza, uchumi wa mtu mmoja mmoja na wafanya biashara umeyumba. Lakini sababu kuu ni kwamba watu wameshtuka na kwa sasa vitunguu vinalimwa na vinastawi kila mahali, hivyo production imekuwa kubwa na demand iko pale pale. Tulizoea vitunguu vinatoka mang'ora, iringa na singida. Lakini leo hata Bagamoyo vitunguu vinalimwa....!!!

Hivyo kupata bei unayotaka ili angalau ikurudishie gharama zako ni ngumu sana.
Kwa hili nakuunga mkono, uko sahihi kabisa.
 
Mkuu inabidi uwaambie watu ni kwanini Ulipata hasara ili wachague kunyoa ama kusuka. Sababu ni zipi kati ya hizi? 1.ilikuwa ni first time kusema hukujua ABC za kilimo husika? 2. Utunzaji ulikuwa hafifu? 3. Ulilima kilimo cha simu? 4. Kwa kutokujua ABC za kilimo husika kuna magonjwa yaliyotokea kati hukuyatambua mapema? 5. Ulivuna vizuri ila ukakuta mzigo mwingi sokoni hence bei ikakupiga? 6. Ulivuna vizuri ukakutana na mvua ikaharibu mazao yako? Ukala hasara?

Pia wakulima tujifunze kuwa hizo takwimu za "utapata gunia 100-120 kwa heka" kuwa mara nyingi zinatolewa na wauza pembejeo hivyo tuwe makini nazo hiyo ni biashara yao tusitegemee kama watainenea vibaya. Pia sokoni kina pembejeo fake zakutosha tu tuwege makini sana.

bei imeshuka sana kwa sababu wafanyabiashara wameyumba kwa sababu ya hali ya uchumi.....gharama za utunzaji hazishuki hasa pembejeo...zimepanda. I mean bei za pembejeo hazishuki.
 
Mkuu tindo tatizo lako dogo tu. Ilikuwa mara ya kwanza kulima ulipaswa uanze kidogo ili ujifunze kwa gharama kidogo. Biashara yoyote unapoianza mara ya kkwanza mieleka ni kawaida, kama unapojifunza kuendesha baiskeli. Mtu asitarajie anapoanza jambo kwa mara ya kwanza apige bingo haiko hivyo. Pia ukae ukijua kuwa kunapokuwa na mafuriko ya zao sokoni wanunuzi wote na si madalali peke yao hunyanyasa sana wakulima. Hali hiyo ipo katika kilimo cha nyanya pia. Mkoa wa Morogoro ukilima nyanya za kiangazi mwezi wa nane hadi wa kumi na moja huwa kuna mafuriko ya nyanya. anaevuna miezi hiyo na kkama ni mara yake ya kwanza ataapa kwamba nyanya si biashara. Kuna msemo huku NYANYA NINYANYUE NYANYA NINYANYASE. Soko zuri la vitunguu ni mwwezi March hadi June. Ukiweza kuwa na kitunguu majira hayo huna maumivu. wateja wanakutafuta na unaweza kuuza kwa utaratibu unaotaka wewe. wakati huo wewe mwenye mali ndio mjanja. suala la madalali linakuwa halina umuhimu na wala si lazima upeleke sokoni na hata ukipeleka sokoni mzigo wako utagombaniwa.

Tumia utaallam uweze kuhifadhi kitunguu uweze kulifikia soko la Mwezi March, au lima vitunguu uvune February au uvune kuanzia mwezi May hadi July. Ukilima kitunguu cha msimu ambacho kila mtu analima maumivu yake ndiyo hayo. Kwenye suala la soko kunapokuwa na mafuriko hakuna serikali itakayokusaidia hapo utakuwa umeumia tu. wewe mkulima ndiyo unatakiwa uchemshe bongo kuona utalifikia vipi soko la mwezi March hadi July. Hii miezi hakuna dalali atakae kunyanyasa. Na pia sio lazima upeleke mzigo sokoni kunawanunuzi wazuri tu hufuata mazao mashambani. watu wengi wanafanikiwa sana kwa kuuzia mashambani. kama huna uzoefu afadhari ukauzia shamba ukapata bei utakayoridhika nayo kuliko kwenda mjini ukakutana na madalali wajanja ukarudi kijijini na story tu huna pesa mfukoni.

Kwa hiyo Mkuu kila biashara inachangamoto zake. Tumia muda mwingi kujifunza kwa wazoefu badala ya kulalamika hivyo. Ulikosea kuanza kwa kulima pakubwa ukapata hasara ukarudia makosa yaleyale kwa kulima pakubwa zaidi huku hujarekebisha kilichokutia hasara ulipo anza. Ushauri wangu msimu wa kwanza jifunze mbinu za kilimo cha vitunguu uzijue changamoto zake. Msimu unaofuata boresha uzalishaji kwa kutatua changamoto, pata ushauri kwa wazoefu. Panua eneo kadri unavyopata uzoefu. Hata kama unauwezo mkubwakifedha usianze kuwekeza eneo kubwa kama huna uzoefu. Usivutiwe na takwimu tamu unazosikia nyingi hufikiwa na wazoefu na nyingi ni exagerated. Ukizalisha eneo dogo inakupa picha halisi itakayokufanya uamue iwapo kilimo hicho kinalipa au la. Na hapo ndiyo utaamua kupanua eneo la shamba kwa kutokana na picha halisi uliyoiona na changamoto zake.
 
Asante sana kwa maelezo yako ya kutoa hamasa, mimi ndo napambana kulima heka tatu na ndio naanza sijawah kulima hata siku moja. nalima kilimanjaro maeneo ya miwaleni.
 
Naomba kuuliza, nataka kulima vitunguu heka moja, nimeambiwa mbolea ya yara milla winner ni nzuri sana. Swali langu je kwa heka moja natakiwa nitumie mifuko mingapi? Na ninatakiwa nirudie kuweka mara ngaoi mpk kuvuna?
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom