Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Licha ya Sheria ya Vileo Sura ya 77 ya Mapitio ya Sheria za Tanzania ya Mwaka 2002 kuelekeza taratibu mbalimbali za kufanyabiashara ya vileo, lakini kwa siku za hivi karibuni kuna viashiria na mazingira ambayo yanaonekana kwenda kinyume mwongozo huo hali ambayo inaacha tafakuri.
Miaka kadhaa iliyopita Serikali ilipiga marufuku matumizi ya pombe za kwenye viroba maarufu kwa jina la 'viroba', pombe hizo zilikuwa zikiuzwa kiholela hali ambayo ilikuwa inaweka hatarini nguvu kazi za Taifa kupitia watumiaji, hata Wanafunzi baadhi ya walidaiwa kutumia pombe hiyo kwa kuwa ilikuwa inapatikana katika mazingira rahisi.
Ni miaka sasa imepita tokea zuio hilo litolewe, lakini hivi karibuni kumeibuka pombe nyingi ambazo zinazalishwa na kuwekwa kwenye chupa ndogo za plastiki, mfano double Kick, Smart Gin, Black Gin…
Pombe hizo zinauzwa kiholela mtaani ambapo asilimia kubwa kwenye Jiji la Dar es Salaam, wafanyabiashara wengi wa bidhaa za kila siku za matumizi ya nyumbani za rejareja ni nadra kuwakuta hawauzi pombe hizo.
Kwenye maeneo mengine hasa yenye mikusanyiko na sehemu za vijiwe baadhi ya vibada vimejengwa na vinauza pombe ya aina hiyo muda wote bila kuzingatia muda na taratibu nyingine zinazotokana miongozo.
Madhara ya kuuza pombe hizi bila utaratibu ni makubwa hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa, kuna vijana wanaanza kunywa pombe hizo asubuhi na mapema na kushinda vijiweni hali ambayo mbeleni kama haitatafutiwa ufumbuzi ikaja kuzalisha wahalifu wengi mtaani kutokana na uteja wa pombe hizo bila kufanya kazi.
Pia kuuzwa kwa pombe hizo kiholela hasa kwenye maduka ya huduma za kijamii za kila siku inaweka uwezekano kwa Watoto au wanafunzi kujihusisha na matumizi ya pombe mapema, ikiwa ni kutokana na pombe hizo kupatikana kwa wepesi muda wote.
Ni muhimu mamlaka husika zikafatilia na kufanya uchambuzi wa kina kubaini athari zinazotokana na suala hilo, pombe hizo kwa sasa imekuwa sawa na viroba vilivyobadilishiwa vifungashio.
Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app