Wakuu salamu,

Nataka kuanzisha kilimo cha umwagiliaji cha kitunguu. Naomba ushauri wenu ni maeneo gani yanayoofaa kwa kilimo cha kitunguu na hasa ambayo yanaweza kuwa na maji kwa ajili ya umwagiliaji.

Nimenunua power tiller ambayo nategemea itanisaidia sana kwenye kilimo cha umwagiliaji!
Kilimo Kwanza!

BAADHI YA WADAU WANAOHITAJI KUELEWA KILIMO HIKI

MICHANGO YA WADAU KUHUSU KILIMO HIKI
Oky, thanks very much Indeed!!
 
Habari Wana jamii
Nina uhitaji wa Miche ya vitunguu maji kwa ajili ya kuotesha shamba la ekari 2. Miche ikiwa Arusha itakuwa vizuri zaidi
 
Safi sna mkuu,

Haya ndio mawazo tunataka hapa JF,

Kuna technolojia mpya na rahisi mno nimeinyaka sehemu juu ya huu ulimaji bado naimalizia resecrh yake nafikiri baada ya miezi sita itakua imekamilika nitaimwaga hapa jamvini.

Kifupi inawezekana kabisa kuchagua ukubwa wa kitunguu chako, kukuza ndani ya miezi miwili tu na kuchangua shape ya kitunguu.

Hii nikiikamilisha nitaileta hapa maana nafikiria kuteka soko lote la Comorro, Kenya na Zanzibar kwa vitunguu bora kabisa na vya bei nafuu na hakuna atakaye shindana na mie.
Mkuu ulifikia lengo la kuteka soko? Maana bei ya kitunguu masokon haishikiki kwa sasa
 
Sisi mabepari utatuweza lakini? Au unasema!

Kama unataka kwenda Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya kitunguu nenda, ukiweza nenda Kibakwe Mpwapwa pia kuna bonde zuri sana na wanalima pia kibiashara. Nenda Mbeya vijijini kuna kitunguu cha kufa mtu au kajichanganye Karatu( Mang`ola),

Maeneo hayo bei ziko juu,kama hutajali nenda kafanye survey bonde moja huko Kipatimu,watu wanalima vitunguu pia,huko bei ya ardhi inaweza kuwa karibu na bure.

Shime nenda shambani leo usingoje kesho.
Kipatimu ipo mkoa gani?
 
Ruaha Mbuyuni.
Nililima mang'ola kijiji cha kisiriri mwaka 2010 mzee mmoja akaniambia mwanangu umetoka chuo huku hatulimagi kwa kufuata elimu njoo nyumbani nikupe dawa uwekee uzio shamba lako na kwa vile shamba lako liko njiani watu wenye macho mabaya watahamisha mazao hutopata kitu, basi nikamshirikisha jamaa yangu tuliyekua tunafanya naye hiyo project akaniambia nimesomea kilimo Mimi ni mtaalamu hapo tuzingatie madawa, mbolea maji hachana na mambo ya kishirikina basi mzee nikamtolea nje akaniambia hili shamba mkilikinga mtatoa scania mbili na nusu ila mkipuuza hamtopata kitu, ebwana we kuja kuvuna tulipata gunia kumi, next year nikasema sikubali nikaenda kwa mzee mmoja milimani huko akanipa dawa nililima mahindi sio vitunguu manake kule ilikua ukikodisha shamba la kulima vitunguu unapovuna unaweka mahindi, nilfuata vigezo na masharti aisee alikuja jamaa na fuso nikamuuzia mahindi mabichi ekari sits, nilivyokunja pesa nilisepa nimevaa pensi na vesti niliacha begi na kila kitu, manake kule walikua na msemo kua mgeni hata aje na mil 500 tutamfirisi hadi akose nauli ya kurudi alikotoka so nilisepa kama nipo around vile sikubeba chochote zaidi ya mapene, mang'ola wale wambulu, mang'ati na wanyiramba Wa kitongoji cha kisiriri niliwavulia kofia kwa uchawi, na historian ya hicho kitongoji cha kisirri ni kijiji kipo iramba huko so wale wachawi waliofukuzwa iramba ndo wakaja kukaa hapo mang'ola na kuliita hill eneo kisiriri.
 
Kilimo bila uchawi unacheza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom