Arusha na Kilimanjaro kuna ongezeko kubwa la pombe za makopo zisizokuwa na Viwango

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko Kubwa la kila aina za pombe ambazo huwekwa katika vichupa na kufungwa vizuri na kisha kusambazwa madukani na katika bar ndogo ndogo za mtaani.

Katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro hali ni mbaya kutokana na ongezeko la kila siku la aina za pombe na nyingi zimekuwa zikitengenezwa kienyeji na kusambazwa madukani na bar za mtaani.

Pombe hizo hutengenezwa na watu tofauti tofauti majumbani kwao, na wengine hufungua ofisi ndogo kwa ajili ya kazi hiyo huku wakiwa hawana ujuzi wowote na wala vibali.

Pombe hizo nyingi zikiwa ni za vikopohazina viwango maalumu vya ulevi bali wahusika hubandika kiwango chochote cha kilevi nje ya kopo.

Madhara ni mengi yamekuwa yakioenekana kwa watumiaji wa pombe hizo ikiwa ni pamoja na kukohoa damu, miguu kulegea baada ya kunywa pombe hizo. Kuchubuka midomo na wengine kuvimba uso.

Wengi wa watumiaji wa Pombe hizo wamekuwa wakiziita sumu, au hutumia neno "nipe sumu" wakati wa kuagiza pombe hizo.

Pombe hizo zimekuwa kimbilio la wengi hususani vijana kutokana na kwamba zinauzwa bei rahisi hivyo ni rahisi kumudu gharama,na kiwango cha ulevi pia kipo juu.
 
Back
Top Bottom