Naam, ukitaka kupata hela weka hela!
 
Daah faida ndogo sana..... Kwelii hakuna kazi nyepesi....
 
Naomba kujuzwa gharama za kilimo cha vitunguu kwa heka moja wadau, kwa Iringa na Kilimanjaro

Nawasilisha

Kwa kilimanjaro.

Kwanza mbegu kwa eka utatakiwa kusia kilo tatu mpaka nne. Ukinunua mbegu dukani hiyo ni 400,000
Kuandaa kitalu, kusia na kutunza mbegu kwa angalau mwezi mmoja na nusu lazima uwe na angalau 300,000
Kupandikiza ekari moja yenye majaruba yasiyopungua 330= 330,000
Utatakiwa ukishapandikiza uwe na mifuko angalau 12 ya mbolea kila mwezi utatia mbolea (yaani mifuko minne kwa eka) 45,000x12.

Utatakiwa kupiga dawa kila wiki ya kuua wadudu, buster, ya kuondoa baridi etc..dawa pekee itakugharimu si chini ya 80,000 kwa ekari moja kila wiki. Utatakliwa either kupiga dawa ya kuua mbegu za magugu yasiote ambayo ni tsh 17,000-27/ lita kwa ekar unaweza kuhitaji lita mbili. au kungolea majani angalau mara nne tangu kupandikiza mpaka kuvuna.

Kwa eka kila wiki utahitaji kumwagilia. Kwa ekari moja angalau uwe na lita 30 za dizeli/petroli kama pumb unayo.

NB: Omba Mungu utakapovuna Mang'ora au Ngage usiwe msimu wa kuvuna vitunguu maana utapata pressure. wengi wamepata hasara kubwa na wengine wamepoteza maisha. Bei kwa sasa kwa gunia la vitunguu haizidi elfu 60,000. Mimi binafsi nimelima na nimepata hasara isiyo kifani.

Kwa ekar kuanzia kusia mpaka kuvuna angalau uwe na tsh 3mil - 4mil. Lakini usitengee kuwa utavuna upate faida kama story zilivyo. Kama unapesa hivyo nakushauri uiwekeze kwa mambo mengine. Mzunguko wa pesa kwa sasa hakuna. Kitunguu hakilipi kwa sababu kinalimwa kila mahali Tanzania kwa sasa. Weka pesa zako hata fixed deposit.

Nazungumza kutokana na uzoefu. Nitumia zaidi ya mil13 kulima. Nilipovuna nikauza kila gunia kwa 40,000 nikapata hasara zaidi ya milion 10. Usisikie story. The truth is terrifying. Na usije ukachukua mkopo ukitegemea kilimo cha kitunguu kitakulipa. Kabla benki hawajakufikia utakuwa umeshakufa kwa pressure. Nenda ngage, kileo, chekereni, mawala, na sehemu zingine za mkoa wa kilimanjaro utapata story za watu waliokufa kwa pressure mwaka huu kutokana na vitunguu kushuka bei na kutofikia hata gharama za uzalishaji.

unaweza kuja inbox kwa maelezo zaidi. lakini kwa sasa kilimo cha vitunguu is not ideal
 

Mkuu shukrani kwa ushauri mzuri,naomba kuuliza eka moja ya vitunguu inatoa gunia ngapi?
Ahsante
 
Mkuu shukrani kwa ushauri mzuri,naomba kuuliza eka moja ya vitunguu inatoa gunia ngapi?
Ahsante

kwa kawaida inapaswa kutoa gunia si chini ya 80. Lakini shida ni kuwa vitunguu vina grade 3. New entrants huwa hawajui hili na wanalijua siku anapovuna anaishia kuwa broke.

First grade inaitwa Origina - ukiuza hii gunia kwa mfano sh. 80,000
Second Grade inaitwa Masela - Utaiuza kwa nusu ya uriginal yaahi sh 40,000
Third Gade inaitwa Segera - hii unaweza kuiuza hata kwa sh 20,000 au less.

Na katika ekari moja kupata first grade hata gunia 20 si mchezo....in short kama una pesa yote cash ya ekari mbili au tatu - ambapo kwa tatu utatumia si chini ya 8mil. Ni vyema kufanya biashara nyingine au ulime mahindi kwa sababu mahindi yanatunzika kwa muda mrefu kuliko kitunguu ambach huwezi kukitunza store kwa muda mrefu.
 

Shukrani mkuu
 
Kiongozi wewe ulilima hekari ngapi? Maana uliwekeza fedha nyingi sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Navyojua kitunguu ukikilima vizur na kikatoka vzr kitakupa faida,ila ukikosea hesabab utaona wanaolima hawana maana,ila nakuakikishien kwamba kilimo kinalipa sanaaa,usione mm nmepata hasara ukadhan nawe utapata hvyhvyo,lah hasha,nenden shamba hasra zipo hata huku kwenye biashara nyingine,na mkulima au mfanya biashara anaeogopa hasara hafai asilan,hatupend hasara ia unaweza kuiepuka ukiwa makin. Kipi ambacho hakina hasara kwa ulimwengu huu wa karne ya 21? Mbona wengine wanalima na wanapata faida kuu pka wanaacha kaz za kuajiriwa?

Muhimu zingatia muda wa kulima,zingatia usimamiaji,zingatia utunzaji na dawa kwa wakat,itakulipa,hakuna usemi ambao unasema jembe linamtupa mkulima ila kuna usemi jembe halimtupi mkulima
 
Kwa huku kwetu Singida ni ka ifuayo
1. Mbegu lt 10 sawa na 125000/-
2.kulima kwa trekta 40000/-
3.kukodi shamba kama sio lako 60000/-
4.kung'olea majani mara 2 sawa na 60000/-

Jumla inawezafika laki 3
Hiyo usiweke mtu wa kutunza shamba na sio kilimo cha umwagiliaji(pump na mafuta na kutengeneza vijaruba na mitaro). Usitumie mbolea wala usitumie dawa za kuuwa wadudu. Kwa nijuavyo mimi atahitaji Profenac au Profit 720EC, Pamoja na Dawa ya magugu Oxfen. Gharama ni zaidi ya hizo.
 
Naungana na kiongozi katika hili. Kilimo cha kitunguu ni gharama sna. Inaweza ikafika milioni 2 kama unavyosema.
Hii kitu nimecheza nayo ndani ya miaka 3 huko mang'ola karatu nilicho kipata siwez shaur mtu alime hii kitu.Na kwa bei hakisomeki kuna pindi gunia linafika hadi 20,000.Na ukibahatika kuvuna kuanzia mwez wa 12-6 kidogo bei huwa juu.lkn baada ya hapo mkuu jiandae kwa maumivu.Ishu ni ku deal na dengu tuu ndiyo mpango mzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee! Kuhusu dengu soko kale lipo vipi kiongozi?
 
sikulima nyingi. nililima nne....nilipata hasara ya tsh 13,000,000. ndiyo sababu naweka mambo wazi ili kama mtu anaingia ajue anaingia katika mazingira gani. Kama una roho nyepesi unaweza kufa kwa pressure


mkuu kwasasa kitunguu gunia ni sh ngap,maana mm ndo nimevuna tangu juz,sokoni kupoje,,napatikana Dodoma
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…