Toka nipo shule ya msingi nilikuwa naenda madrasa sana nikawa najiuliza kama Mungu anajua kesho yetu ina maana hadi motoni na peponi basi katupangia watu wa dini ukiwauliza wanasema anajua ila hajakupangia sasa anachokuwa anajua nini huwa siwaelewi kabisaaa
Ametakasika Allah mtukufu.
Muktadha wa swali lako ni kwamba, Allah subhaanahu wataa'la- anawadhulumu/kuwapendelea waja wake kwa sababu atawaingiza peponi/motoni kwa vile anavyotaka yeye.
Lakini Allah subhaanahu wataa'la-hamdhulu yeyote katika viumbe wake, bali amejiharamishia nafsi yake kudhulumu.
Ni kweli Allah kwa elimu yake anajua mafikio ya Kila mmoja wetu ima peponi/motoni.
Lakini kwa hekma zake na uadilifu wake hajajaalia elimu yake kuwa ndio hukmu ya mja kuingia peponi/motoni, bali watu wataingia motoni au peponi kulingana matendo yao(amali).
Ukiisoma Quran kuna Aya ngingi sana Allah amekariri hilo.
Na ndio maana tumepewa khiyari katika kutenda, pia ametuletea mitume wake, Kisha siku ya mwisho kuna kuhesabiwa matendo yetu na kuna mizani.
Kama ingelikuwa hukmu ya kuingia motoni au peponi ni kutoka na elimu ya Allah sasa haya yote yanini?
Hivyo mtu kuingia peponi au motoni ni kutokana na matendo yake.
Amesema Allah mtukufu:-
"Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda."(36:54).
"Na hiyo ni Pepo mliyo rithishwa kwa hayo mliyo kuwa mkiyafanya."(43:72)
Wallahu aa'lam.