Kati ya jambo la hatari sana katika maisha ya Kiroho na ambalo shetani analifurahia ni dhana ya kumfikiria kwamba shetani ni kiumbe mwenye sura mbaya na Mwenye pembe na makucha marefu.
Mara nyingi utaona picha zinazomuwakilisha shetani ni picha za kutisha sana.
Ki uhalisia shetani hana Sura mbaya ya namna kama anavyowasilishwa, bali shetani ni malaika aliyeasi.
Sasa shetani na malaika zake hutenda kazi kwa kuvaa uhusika wa Kiumbe fualani au Mwanadamu.
Mfano: alipoenda kumdanganya Hawa alivaa umbile la nyoka ambaye nyoka alikuwa mzuri na mwerevu kuliko wanyama wote:
(Mwanzo 3:1).
Kwa hiyo kazi ya shetani na malaika zake wanafanya kazi kwa kujibadilisha.
2 Wakorintho 11:14
Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
Mfano mwingine ni pale ambapo shetani alijifanya yeye ndio Petro na kuanza kupinga kifo cha Yesu, lakini Yesu alitambua huyu ninayezungumza naye sio Petro Bali ni shetani katika umbile la Petro, na ndio maana Yesu alipokea hakusema rudi nyuma yangu Petro Bali alisema rudi nyuma yangu shetani.
Mathayo 16:21-23)
Kwa hiyo shetani anaweza kuja kwako kwa maumbile mbalimbali, kulingana na udhaifu wako, Shida yako, mazingira uliyopo nk.
Shetani anaweza kujifunua kwako kama: Mchungaji, mume wako, mchumba wako, Baba yako, jirani yako nk.
Na mara nyingi shatani anajifunua kwetu kupitia vitu tunavyo vipenda na vyenye mvuto mzuri, shatani anafanya kazi na mashirika, viwanda na makampuni makubwa ya Dunia hii. Mfano anaongiza viwanda kutengeneza nguo zisizo na maadili, ili watu waingie katika uasherati na uzinzi.
Sasa tutamtambuaje shetani anapokuja kwetu kwa maumbile ya ndugu, jamaa na marafiki?
Kikubwa tunahitaji kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu kwa kusoma Maandiko na kuomba ili tujazwe Roho Mtakatifu.
Na hatimaye Roho Mtakatifu ataweza kutupambanulia hila zote za shetani pindi anapokuja kwetu kama malaika wa Nuru.
Mathayo 7:15,16
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
Kwa hiyo ndugu yako, bosi wako, jirani yako, rafiki yako nk anaweza kuwa ndio Sura na umbo ambapo shetani amejifunua kwako.
Wakati fulani tunaenda katika nyumba za ibada na mhubiri anakuwa ni shetani mwenyewe kwa umbile la Mchungaji wako au Nabii wako.
Mungu akubariki