Point of no return

Point of no return

insane

Member
Joined
Jun 9, 2026
Posts
16
Reaction score
26
Ilikuwa ni siku ya graduation kumaliza kidato cha nne siku hiyo mvua ilikuwa na inanyesha vibaya mno wenye wapenzi wao walikuwa wamekumbatiana huko bwaloni huku mziki ukigonga watu hawaelewi, sisi tusiokuwa na wapenzi na hatuna vaibu ya mziki tumetulia tu mahali baridi inatupiga.

Lakini hatukukaa kinyonge tulikuwa tumekaa na mdada mmoja hivi nae ametulia tu wala hana mambo mengi. Katika kupiga stori tugamgusia maswala ya mapenzi. Lengo ilikuwa tukafanye mapenzi tulimshawishi sana lakini alikataa. mpaka tukawa tunahisi au hawa huwa hawafanyi maana alikuwa mtu wa dini dini sana. tukamwambia kabisa. kwani nyie huwa hamfanyi?. alicheka sana na kusema sio kwamba hawafanyi ila mtu atakayemuoa ndiye atakayeenjoy penzi lake na bikra. Tulishawishi sana lakini tulishindwa. tulimwambia tu magdalena siku ya mwisho haitakuwa na thamani hiyo Kwa miaka karibuni 11 kuwa pamoja hatujakuwa na hazi ya kusex pamoja. Na mazingira yalikuwa yanaruhusu kabisa. Ile mvua pamoja na kelele ya mziki hakuna ambae angetuona wala kutuhisi.

Anyway tuachane na hayo hiyo haikuwa sehemu ya story. Katika sehemu ya kufulahi kumaliza kidato cha nne tulikuwa na trip ya kwenda ziwa tanganyika kuenjoy yaani baada tu ya graduation kesho asubuhi asubuh tunakwea pipa Tunaenda zetu kuenjoy ziwa tanganyika. Watu waliohitaji kwenda waliwasilisha majina yao na michango. Kesho asubuhi safari ikarod to tanganyika. Watu walikuwa vaibu sana kwenye gari kuimba mix matusi humohumo na hakuna anaejali kuwa kuna viongozi tulioongozana nao. Watu walikuwa wakitulizana wenyewe, wanaotulizwa wanasema kwanini hawakupanda private maana tulienda na gari mbili basi pamoja na private car moja basi kelele ziliendelea ilionekana walitaka wenyewe kukaa sehemu iliyochangamka. Kuna sehemu gari inasimama tunanunua vya kununua tunaunga mbele. Mpaka tukafika tulipokua tunaenda.

Hatua ya kwanza ilikuwa kuungana na wanafunzi wa shule ya huko tuliowakuta pamoja na kufanya vijisemina semina vilivyokuwa sehemu ya ratiba. Baada ya kufika saa9 tukaelekea ziwani kwenyewe watu walikatazwa kuogelea mpaka wapewe utaratibu. Basi tukawa tunaangalia mazingira tu yalivyomazuri miti mirefu pamoja na minazi sijui migazi maana ilinichanganya baada ya kuwauliza wenyeji kuwa napata wapi hapa minazi mimi nilikuwa naifahamu kama minazi lakini wenyewe walinikatalia hiyo sio minazi ni migazi basi nikashindwa kuelewa lakini nikawakubalia tu wenyeji.

Baada ya utaratibu kufuatwa watu tulianza kuoga. Mimi nilikuwa ni fundi katika kuogelea maana huku kwetu kuna mto lakini kumbe maji ya mto na maji ya ziwa ni tofauti hilo sikujua. Sasa ambacho nilifanya na nilijuta ni kwenda mbali na fukwe ambayo ilikuwa ni idea yangu toka tunajiandaa na safari kwamba nikifika nitaogelea hata katikati ya maji kisha kurudi. Sasa nikaanza vizuri kuogelea huku nyuma watu wakinishangilia nikaenda mbali kiasi sasa nikaanza kuhisi kuchoka. kama tu huu umbali nimekoka hivi itakuwaeje wakati wa kurudi. Dah nikageuza hapohapo nikaanza kurudi lakini ajabu oga na kuoga lakini sisogei mbele yani unatumia nguvu nyingi kuoga lakini na kuchola lakini upo pale pale husogei mbele ukisogea labda yamekuhamisha yenyewe sasa kukuhamusha ni either yakupeleke mbele au yakurudishe nyuma tena nilijuta mpaka nikataka kuanza kulia. Nikiangalia wenzangu kule wengine walishaanza kucheka kweli mpaka wanadondoka chini.

Nikaona hapa nisipaniki nitumie ufundi na kujifunza kitu kipya. Idea iliyokuja chapu niache kuogelea kisha nizame nianze kutumia both miguu na mikono kunisogeza mbele kwa maana ukiwa unaogelea mikono tu ndio inafanya kazi ya kukusogeza ila miguu yenyewe kukufanya uelee. Nilizama Kweli mbinu ilifanikiwa lakini ilihitaji pumzi maana inatakiwa uwe ndani ya maji kuepuka yale mawimbi ya juu kukuchezesha huku na huku. Nilifanikiwa kutoka ila hamu ya kuoga ikaisha pale pale. Nikachukua tu simu nikaanza kupiga picha pamoja na kushoot

Sasa ile napiga picha kakatokea kaboti ka kisasa kamefungiwa mashine kanatembea hatari. Nikaanza kukachukua picha kanaenda huku kanarudi huku. Basi ni funjo. Kakienda huku nakafata kakirudi narudi. Muendeshaji baada ya kuniona akasogea karibu ili nichukue picha vizuri. Baanzi ya wenzangu pia waliookaona walikuja. Sasa ile mimi napiga picha wenzangu waliomba kupanda. Dah niliumia ningejua na mimi ningechangamkia furusa mapema ili nipande. Nikang'ang'ania kupanda pale lakini nafasi ikawa haitoshi. Mbaya zaidi waliopanda walikuwa ni viongozi wa safari wakawa wananiambia dogo toka hapa tutakuchapa viboko lakini yule dereva mshikaji nikama hakulizika alipenda nipande mimi bahati mbaya nafasi ilikuwa haitoshi walishaiwahi walimu. Nikavunga.

Sasa yule mshikaji (dereva) akawapa maelekezo wale ndugu zake watatu aliokuja nao waende nyumbani. alikuja na wadogo zake wakike watatu nazani ni ndugu zake tu au marafiki maana walikuwa hawatofautiani sana kiumli kuwa ni ndugu wa familia moja. Akawapa maelekezo waende nyumbani afu yeye akabaki na kale kachopa. Wale ndugu zake walikuwa wazuri ajabu. Ni kama warabu fulani hivi lakini sio moja kwa moja kiufupi ni chocolate. Midomo yao niya rangi nyeusi. Wanene hivi na shepu inaonekana. Sikuwafatilia mwanzo kwasababu akili ilifocus kwenye chopa.

Jamani walikuwa wazuri mpaka nikashindwa kujizuia na kuwambia jamani nyinyi mbona wazuri hivyo wakawa wanacheka tu. yani ukimwangalia huyu unahisi kabisa ni mwanamke wa ndoto yako. Basi nikazuia Tamaa nikamfata mmoja na kumuomba picha kweli akakubali na wenzie ndiyo wakawa wapiga picha.

Wale wengine wakavutiwa na picha mjongeo (muliro's quote) nilizokuwa nikiwachukua pale walipokuwa na boti wakawa bize kuangalia. tukawa huru kidogo na hii pisi nyingine. Nkamuelezea vile nimempenda na kunichanganya. Akawa anacheka akawaambia na wenzake sikieni huyu eti ananipenda. Pia wanalafudhi ya arusha nikama wenyeji wa arusha. Wenzie wakasema tumbebe tu akakuoe. Nayeye akasema kwakweli nimepata kakijana kazuri zuri kakanioe. Ikawa kama utani utani kila huyo anaogea la kwake huku safari ikiendelea bila mimi kujua. nakuja kushituka tulipotoka sijui njia.

Lakini sikuonesha kama nimeingiwa na wasiwasi. Tunapiga stori, tunacheki picha tulizopiga kwenye simu. Sometime namuuliza kitu kwenye simu nikiwa nakijua kabisa. Anaacha kuangalia simu ananiangaliaa basi anaguna tu. Namuuliza nini? Anasema aah. Anyway wenyewe walikuwa hawaelewi kama mimi ni mgeni.

Tumetembea tembea lakini ikafika sehemu ambayo sielewi kabisa kwamba hapa nikisema nirudi naenda kusini au kaskazini. Mpaka Wale mademu wengine wawili walishafika kwao tukaachana nao tukabaki wawili tu nae anaenda tu uvumilivu ukanishinda nikaanza kujiuliza ivi kwanza nimefata nini huku. Na ndio wazo la kuwa nilimtongoza huyu likarudi maana mda wote nilikuwa nawaza nilishapotea. Nikawa tu nafikili ivi mimi sina akili kisa mwanamke nimefika huku nikamwambia mimi narudi. Akasema imekuaje tena mpenzi.

Itaendelea
 
Back
Top Bottom