Elections 2010 Kikwete apewa report ya kura za Slaa

Status
Not open for further replies.
You never know if the snake is pregnant.... Juzi nilikuwa vijijini sana ktk mkoa mpya wa Simiyu nikaamua kufanya mini research, ktk wanakijiji 20 niliowahoji, wote wanajua kuwa Dr Slaa anagombea urais kupitia CHADEMA.... Kwa hiyo sibishii wala kushangaa sana hiyo takwimu yako... ingawa kuikubali pia simo
 
Mkuu, utashi wako uko wrong! Serikali za mitaa ndiyo kuna wapiga kura wote. Taswira ya nchi yoyote inaanzia mitaani. Statistics zote unazosikia hizi za REDET etc zinatoka huko na si kwingine. Kwa hiyo haikuwa vema kabisa kumwambia jamaa ulivyomwambia, unless amekukwaza na chadema yenu.
Kama uchaguzi wa serikali za mtaa ndicho kigezo chako hivi Tarime, Busanda na Biharamulo mashariki hawakufanya huo uchaguzi wa serikali za mitaa mbona CCM walitokea dirisha la choo, my friend upepo wa kimbunga huwa hauangalii juzi ulielekea upande gani unakuja kwa kuzunguruka.
 
Issue ya REDET na Synovate waulize wenyewe... lakini ukitumia medula oblangata uliojaliwa na Mungu, ulizia uchaguzi wa serikali za mitaa CCM iliibuka na kura kiasi gani? Alafu jiulize ni kitu gani cha ajabu kimetongea tangu wakati huo mpaka sasa? Jiulize kipi CHADEMA imekuja nacho cha ajabu ambacho kitaweza kubadili matokeo kiasi hicho? Jiulize CCM inaowabunge wangapi? Niulize CCM inatarajia kupata wabunge wangapi? Jiulize wabunge na madiwani wa CCM ambao wametapakaa nchi nzima hawana mchango kwa kura za Rais wao.

Sisi waTanzania watu wa ajabu sana tunaamini mazingaombwe mno....

Kasheshe usijifanye hujui hizi taasisi za utafiti kwa nchi zetu jinsi zinavyofanya kazi na zinafanya kazi kwa maslahi ya nani. Haziko huru katika kutoa matokeo yao na ndio maana mwaka huu wameshikwa na kigugumizi.

Naomba nawe utumie medula oblangata yako kujiuliza, ni kwanini JK ambaye ni mgonjwa ameongezewa ratiba ya kuzunguka kwa ajili ya kampeni? Siku ya uzinduzi wa Kampeni Kinana alisema kwamba mwaka huu kwa kuzingatia afya ya mgombea wao, wamempunguzia kilomita atakazosafiri kwa njia ya barabara ikilinganishwa na alizozunguka mwaka 2005. Swali, je kwanini wamebadilisha huo mwelekeo? Kwanini Mama kikwete anahaha kila kona kuomba kura za JK? Kwanini Ridhiwani anazunguka kila kona kusaka kura za JK? Something is wrong some where na ndio maana REDET na Synovate wamekaa kimya kwa kuwa jahazi linakwenda mrama.

Maswali yako yananifurahisha sana, kutapakaa wabunge nchi nzima haimaanishi kwamba wanakubalika, na ninaomba nikusahihishe kwamba ni wagombea ubunge. Kumbuka hii ni ngwe mpya ndugu yangu na ndio maana kuna wabunge wengi wa CCM ambao walikuwepo miaka 5 inayoisha sasa, lakini wamepoteza nafasi za kutetea ubunge kwenye kura za maoni ndani ya chama chao. Kama mtu alikuwa mbunge kipindi cha 2005 - 2010, haina maana kwamba atachaguliwa tena. Kwa hiyo hoja yako kwamba CCM wabunge wake wametapakaa nchi nzima, is invalid.

Labda nikuongezee angalizo, uchaguzi mkuu wa 2005, kwenye majimbo ya Kiteto, Busanda na Biharamulo, CHADEMA walipata kura chache sana, lakini kwenye chaguzi ndogo ilibidi top brass ya CCM ipige kambi kwenye hayo majimbo na bado CHADEMA ilipata zaidi ya 40%.

Huwezi kulinganisha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, ni vitu viwili tofauti na vinachukuliwa kwa uzito tofauti hata ndani ya CCM yenyewe. Kwa hiyo let us focus on the general election iliyo mbele yetu.

Bottom line ni kwamba kama CCM ingekuwa na uhakika wa ushindi wala wasingebadilisha ratiba ya JK ambaye ni mgonjwa na tayari alishaanguka tangu siku ya kwanza. Pia wasingeishirikisha familia kama wana amini kwamba wagombea ubunge na udiwani waliotapakaa nchi nzima wana mchango kwenye kura za JK.
 
Mhh naamini its vice versa yaani deep green watakula kiivyo but point is ampe kazi Slaa. Ni mtazamo wangu changanya na zako
 
My $100m bet.....Huyu jamaa hamwongelei mlinzi wa CJ?

Umewaza niliyowaza. Kuna taarifa mbili za kifo cha yule dogo. Kafa ghafla na kajiua! Baada ya hapo hakuna taarifa nyingine iliyotoka hata ya mazishi. Poor boy was only 32 years. RIP kamanda!
 
Hiyo ni wastani wa 51.8!!Sample imechukuliwa karibu nusu ya mikoa yote ya TZ,let us keep educating people kuhusu umuhimu wa kuleta serikali mpya huku tukimuombea Dr.Slaa kwa MUNGU ili amlinde!Tanzania bila CCM inawezekana...
 
Umewaza niliyowaza. Kuna taarifa mbili za kifo cha yule dogo. Kafa ghafla na kajiua! Baada ya hapo hakuna taarifa nyingine iliyotoka hata ya mazishi. Poor boy was only 32 years. RIP kamanda!

Halafu something for doubt as well taarifa ya kwa nini kijana yule aliaga dunia, upelelezi wake ulifanyika ndani ya siku 1 maanakesho yake baada ya tukio polisi walitoa taarifa ya upelelezi eti amejiua. Unless kama watu mmeisahau bongo, ni lini wapelelezi wa kibongo wamewahi kutoa taarifa that fast???????????
 

Sept 14, source: Nipashe

Mlinzi wa Jaji Mkuu fariki dunia








Mlinzi wa Jaji Mkuu, Augustine Ramadhani, Mzee Mnyeti (32), amefariki jana akiwa nyumbani kwake Makumbusho, jijini Dar es Salaam.

Mnyeti alikutwa amekufa asubuhi ya jana, baada ya majirani zake kubomoa mlango wa nyumba alimokuwa akiishi. Jaji Mkuu Ramadhani, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho lakini hakutoa maelezo ya kina, badala yake aliagiza kuwasiliana jeshi la polisi.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, alithibitisha kutokea kwa kifo cha Mnyeti.

"Ni kweli mwili wake ulikutwa saa 8:45 ukiwa chumbani mwake, baada ya watu kubomoa mlango," alisema Kalinga.

Kalinga alisema polisi inaendelea na uchunguzi kuhusiana na kifo hicho.
Kwa mujibu wa Kalinga, hadi alipokutwa na mauti, Mnyeti alikuwa hajaoa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia NIPASHE, Mnyeti alikuwa na Jaji Mkuu hadi saa mbili usiku juzi na kwamba afya yake ilikuwa nzuri.
 
................................................

15th September 2010


Source: The Guardian



Police yesterday confirmed that Chief Justice's bodyguard the late Mzee Mnyeti committed suicide, saying investigations have been launched to establish the motive.



Kinondoni Regional Police Commander Elias Kalinga assured the public that police investigations would unearth the cause.

"Similar cases are common these days although it is difficult to tell exactly what drives one to reach such a decision and more so when the deceased did not leave a message behind," said Kalinga.

He said the body of the late Mnyeti was found on Monday morning lying in his apartment at Makumbusho with gun shots on the head, after numerous attempts to locate him for a special assignment proved futile.

His colleagues broke his door to gain access and found him lying in a pool of blood raising suspicion that he must have shot himself through the mouth.

Kalinga said the police would spare no lead in its investigations into the suicidal act of the late Mnyeti who was with the CJ up to 8 pm on Sunday night while in good health.
"We will carry out investigations as directed by law," he said.

On security personnel keeping arms at their homes, Kalinga admitted that certain conditions dictated an officer to be fully armed on 24-hour basis.

In June this year a similar incident occurred in Tarime whereby a policewoman WP7338 Suzan (22), shot herself after she allegedly misdirected President Jakaya Kikwete's motorcade in Mara Region.

Reports said Suzana decided to shoot herself out of frustration shortly after she returned to her working centre at Tarime police station allegedly for directing the motorcade in the wrong direction.
A probe team formed to investigate her death cleared everyone of the blame.

My Take:

Kwa wale tunaongalia zile channel za Crime investigation, you can immediately smell something fishy!!!!!
 
Issue ya REDET na Synovate waulize wenyewe... lakini ukitumia medula oblangata uliojaliwa na Mungu, ulizia uchaguzi wa serikali za mitaa CCM iliibuka na kura kiasi gani? Alafu jiulize ni kitu gani cha ajabu kimetongea tangu wakati huo mpaka sasa? Jiulize kipi CHADEMA imekuja nacho cha ajabu ambacho kitaweza kubadili matokeo kiasi hicho? Jiulize CCM inaowabunge wangapi? Niulize CCM inatarajia kupata wabunge wangapi? Jiulize wabunge na madiwani wa CCM ambao wametapakaa nchi nzima hawana mchango kwa kura za Rais wao.

Sisi waTanzania watu wa ajabu sana tunaamini mazingaombwe mno....
endelea na fikra zako za uchaguzi wa serikali za mitaa halafu usubiri novemba uone tofauti yake
 
Inasikitisha, kafa Mlinzi wa Mwanasheria mkuu, kifo hakieleweki, hata wiki haijaisha kafa Mkemia Mkuu, kifo hakieleweki. Nini kinaendelea? Watu mtasema haihusiani na hoja hii, lakini niwambie taifa linahitaji ukombozi, kama hatutaamua basi tujue vizazi vyetu vitateseka sana
 
Taarifa hizi nilizisikia, sikujua zishaanza kusambaa... Inabidi kuanza kutafuta ukweli wake. Inasemekana Slaa ameanza kukubalika vijijini sana, nini kinasababisha?

Mkuu na wewe unauliza?............I Love JF Wallah!
 
Hiyo ni wastani wa 51.8!!Sample imechukuliwa karibu nusu ya mikoa yote ya TZ,let us keep educating people kuhusu umuhimu wa kuleta serikali mpya huku tukimuombea Dr.Slaa kwa MUNGU ili amlinde!Tanzania bila CCM inawezekana...

Na hili ndilo la msingi.................Ila tuongeze kasi jamani................tukumbuke kuwaambia wale tunaowashawishi kuwa wazitunze shahada zao wasinunuliwe......na kwamba waendelee kwenda kwneye mikutano........lakini siku ya kura PIGA kwa Dr. Slaa
 
...................
Kazi bado mbichi sana jamani. Dr. Slaa na kamati yake ya kampeni wakaze buti tu mpaka tarehe 31.10 na tusilose focus kwa vijitakwimu tusivyojua vimepatikanaje.

Let us be a ''home of great thinkers'' for once
...

Maneno hayo hapo juu ni ya KUZINGATIA SANA................mmeambiwa
 
Ninachokiona hapa ni CCM/Govt Intelejensia VS Peoples power.

Mtaua sana ila Mungu atawapatiliza hapa hapa duniani
 
Nimesikia ni kweli; muda si mrefu itapatikana tuko tunaitafuta tarifa maalum; wamebana ni ya synovate ndio maana wametoa nusu nusu tu

Acha Bwana, inaweza ikawa kweli!?? Mbona Kikwete anataka kuondolewa madarakani kwa sifa ya kurubuni na kudanganya. Mwanademokrasia akishagundua hana lake, huinamisha kichwa na kumwinukia yule anayetakiwa na kumpongeza! Huyu ameachana na ushauri wote aliopewa kuhusiana na kupunguza safari, kwa manufaay afya yake. Sasa akianguka tena au mambo yakawa mazito kweli hasara ni ya nani. Kikwete kwa nini unatka kutupa shida, pumzika, kuugua kwako ni kutuongezea matatizo sisi watanzania, itabidi tugharamia ugonjwa wako, familia yako itasononeka na hata taifa, Please take rest and concede defeat before it is too late! (HIVI SI ANANISOMA HAPO HUYU!).
 
................................................


My Take:

Kwa wale tunaongalia zile channel za Crime investigation, you can immediately smell something fishy!!!!!

Mhhh, hapo kweli kuna madudu mengi ya kufanya libichwa bovu lianze kuzunguka.

Taarifa ya kwanza inasema alikutwa amekufa nyumbani kwake baada ya majirani kuvunja mlango sasa 8.45 (sina hakika kama ana maana ya 8.45 AM au 2.45 PM). Hata hivyo hao majirani zake ni akina nani kama huyo juu alikuwa anaishi kweye Barracks za TISS? Na walikuwa wanatafuta nini au wanamtaka wa nini mtu ambaye ni bachelor?

Taarifa ya pili ndiyo inalikoroga kabisa. Hivi mtu akijipiga risasi (hata kama ni mdomo) mlio wa bunduki hautoki nje? Na hao wenzake walio mkuta amekufa ni akina nani na walikuwa wanatafuta nini?

Ukiwaza zaidi kuhusu hizi repoti 2 unazidi kupata kizunguzungu.....you end up smelling evil!
 
Lisemwalo kumbe lipo, hata Mbowe anajua tayari tafit za hawa jamaa zinasema nini:

"...

Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika Viwanja vya Isanja, wilayani ya Siha, mkoani Kilimanjaro, wakati akimnadi mgombea urais wa Dk. Willibrod Slaa, mgombea ubunge na udiwani.
Alisema tayari chama hicho kina matokeo kamili yaliyofanyiwa kazi na taasisi hiyo hivi karibuni, ambayo yanaonyesha Dk. Slaa, anaongoza kwa asilimia 44, huku mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete akifuatia kwa asilimia 41. Alisema baada ya Synovate kukamilisha matokeo hayo, CCM ilipata taarifa, ikaamua kuwazuia kuyatangaza, kwa madai kuwa yatakidhalilisha chama hicho.....
Source: Tanzania Daima 20 September 2010
 
Mhhh, hapo kweli kuna madudu mengi ya kufanya libichwa bovu lianze kuzunguka.

Taarifa ya kwanza inasema alikutwa amekufa nyumbani kwake baada ya majirani kuvunja mlango sasa 8.45 (sina hakika kama ana maana ya 8.45 AM au 2.45 PM). Hata hivyo hao majirani zake ni akina nani kama huyo juu alikuwa anaishi kweye Barracks za TISS? Na walikuwa wanatafuta nini au wanamtaka wa nini mtu ambaye ni bachelor?

Taarifa ya pili ndiyo inalikoroga kabisa. Hivi mtu akijipiga risasi (hata kama ni mdomo) mlio wa bunduki hautoki nje? Na hao wenzake walio mkuta amekufa ni akina nani na walikuwa wanatafuta nini?

Ukiwaza zaidi kuhusu hizi repoti 2 unazidi kupata kizunguzungu.....you end up smelling evil!
ISHU hizi wamezifanya kimyakimya kwa muda mrefu sana. Sasa wanaua bila huruma na kushadidiza uongo.
NCHI yenye amani na utulivu kama tanzania lazima iweke uthamani wa maisha ya watu wake.

Kuanzia yule mkufunzi wa upolisi kule kilwa, kisha yule binti trafic kule mara na wengineo wengi.

Tuongeze nguvu kwenye kampeni wajameni. lazima tushinde safari hii
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom