Umeuliza swali rahisi sana. Jibu lake ni hili swali wewe unajua ni wa motoni au peponi ? Kama hujui na umepewa akili na afya njema, kwanini usitende wema ukaenda peponi ?
Maana halali iko wazi na haramu iko wazi. Kujua kwake Allah kila kitu hakukuzuii wewe kutenda unachotaka. Ndiyo maana ule uhuru alio kupa ukatafakari kwa mtindo huu.
Ngoja nikupe mfano mdogo, leo hii kwa sisi tulio jaaliwa watoto, mathalani kwa kumjua mwanao kinaga ubaga, ukimpa hela tu kiasi fulani unajua kabisa huyu lazima ataenda kununua kitu fulani, mfano labda pipi, na kweli baada ya dakika kadhaa anarudi na pipi. Ila kwa Mola kujua kwake ni kwa hakika kabisa kwa asilimia mia tofauti na sisi.
Kunakufikiri na kuna kufikiri kwa usahihi. Hili nalo linataka elimu.