Kilimanjaro: Pombe ya Simba yatajwa kusababisha vijana kuvimba mashavu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amekifungia kiwanda kinachozalisha pombe aina ya simba kampuni ya Turn Bus Investment, kutokana na kuzalisha pombe zenye kiwango kikubwa cha asidi na kwamba hakifai kwa matumizi ya binanadamu.

Mbali na kufungia kiwanda hicho ameliagiza Shirika la viwago Tanzania (TBS), mkoani humo kuchunguza viwanda vinavyozasha pombe zinazotokana na ndizi , ili kujiridhisha kama zinafaa kwa matumizi ya binadamu .

Akizungumza leo jumatatu Novemba 29,2021 na waandishi wa habaria ofisini kwake, amesema amefungia kiwanda kinachozalisha pombe aina ya Simba kilichopo wilayani Rombo kutokana na kuzalisha pombe ambayo haifa kwa matumizi ya binadamu.

Ameongeza kusema kuwa alifika kiwandani hapo na kuchukua sampuli ya pombe na kupeleka TBS na kwamba majibu yametoka kuwa pombe hiyo inayotokana na zao la ndizi haifai kwa matumizi kutokana na kuwepo kwa asidi nyingi.

"Pombe hii aina ya simba inazalishwa kwa wingi wilayani Rombo na kwamba huenda ndio inawaletea madhara vijana wa wilaya hiyo, kwa kuwa kumekuwepo na malalamiko kama inavyo elezwa kuwa vijana wanavimba mashavu pamoja na madhara mengine ikiwemo kutelekeza familia na watoto kutunzwa na bibi wazee."amesema Kagaigai.

aliongeza kuwa TBS watachukua sampuli ya pombe zinazotokana na ndizi katika viwanda vyote mkoani kilimanjro na kuzichunguza upya ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kuwapata vijana ambao ndio wapenzi wa pombe hizo .

Meneja wa viwango TBS kanda ya kaskazini, Happy Kanyeka, amesema katika kiwanda hicho bidhaa ya simba haijakidhi matakwa ya uzalishaji na kwamba kimefungiwa hadi uchunguzi utakapo kamilika.

"Mbali na kiwanda hicho viwanda vyote vinavyozalisha banana Mkoani Kilimanjaro na mikoa mingine vitachukuliwa sampuli upya ili kujiridhisha"

Aidha amesema watafanya uchunguzi zaidi kwa viwanda vya Rombo, kuchunguza malighafi zinazotengeneza pombe hizo na kwamba huenda hawatumii ndizi bali wanatumia malighafi nyingine ambazo zinapeleka kuleta madhara katika pombe hiyo.

MWANANCHI
 
Kwa mara nyingine tena ni Rombo, Rombo na Rombo. Jamani kunani huko Rombo. Pombe, kuacha familia nyumbani, kusaidiwa kazi na jirani zetu wa upande wa pili n.k. Wakazi wa Rombo mjitafakari.
 
Sasa hadi uzalishaji umeanza bidhaa imeingizwa sokoni TBS walikuwa wap? Ila hii nchi niya ovyo sana
 
Kuvimba mashavu ni tatizo...

Ila kutelekeza familia siyo hoja ni binadamu mwenyewe hata asipotumia pombe anaweza telekeza...
 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amekifungia kiwanda kinachozalisha pombe aina ya simba kampuni ya Turn Bus Investment, kutokana na kuzalisha pombe zenye kiwango kikubwa cha asidi na kwamba hakifai kwa matumizi ya binanadamu.
Kuwa na shavu dodo ni dalili ya kuridhika na maisha, Rombo ndizi, parachichi, supu ya nyama na kitiz (kitimoto) vyote bei che na bia ndiyo usiseme sh 400/= tu mambo safi, utakosaje shavu dodo.
ROMBO OYE.
 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amekifungia kiwanda kinachozalisha pombe aina ya simba kampuni ya Turn Bus Investment, kutokana na kuzalisha pombe zenye kiwango kikubwa cha asidi na kwamba hakifai kwa matumizi ya binanadamu.
Aidha amesema watafanya uchunguzi zaidi kwa viwanda vya Rombo, kuchunguza malighafi zinazotengeneza pombe hizo na kwamba huenda hawatumii ndizi bali wanatumia malighafi nyingine ambazo zinapeleka kuleta madhara katika pombe hiyo.
 
Kuwa na shavu dodo ni dalili ya kuridhika na maisha, Rombo ndizi, parachichi, supu ya nyama na kitiz (kitimoto) vyote bei che na bia ndiyo usiseme sh 400/= tu mambo safi, utakosaje shavu dodo.
ROMBO OYE.
Rombo juuuuuu juuuu zaid
 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amekifungia kiwanda kinachozalisha pombe aina ya simba kampuni ya Turn Bus Investment, kutokana na kuzalisha pombe zenye kiwango kikubwa cha asidi na kwamba hakifai kwa matumizi ya binanadamu.

Mbali na kufungia kiwanda hicho ameliagiza Shirika la viwago Tanzania (TBS), mkoani humo kuchunguza viwanda vinavyozasha pombe zinazotokana
Waziangalie na hizi Energy drinks
 
Simba Dume hatari sana hii kitu.

20210707_182307.jpg
 
Back
Top Bottom