Kweli juu ya Pombe au Kilevi

Kweli juu ya Pombe au Kilevi

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
384
Reaction score
758
UTANGULIZI
Historia ya maandiko na sayansi ya tiba inatuambia juu ya matumizi ya kileo kama tiba ya malazi ya tumbo etc

Kitu chochote kinapotumika pasipo kihasi kinakuwa ni kileo, haijalishi ni kitu cha aina gani ? Neno la Mungu limesisitiza Sana juu ya kiasi

1 Petro 5:8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Kwa hiyo pombe licha ya kutumika Kwa ajili ya matibabu kadiri maendeleo ya sanyansi na technology kuendele matumizi ya pombe yalitoka kuwa tiba na kuwa kileo

Sababu za Kibiblia juu ya Matumizi ya Pombe

Sababu ya Kwanza
Pombe ni roho , Biblia inasema
Waefeso 5:18Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

Kwa hiyo kama kazi ya pombe katika mwili wa Mwanadamu ni Sawa Sawa na kazi ya roho ndani ya mwili wa Mwandamu Kwa hiyo pombe ni roho

Kuna baadhi ya pombe zinamajina kabsa ya spirit na tafsiri ya spirit ni roho Kwa hiyo pombe ni roho.

Kama pombe ni roho , hivyo basi kazi ile ile ambavyo inafanywa na Roho wa Mungu inafanywa na pombe

Madhara ya pombe
A. Kuondoa ufahamu
Madhara ya Kwanza , pombe kazi yake inaondoa ufahamu na kufunga mlango wa akili kumsaidia Mwandamu kufanya kazi na kufungulia Moyo WA mwandamu kumwongoza mwandamu

1 Wakorintho 14:14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.

Mithali 31:4-5 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme;
Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?

[5]Wasije wakanywa na kuisahau sheria,
Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.

Kwa hiyo kazi ya kileo ni kuondoa ufahamu ndani ya MTU kuondoa matunda ya akili ndani ya mwandamu

Ushawaikujiuliza kwanini watu wengi wakiwa wanatumia kileo uwezo wao kufanya maamuzi ya kuyakataa mabaya na kutachagua mema unapungua

Unaweza kuwa na maamuzi mazuri Sana ukiwa haujalewa lakini ukiishaingia kwenye ulevi Yale maamuzi yako yanapotea

Unafikiria kwanini MTU akiwa mwaji anakosa nguvu za kushinda uzinzi, Kwa sababu mlango wa akili unakuwa umefungwa na ndio maana watu ambao wanakuwa wanywaji mara nyingi wanakuwa pia wanaambatana na uzinzi ndani yake

Wengine Kwa sababu ya pombe wanakosa uwezo wa kufunga Miguu Yao wanajikuta wako kwenye ngono na watu ambao hawakutarajia kuwa nao Ila ni kwasababu ya pombe sio kwamba walikusudia Ila pombe ilifungua mlango wa Mwili kutawala Maisha ya mwandamu badala ya akili na Roho ya Mungu
 
Madhara ya pili
Inaondoa nafasi ya Mungu
Mwanadamu aliumbwa Katika utatu na Mungu yaani roho , nafsi na Mwili, na baada ya dhambi kuingia ulimwenguni Roho wa Mungu aliondoka ndani yetu

Mwandamu aliumbwa kuishi duniani kwa msaada wa Roho wa Mungu, Kwa hiyo mara baada ya dhambi , mwandamu alikuwa chini ya roho ya dunia hii

MTU anapotumia kileo anaongozwa na roho ambayo sio roho wa Mungu, Kwa hiyo nafasi ya Roho ya Mungu inaondoka Kwa njia ya pombe , Kwa sababu Mungu ni Mtakatifu hataki michanganyo , ulevi unamwondoa Roho WA Mungu katika nafasi yake

Hosea 4:11Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.

Tito 3:3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


1 Yohana 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. .

Kwa hiyo kazi ya akili ni kukusaidia kumjua Mungu, pasipo akili kutumika sawasawa ni vigumu kumjua Mungu, Kwa hiyo pombe inakuondolewa fursa ya kumjua Mungu na kupokea msaada wake

Madhara ya tatu
Kupokea hekima ya duniani

Ayubu 32:8 Lakini imo roho ndani ya mwanadamu,
Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.

Kama tulipooona hapo awali kwamba pombe ni roho ndio maana inaitwa spirit Kwa hiyo kazi ya roho ni pamoja na kuachilia ufahamu ndani ya mwandamu

Kwahiyo kama kazi ya roho ni kutoa ufahamu ujue kwamba kama Roho wa Mungu anatoa ufahamu WA kimbingu hivyo basi ni sawasawa na roho ya ulevi pia inatoa ufahamu wake Ambao unaitwa hekima ya dunia hii

Yakobo 3:14-17
[14]Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
.
[15]Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.
.
[16]Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.

[17]Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom