Kilichonifanya niache kuamini kwenye dini

Kilichonifanya niache kuamini kwenye dini

Nasubiri kuona mapovu ya wafia dini, woiiiiiiiiiih.
Maana wameguswa penyeweee [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23][emoji23]

Ahahh wanakuja kumtetea shetani aka mungu[emoji23]
 
Na pia ubaya wa dini imeshakwisha kujimilikisha Mungu yaani inaamini kuwa yenyewe ni kazi ya Mungu / imetengenezwa na kuletwa na Mungu wakati ni matokeo ya watu Kama tu ilivyo sayansi ambavyo ni matokeo ya watu wenye akili walioanzisha .Sasa yenyewe dini imeshakwisha kujimilikisha na Mungu kwa hio ni kazi Sana kwao kuamini kuwa Mungu alieanzisha dini anakosea

Kama mungu alikua hana source je dunia haiwezi kuwepo bila mkono wa mtu?)
 
Watu wa dini wengi humu naona wameishia kumtisha na kumtamkia maneno ya sio na manufaa mtoa mada. Hii inaonesha ata wao hakuna walijualo juu ya Mungu.
Hoja IPO hapa "kwenye Mungu kujua Kila kitu" inamaana wa motoni anawajua wa peponi anawajua, anajua kesho yako ipoje anajua Leo yako itaishaje, kwaiyo dunian watu tupo kama character wa kwenye movie ambao watazamaji wanajua mwisho wao upoje.

N kweli hapo tafsiri yake mungu ndo shetani mwenyewe
 
Mimi swali langu ni. Ikiwa yeye anafahamu ata kabla hujazaliwa kwa nini anaruhusu azaliwe mtu ambaye hatumuabudu yeye, atakua mdhambi, mtesi na muuaji wa watu.?

Kwa nini anaruhusu mtu azaliwe katika mateso, mfano mtu viungo havipo ambapo ataishi kwa mateso na kuomba omba.

Kaka huwa nawaangalia sana vilema najiuliza kwann mungu kawaruhusu wanakuja wanateseka na kudhalilika dunian
 
Ndugu weka akiba ya maneno!

Siku inakuja utatamani urekebishe japo herufi moja ktk ulichoandika hapa ushindwe,though sipo hapa kukutisha yote ni maoni yako maana unao utashi wako.
hiyo siku ni ipi? uliwahi kuiona?
 
Ametakasika Allah mtukufu.

Muktadha wa swali lako ni kwamba, Allah subhaanahu wataa'la- anawadhulumu/kuwapendelea waja wake kwa sababu atawaingiza peponi/motoni kwa vile anavyotaka yeye.

Lakini Allah subhaanahu wataa'la-hamdhulu yeyote katika viumbe wake, bali amejiharamishia nafsi yake kudhulumu.

Ni kweli Allah kwa elimu yake anajua mafikio ya Kila mmoja wetu ima peponi/motoni.

Lakini kwa hekma zake na uadilifu wake hajajaalia elimu yake kuwa ndio hukmu ya mja kuingia peponi/motoni, bali watu wataingia motoni au peponi kulingana matendo yao(amali).

Ukiisoma Quran kuna Aya ngingi sana Allah amekariri hilo.

Na ndio maana tumepewa khiyari katika kutenda, pia ametuletea mitume wake, Kisha siku ya mwisho kuna kuhesabiwa matendo yetu na kuna mizani.

Kama ingelikuwa hukmu ya kuingia motoni au peponi ni kutoka na elimu ya Allah sasa haya yote yanini?

Hivyo mtu kuingia peponi au motoni ni kutokana na matendo yake.

Amesema Allah mtukufu:-

"Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda."(36:54).

"Na hiyo ni Pepo mliyo rithishwa kwa hayo mliyo kuwa mkiyafanya."(43:72)


Wallahu aa'lam.

Mungu kesho yako anaijua??? Kama hakuna atakae dhulumiwa inakuaje uadhibiwe miaka tofaut na dunian huoni kama sio haki uchomwe na moto wa milele hata dunian kuna vifungo vya maisha ila vina umri fln kwann mungu wako anashindwa utashi na binadamu alio waumba
 
Vijana mkishajua kugegeda mademu mnajifanya mnajua kila kitu na confidence za kijinga jiangalie Sasa kijana utapata tabu bado mdogo

Mungu hadhihakiwi heshimu imani no bora mawazo hayo ungebaki nayo .Ushakuwa mzinzi Sasa unajifanya huamini dini we ndo SHETANI mwenyewe sasa

[emoji28][emoji28][emoji28] nitakua ndo dajjal mwenywe
 
Toka nipo shule ya msingi nilikuwa naenda madrasa sana nikawa najiuliza kama Mungu anajua kesho yetu ina maana hadi motoni na peponi basi katupangia watu wa dini ukiwauliza wanasema anajua ila hajakupangia sasa anachokuwa anajua nini huwa siwaelewi kabisaaa.

Kwa maono yangu Mungu ndio shetani mwenyewe maana kila kitu kakiumba yeye.
Hivi kwanini huwa mnautumia Uislamu kuwasilisha Uongo wenu ?

Yaani usome madrasa halafu useme "Mungu ndiyo shetani" hata kama mlikuwa mnapiga dufu tu hamsomi dini, hili halipo kwa mtu aliye soma madrasa, atafanya ujinga wote ila hatosema kama ulivyo andika wewe.

Jiwekeni mahali penu, msijipenyeze sehemu ambazo siyo zenu, matokeo yake ndiyo haya.

Wewe nakuona wa pili. Wewe siyo Muislamu. Aya yako ya mwisho inathibitisha hilo.

Kuna mja mwema mmoja alipata kusema hivi "Hata uongo ungekuwa ni jambo la halali, yeye asingelifanya kwa lengo la kujitakasa"

UONGO MBAYA SANA.
 
Sitasemea dini ila mimi nitaisemea imani yangu,,

Yeah ni kweli Mungu anatujua vzuri toka tukiwa tumboni mwa mama zetu maana yeye ndio yule alietuumba!!

Kila uumbaji uliofanyika ulikuja na kusudi ndani yake namaanisha kila binadamu kaumbwa kwa kusudi la Mungu, (ndani yake kuna kitu cha kiMungu kakibeba) ili akitimize akiwa hai hapa duniani,

Shetani ni baba wa uovu kazi yake kubwa ni kupotosha ile kweli, anapoona una kitu cha kiMungu ndani yako kazi yake yeye ni kuhakikisha anakupotosha either utumike vibaya tofauti na vile ulivyoumbwa au usitumike kabisaa!!

Narudi kujibu hoja yako sasa, Mungu hakulazimishi uamini katika yeye, kakupa utashi na uelewa, kakupa uwezo wa kujua mema na mabaya!! Kakupa uhuru wa kufanya uchaguzi wako mwenyewe either umtumikie au usimtumikie,, lakini pamoja na hayo kakupa kabisaa na matokeo yake kule mwisho ni nini, umtumikie ili urithi uzima wa milele au usimtumikie ili uende Jehanamu!!!

Amekuumba wewe hivyo anakujua wewe vizuri anachotaka yeye umwamini kwa uhuru, umwabudu kwa uhuru na kwa kumaanisha ndani yako, kiasi kwamba hata kama utapitia vishawishi gani basi uwe tayari kuitetea imani yako,, ila kama ukiteteleka kiimani ukaacha kumfuata yeye basi na yeye atakuacha usubiri hukumu yako mwisho, ila kama utatubu na kurejea tena kwa kumaanisha yupo tayari kukupokea tena!!

NB: Yeye hataki mtu yeyote apotee anatamani wote waufikie uzima wa milele,

anaowatufuta yeye ni wale wamwabudua halisi na si wale wanaomwabudu kisa tu hawaana namna nyingine ya kufanya

Hulazimishwi ndo maana mwisho wako uko mikononi mwako mwenyewe

Umezunguka sana kaka kujua kesho yako n kupi akat matendo ndo yanadetermine sku yako so anajua matendo yako ya kila sku au hajui?
 
mi nina swali Je huyo mungu alitoka wapi? nahitaji jibu lenye logic
 
Mungu hayupo, shetani hayupo.

Habari za kuwepo kwa Mungu na shetani ni hadithi walizotunga watu tu.

Ndiyo maana swali lako halina jibu lililo logically consistent.

Kweli bro Kiranga mungu wavitabu vya dini hayupo dunian au huenda alishakufa maana anashindwa kujitetea kwnn asitokee tu aondoe mkanganyiko huu
 
Kati ya jambo la hatari sana katika maisha ya Kiroho na ambalo shetani analifurahia ni dhana ya kumfikiria kwamba shetani ni kiumbe mwenye sura mbaya na Mwenye pembe na makucha marefu.

Mara nyingi utaona picha zinazomuwakilisha shetani ni picha za kutisha sana.

Ki uhalisia shetani hana Sura mbaya ya namna kama anavyowasilishwa, bali shetani ni malaika aliyeasi.

Sasa shetani na malaika zake hutenda kazi kwa kuvaa uhusika wa Kiumbe fualani au Mwanadamu.
Mfano: alipoenda kumdanganya Hawa alivaa umbile la nyoka ambaye nyoka alikuwa mzuri na mwerevu kuliko wanyama wote:
(Mwanzo 3:1).

Kwa hiyo kazi ya shetani na malaika zake wanafanya kazi kwa kujibadilisha.
2 Wakorintho 11:14
Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Mfano mwingine ni pale ambapo shetani alijifanya yeye ndio Petro na kuanza kupinga kifo cha Yesu, lakini Yesu alitambua huyu ninayezungumza naye sio Petro Bali ni shetani katika umbile la Petro, na ndio maana Yesu alipokea hakusema rudi nyuma yangu Petro Bali alisema rudi nyuma yangu shetani.
Mathayo 16:21-23)

Kwa hiyo shetani anaweza kuja kwako kwa maumbile mbalimbali, kulingana na udhaifu wako, Shida yako, mazingira uliyopo nk.

Shetani anaweza kujifunua kwako kama: Mchungaji, mume wako, mchumba wako, Baba yako, jirani yako nk.

Na mara nyingi shatani anajifunua kwetu kupitia vitu tunavyo vipenda na vyenye mvuto mzuri, shatani anafanya kazi na mashirika, viwanda na makampuni makubwa ya Dunia hii. Mfano anaongiza viwanda kutengeneza nguo zisizo na maadili, ili watu waingie katika uasherati na uzinzi.

Sasa tutamtambuaje shetani anapokuja kwetu kwa maumbile ya ndugu, jamaa na marafiki?

Kikubwa tunahitaji kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu kwa kusoma Maandiko na kuomba ili tujazwe Roho Mtakatifu.

Na hatimaye Roho Mtakatifu ataweza kutupambanulia hila zote za shetani pindi anapokuja kwetu kama malaika wa Nuru.
Mathayo 7:15,16
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

Kwa hiyo ndugu yako, bosi wako, jirani yako, rafiki yako nk anaweza kuwa ndio Sura na umbo ambapo shetani amejifunua kwako.

Wakati fulani tunaenda katika nyumba za ibada na mhubiri anakuwa ni shetani mwenyewe kwa umbile la Mchungaji wako au Nabii wako.

Mungu akubariki

Mungu alikua anajua kama shetani atakuja kubadilika au alikua hajui?? Kesho yako mungu s anaijua nambie anaijua vipi kupinga msemo wako
 
Back
Top Bottom