Mchanganyiko wa nyanya, parachichi na vitunguu maji ni sahihi kiafya?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,694
6,396
Nimepanga niwe ninaula huo mchanganyiko mara tatu kwa wiki. Ni kachumbari ya nyanya, parachichi na vitunguu maji.

Japo naweza kuitumia bila ya kuiwekea chumvi, ikiwekwa alau kidogo ladha yake inakuwa nzuri sana. Hata hivyo, kwa kuwa lengo langu kuu si shibe wala ladha bali afya, nimekuwa nikitumia bila chumvi.

Maswali yangu ni kama ifuatavyo:
1. Kuna hasara yo yote ya kiafya kula pamoja nyanya, parachichi na vitunguu maji?

Nafahamu kuwa parachichi na nyanya zinakubalika kuliwa pamoja, lakini sina uhakika kwa upande wa vitunguu maji.

Nimeangalia mtandaoni lakini siajapata jibu.

2. Kuna hasara yoyote ya kiafya endapo chumvi kidogo itawekwa kwenye huo mchanganyiko kwa lengo la kuboresha ladha?

Ni hayo tu Wakuu! Naomba kuwasilisha.

Asanteni🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom