Elections 2010 Kikwete apewa report ya kura za Slaa

Status
Not open for further replies.
Kwamba Dr. Slaa anapendwa hili halina ubishi.. kuna makosa ambayo CCM wameyafanya kwenye kampeni hii ambayo sikutarajia kwa chama kikongwe na chenye kujua propaganda kingeweza kuyafanya. Makosa haya yanaweza kuigharimu CCM vibaya sana. Ninaamini matokeo makubwa ya kushangaza yatatoka Tanzania vijijini ambako kuna watu wameendelea kutuambia kuwa "ati wanakijiji hawajui tuwape elimu". Watu ambao watatudisappoint sana nina wasiwasi inabakia Dar! Hawa watu wa Dar ndio tatizo kubwa sana la mabadiliko nchini...

.
Ni kweli mkuu, mfano mzuri wa vijiji ni chaguzi ndogo zilizopita. Ccm na serikali yake walishangazwa na ujasiri wa wanavijiji hasa huko Busanda, B/vijijini na tarime. Kama sii kutumia nguvu kubwa na mabavu wasingeambulia hata jimbo moja. Jijini DSM uswahili umezidi na watu wenye njaa wanaotafuta mlango wa kutokea hata kwa kuuza haki yao ya uzaliwa.
DR SLAA HANA BILIONI HAMSINI, HANA FUSO ZA KUWABEBA WASHABIKI KWENYE MIKUTANO YAKE ILA ALIMELIBEBA TUMAINI LA WATANZANIA LILILOPOTEA. HICHO NDICHO KITU WATU WANAKITAKA KUTOKA KWAKE!
 
Habari zilizopatikana ndani ya kikao cha siri kati ya vigogo waandamizi wa usalama wa taifa,Kikwete na Kinana wiki iliyopita zimedokeza kwamba JK amepokea report inayoonyesha kura za Dk Slaa atakazopata october 31 2010.

Mpashaji wa habari amebainisha ya kwamba baada ya JK kupewa tathimini hiyo hakuamini alichoambiwa, zaidi aliongea kwa kiingereza maneno mawili '' Is it?''.

Hii ni taarifa fupi iliyotolewa wiki tatu zilizopita ikulu jijini dar es salaam ikiwa ni mpango wa usalama wa taifa kukamilisha awamu ya kwanza ya utafiti wao kwa baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa, kati, pwani na kaskazini. Machache yameibwa kwenye taarifa hiyo:

Mara: Dr Slaa 59.7%
Mwanza:Dr Slaa 58.3%
Kigoma:Dr Slaa 52.7%
Singida: Dr slaa 34.7%
Shinyanga: Dr Slaa 43.2%
Kilimanjaro: Dr Slaa 51.7%
Arusha: Dr Slaa 47.1%
Manyara: Dr Slaa 53.8%
Tanga:Dr Slaa 46.2%
Dar es Salaam: Dr Slaa 66.4%
Geita: Dr Slaa: 62.7%
Kagera: Dr Slaa 48.2%
Dodoma: Dr slaa 42.4%
Tabora: Dr Slaa 57.6%

Wait a minute. Usalama wa taifa wanamfanyia kampeni mgombea urais, JK. So campaigning for JK is among responsibilities of TISS. Tanzanians pay salaries of TISS for them to campaign for one political party and not for the interest of whole nation, Why?
 
Mkuu post yako hakika inachoma mioyo yetu. Naamini behind this wapo UwT manunuzi ambao kwao kuzima maisha ya mtu ni sawa na kuzima mshumaa. hawajui kwamba unapomuua mtanzania mmoja ni sawa unamuua mwanao mchanga kwa kosa la kunyea mkono.
Hapo kwenye bold unaweza kutupatia data japo clue on why and how does that happen? Na kama imetokea Tanzania hii why not to approach The Hague for cleansing this sin?

Kura yangu na familia yangu na wafanyakazi wenzangu tumeshaamua kumnyima mzee wetu mpendwa kikwete, tutampa mtu anayeonesha kutujali zaidi yaani Dr. Slaa.

My $100m bet.....Huyu jamaa hamwongelei mlinzi wa CJ?
 
Kinachonishangaza ni jinsi watu wanavyompa "thanks" aliyewalisha upupu wa data za hovyo. Wengine kama MMJJ huwa naamini kuwa ni mwana falsafa kumbe yumo kundini mwa vipofu
 
Issue ya REDET na Synovate waulize wenyewe... lakini ukitumia medula oblangata uliojaliwa na Mungu, ulizia uchaguzi wa serikali za mitaa CCM iliibuka na kura kiasi gani? Alafu jiulize ni kitu gani cha ajabu kimetongea tangu wakati huo mpaka sasa? Jiulize kipi CHADEMA imekuja nacho cha ajabu ambacho kitaweza kubadili matokeo kiasi hicho? Jiulize CCM inaowabunge wangapi? Niulize CCM inatarajia kupata wabunge wangapi? Jiulize wabunge na madiwani wa CCM ambao wametapakaa nchi nzima hawana mchango kwa kura za Rais wao.

Sisi waTanzania watu wa ajabu sana tunaamini mazingaombwe mno....

Huwezi kutumia matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kama benchmark ya uchaguzi mkuu. Huu ni utaahira wa hali ya juu. Mengine malizia mwenyewe.
 
Hizi observations zinaweza kuwa kweli kwani kama hali ingekuwa swali kwenye kambi ya ccm kusingekuwa na sababu ya kumuongezea ratiba ya kampeni mgombea ambae wanajua afya yake inamgogoro! Mara baada ya Idd Jakaya amepangiwa full ratiba ya kampeni hivyo inaashiria kuwa Dr. Slaa watu wameanza kumkubali hivyo ccm wamepata mchecheto!!

Maji yapo shingoni ndiyo maana wamebadirisha ratiba. kwani wakati wanapanga ratba ya kwanza si walijua itaendelea hata baada ya Idd? Tatizo ccm wanakwenda kusi kwa ngalawa wakati pepo ni za kasi na zenye mawimbi makubwa na dhoruba.
 
Wait a minute. Usalama wa taifa wanamfanyia kampeni mgombea urais, JK. So campaigning for JK is among responsibilities of TISS. Tanzanians pay salaries of TISS for them to campaign for one political party and not for the interest of whole nation, Why?

Mkuu unategemea nini when TISS is not impatial and has completely lost its direction! Hebu tafuta mahojiano ya Arcado Ntagazwa na Raia mwemma utaona hili ninalolisema. TISS siyo yetu tena, ni yao. Tunatakiwa kuwapiga bao pamoja na TISS yao ili tuanze kazi ya kulisuka upya hili taifa. Miaka mingine mitano ya hasara ni jambo lisilokubalika hata kidogo.

If we don't screw them now, they do us!
 
Freeman Mbowe 2005 mikutano yake ilikuwa inajaza watu kama hii ya Wilberd Slaana matumizi ya HELKOPTA na la kushangaza Mbowe alikubali kushindwa kwa kishindo tena alihunduria kuapishwa kwa JK wakati CUF na TLP walikataa kukubali matokeo! jee DR. Slaa atakuwa tayari kufuata nyayo za Mwenyekiti wake Mbowe kukubali matokeo ya ushindi wa CCM wa TSUNAMI

CHADEMA munaota ndoto za mchana! hata mwaka 2005 mulikuwa na ndoto hizi hizi za kudai ushindi hewa! sasa ngojeeni 31 october mtakavyo garagazwa! ila tunamuomba Slaa akubali matokeo kama alivyofanya Mbowe 2005!

CHADEMA wacheni FITINA na UMBEA wa kuwasingizia viongozi wa CCM kuwa wananjama za kuwauwa viongozi wenu! huu ni uongo wa wazi kabisa na kama munaushahidi toka kwa USALAMA wenu wa TAIFA si mupeleke tuhuma zenu POLISI? munangoja nini? WACHENI KUWADANGANYA WANANCHI KUWA SLAA ATASHINDA! HUKO VIJIJINI NA MIKOA YA PWANI, KUSINI NA KUSINI MAGHARIBI, MIKOA YA KATI NA ZANZIBAR HAKUNA ANAEMJUWA SLAA ILA HUKO MBULU, UCHAGANI NA BAADHI YA MIKOA YA MAGHARIBI LABDA NDIPO ANAPOWEZA KUAMBULIA KURA CHACHE! TAKWIMU NILIZIWEKA HAPA LAKINI ZIMEFUTWA NA LA KUSHANGAZA NI KUWA FORUM HII INATAKA MAWAZO YA KUMSIFIA SLAA NA CHADEMA NA HUU NI UWOGA! KWANI WANAOAMUA NANI ATAKUWA RAIS SIO JAMII FORUM BALI NI WA TZ! NA WA TZ WENGI WANATEGEMEWA KUMPA KURA ZAO KIKWETE!

SASA KAMA NYINYI HAMTAKI KIKWETE AU LIPUMBA AWE RAIS HAKUNA ANAEWALAZIMISHA LAKINI SIO MULAZIMISHE WATU WOTE WAMPENDE DR.SLAA NA CHADEMA!

MUNASIKIAEEE!!

Good observation; SASA mshauri bwana wako JK awe mstaarabu kama MBOWE alivyofanya 2005. Akubali matokeo kistaarabu atakapojulishwa kuwa Dr. Slaa ameshinda.
 
Mkuu Sikonge,

Una maoni yoyote hapo nilipo-bold?

Ndugu yangu Keil,

Hii habari imenishangaza saana. Sikutegemea Wanyamwezi wangu wawe na mwamko mkubwa namna hii kwa kipindi hiki kifupi. Naona kilimo cha Tumbaku kimewapiga Rumba hadi wenyewe wamepata hamu ya kubadili.

Nilikwama kumpata Sister hadi leo. Tatizo kubwa ni simu yangu ya kikazi ninayotumia, huwa haionyeshi namba na sasa hivi Tanzania wanaogopa simu zinazokuja bila namba. Wanasema huko Kenya watu 70 wamekufa na Arusha wamekufa wawili. Ila yeye nashindwa kabisa kumpata. Labda kaenda Kiloleli ingawa kuna kijana nilimpigia siku moja na nikampata akiwa Kiloleli. Hivyo hadi leo hii sifahamu ni Wabunge gani wa Upinzani huko Sikonge wanagombea. Kama Kakunda alihamia Chadema na Upepo huu, anaweza kuneemeka.

Wanyamwezi wangu wa TABORA Oyeeeeee!!!!!.

Nyie si Mabwege tena. Dr. Slaa tafadhali fika SIKONGE.
 
Wait a minute. Usalama wa taifa wanamfanyia kampeni mgombea urais, JK. So campaigning for JK is among responsibilities of TISS. Tanzanians pay salaries of TISS for them to campaign for one political party and not for the interest of whole nation, Why?

Mkuu kwani ni mara ya kwanza UwT kufanya kazi za kampeni? Mwaka 2005 ni hao hao UwT walifanya kazi ya kum-nominate JK, ndio maana unaona akina Tom Mwang'onda wakapewa u-Bunge wa kuteuliwa na Rais. DG-TISS [Apson] wakati wa mchakato wa nominations ndani ya CCM na uchaguzi ni baba wa Tom Mwang'onda. To me, Tom Mwang'onda kupewa ubunge wa kuteuliwa na Rais ilikuwa ni shukurani kwa Mzee Apson kwa kazi aliyofanya, ambayo hatuijui. Kama unataka more details, kamuulize Mzee Mangula [former CCM Secretary General].

Kuna mengi sana yanafanywa na watu wa UwT linapokuja swala la Uchaguzi Mkuu. Kwa hiyo usishangae na hizo ndio taasisi zetu ambazo zimeundwa kwa sheria za ajabu ajabu zikiongozwa na Katiba ambayo iko outdated. Ukiwaambia CCM tunataka mabadiliko, watakuja na viraka hata kama nguo yenyewe imeishachakaa, mwisho watakuwa wanabandika kiraka juu ya kiraka kingine ili mradi tu wahakikishe kwamba Katiba inaendelea kuwalinda na kulinda maslahi yao binafsi na ya chama chao.
 
Huwezi kutumia matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kama benchmark ya uchaguzi mkuu. Huu ni utaahira wa hali ya juu. Mengine malizia mwenyewe.

Mkuu, utashi wako uko wrong! Serikali za mitaa ndiyo kuna wapiga kura wote. Taswira ya nchi yoyote inaanzia mitaani. Statistics zote unazosikia hizi za REDET etc zinatoka huko na si kwingine. Kwa hiyo haikuwa vema kabisa kumwambia jamaa ulivyomwambia, unless amekukwaza na chadema yenu.
 
.......CHADEMA wacheni FITINA na UMBEA wa kuwasingizia viongozi wa CCM kuwa wananjama za kuwauwa viongozi wenu! huu ni uongo wa wazi kabisa na kama munaushahidi toka kwa USALAMA wenu wa TAIFA si mupeleke tuhuma zenu POLISI? munangoja nini? WACHENI KUWADANGANYA WANANCHI KUWA SLAA ATASHINDA! HUKO VIJIJINI NA MIKOA YA PWANI, KUSINI NA KUSINI MAGHARIBI, MIKOA YA KATI NA ZANZIBAR HAKUNA ANAEMJUWA SLAA ILA HUKO MBULU, UCHAGANI NA BAADHI YA MIKOA YA MAGHARIBI LABDA NDIPO ANAPOWEZA KUAMBULIA KURA CHACHE! TAKWIMU NILIZIWEKA HAPA LAKINI ZIMEFUTWA NA LA KUSHANGAZA NI KUWA FORUM HII INATAKA MAWAZO YA KUMSIFIA SLAA NA CHADEMA NA HUU NI UWOGA! KWANI WANAOAMUA NANI ATAKUWA RAIS SIO JAMII FORUM BALI NI WA TZ! NA WA TZ WENGI WANATEGEMEWA KUMPA KURA ZAO KIKWETE!

SASA KAMA NYINYI HAMTAKI KIKWETE AU LIPUMBA AWE RAIS HAKUNA ANAEWALAZIMISHA LAKINI SIO MULAZIMISHE WATU WOTE WAMPENDE DR.SLAA NA CHADEMA!

MUNASIKIAEEE!!
Pamoja na kiswahili chako kibovu nimekuelewa
ila hizo bold mbili ninakupasha kama ifuatavyo. Kama UwT wanahusika na mchezo mchafu wa kuua demokrasia nchini unatarajia kuna polisi wa kuwakamata? dawa yao pekee ni kura zetu na bunge period.

Hiyo bold ya pili unaonesha wazi kabisa kuwa unafahamu NDOA iliyopo kati ya Lipumba na CCM (nawatoa wanaCUF ktk hili maana hawajui) ndo maana umewaona wagombea wawili waliopo hatarini kupoteza reputation ni hao tu na siyo wagombea wengine wa vyama vingine. Sasa nenda kawaambie core kwamba hali imebadilika na wimbi la mabadiliko limeshachukua kasi halizuiliki.

MWISHO NI KWAMBA VITISHO NA KEBEHI HUWA NI BREAD CRUMBS MBELE YA MWANAMAPINDUZI MAKINI
 
Mkuu, utashi wako uko wrong! Serikali za mitaa ndiyo kuna wapiga kura wote. Taswira ya nchi yoyote inaanzia mitaani. Statistics zote unazosikia hizi za REDET etc zinatoka huko na si kwingine. Kwa hiyo haikuwa vema kabisa kumwambia jamaa ulivyomwambia, unless amekukwaza na chadema yenu.

Ha ha haaa! My dustbin is several meters away from me, lucky you!
 
Kama kweli habari hii isingekuwa na uzito tusingewaona wanaingia kwa fujo vibaraka wa CCM kuponda na kutubeza! Wengine tumesoma pschology na tumejifunza kusoma between the lines. ... utetezi wa akina Kasheshe kwangu ni ushahid tosha kuwa something fishy is going on and there is truth in this.
Pia niliata sikia ishu hii kama wiki 2 zilizopita... ndo maana tunasikia Pinda yuko UN sasa hivi badala ya JK ambaye alitarajia apumzike siku 16 na kufanyiwa ukarabati... :wink:
 
Propaganda ni kisu kinachokata pande zote, inategemea upande upi utaumia. Lakini "tuwaache watoto waende SHULENI, na wakubwa VITANI".
 
Nimesikia ni kweli; muda si mrefu itapatikana tuko tunaitafuta tarifa maalum; wamebana ni ya synovate ndio maana wametoa nusu nusu tu
 
Mwenye kuamini hizo statistics kwa kweli hana tofauti na aliyeamini kwamba CCJ ni chama tishio.....

Badala ya watu kujiuliza au kumuuliza HUTAKI UNAACHA hiyo ''statistics'' au survey iliendeshwaje na kwa sample ya watu wangapi kila mkoa, watu wapo excited kichizi na wanafurahia!

Inawezekana utafiti huo ulihusisha watu wachache mno (wasiozidi hata 100) kwa mikoa hiyo na watu wakaibuka na %!

Kazi bado mbichi sana jamani. Dr. Slaa na kamati yake ya kampeni wakaze buti tu mpaka tarehe 31.10 na tusilose focus kwa vijitakwimu tusivyojua vimepatikanaje.

Let us be a ''home of great thinkers'' for once...
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom