Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,904
- 4,630
Kwamba Dr. Slaa anapendwa hili halina ubishi.. kuna makosa ambayo CCM wameyafanya kwenye kampeni hii ambayo sikutarajia kwa chama kikongwe na chenye kujua propaganda kingeweza kuyafanya. Makosa haya yanaweza kuigharimu CCM vibaya sana. Ninaamini matokeo makubwa ya kushangaza yatatoka Tanzania vijijini ambako kuna watu wameendelea kutuambia kuwa "ati wanakijiji hawajui tuwape elimu". Watu ambao watatudisappoint sana nina wasiwasi inabakia Dar! Hawa watu wa Dar ndio tatizo kubwa sana la mabadiliko nchini...
.
Ni kweli mkuu, mfano mzuri wa vijiji ni chaguzi ndogo zilizopita. Ccm na serikali yake walishangazwa na ujasiri wa wanavijiji hasa huko Busanda, B/vijijini na tarime. Kama sii kutumia nguvu kubwa na mabavu wasingeambulia hata jimbo moja. Jijini DSM uswahili umezidi na watu wenye njaa wanaotafuta mlango wa kutokea hata kwa kuuza haki yao ya uzaliwa.
DR SLAA HANA BILIONI HAMSINI, HANA FUSO ZA KUWABEBA WASHABIKI KWENYE MIKUTANO YAKE ILA ALIMELIBEBA TUMAINI LA WATANZANIA LILILOPOTEA. HICHO NDICHO KITU WATU WANAKITAKA KUTOKA KWAKE!