Ngona niendeleze kazi yangu kwenu nyinyi msio kuwa na maarifa wala kutafakari, nilijua hata ukijibu lazima utakosea.
Naanzia hapa, akili huwezi kuiona japo ni hali au uwezo wa mtu kujizuia kutokana na kukosea, hii ndiyo akili. Kwahiyo hata ubongo usagwe sagwe namna gani akili huwezi kuiona. Kwahiyo najua nina akili au kutokuwa na akili kwa kurejelea ile maana ya akili.
Kadhalika njaa ni hali vile vile, ambayo kwyo huijua kupitia maana yake na viashiria kwa kuzingatia maana yake, japo si kila hali haionekani, bali kila hali ina ishara zake zinazo onyesja uwepo wa hali hiyo. Nikacheka sana uliposema kwamba kwamba ukiwekewa camera unaiona njaa, nikasema kweli utakuwa huna tofauti na mwanao kwa akili ndiyo maana angeweza kujibu maswali yako, kwenye field ya uhandisi umeme kuna kinafaa kinaitwa "Thermography" hiki ni kifaa kinachopima hali joto na athari zake katika kifaa, bila ushirikiano wa nje, yaani athari ya ndani, kinakuonyesha picha kwa maana ya athari tu kulingana na namna kilivyofanisiwa na muhusika, kingesanifiwa kionyeshe maduara kuthibitisha hali joto ya ndani basi kingefanya hivyo. Kwahiyo njaa haionekani hata kwa nini, ila kwa kuzingatia maana ya njaa na ishara zake ndipo tunaitambua njaa.
Kadhalika maumivu ya kuachwa, achana na porojo za sayansi ambaz hata nikitaka unithibitishie hutaweza, jibu sahihi ni kuwa huzuni inafasiriwa kihisia na kimaana, na kihisia unaijua huzuni kulingana na hali unayo isikia na mfaungamano yako na jambo husika.
Maswali yangu umejibu ila hujapatia katika kujibu maswali husika na umeweka uongo mwingi.
Uwepo wa Jahanamu upo na hakika, kama ilivyo njaa inavyothibitishika. Hakuna aliye ona Jahanamu kwa macho ila tunaamini na lusadikisha sababu maneno hayo yametoka kwa Mola muumba na ni ya kweli. Yaani kuna ishara zinazo onyesha uwepo wa jambo hilo.