GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Acha hizo, kuanguka jukwaani na kuanguka bafuni ni vitu viwili tofauti. Huyu aliyeanguka bafuni aliteleza hata kama alikuwa amekunywa pombe huwezi kulinganisha na kuanguka jukwaani kwenye kampeni nzito kama hiyo. Tuache ushabiki, something is wrong

Hivi Watanzania wanataka dalili gani ZADI kutoka kwa mwenyezi Mungu kuwa huyu bwana hafai. Mungu wetu huyu alitutumia huo ujumbe siku ya mwisho ya kampeni ya JK mwaka 2005, akaanguka Jkwaani siku ya mwisho, kampeni muhimu sana ni siku ya mwanzo na siku ya mwishoi Tukamdharau Mungu tukamchagua JK kwa kishindo. Mungu akasema OK mmeifanya mioyo yenu kuwa migumu, miaka mitano Mungu akatupiga na kipupwe kikali kabisa cha maisha magumu na umaskini, maradhi, ajali, mafuriko ukame, uchumi mbaya, inflation, ufisadi na uonevu etc chini ya utawala wa JK. This time Mungu amesema Watanzania bado nawapenda sana, na kwa kuwa ni wagumu kuelewa mapema ngoja niwapelekee ujumbe mwanzoni kabisa labda wataelewa mbele ya safari. Kama Watanzania hatutaelewa ufunuo huu tena, nadhani miaka mitano ijayo itakuwa kiama, vilio na kusaga meno. Believe me, na si ajabu nchi ikatumbukia kwenye machafuko!!

Hili la kuanguka jukwaani kama ni kweli haliwezi kuwa jambo la kawaida, wale wenye historia ya mambo ya uraisi watakubaliana nami kuwa JK ni raisi labda wa kwanza na pekee aliyeongoza kuanguka kwenye majukwaa ya siasa na kampeni. Hata Joh Mccain au Robert Mugabe ambao kiumri ni wakubwa kuliko JK hawakuwahi kudondoka kwenye majukwaa ya kampeni. Last time alipodondoka Mwanza walisema ni sababu ya uchovu, je leo alikuwa amechoka? si alijua ana kampeni nzito na muhimu? Mbona hakudondoak juzi alivyorudisha fomu? Swaumu sio issue, Waislamu wanabadili ratiba ya kula tu na si kuwa hawali!

SIKU NJEMA HUONEKANA ASUBUHI. MUNGU AMETUPA ZAWADI HII ADIMU YA UFUNUO, MWAKA 2005 ALITUONYESHA MWISHONI, TUKAIFANYA MIOYO YETU MIGUMU, THIS TIME KWA UPENDO WAKE KWA WATANZANIA NA KWA KUWA AMESIKIA MATESO NA VILIO VYA WATU WAKE AMEAMUA KWA NEEMA KUTUONYESHA MWANZONI KABISA KABISA, JE TUTAIFANYA TENA MIOYO YETU MIGUMU KAMA FARAO!!!
WATCH AND PRAY!
 
Mkuu hata Mwinyi ambaye naamini pia alikuwa anafunga sana tu, sina taarifa kama aliwahi kuanguka. Nakumbuka pamoja na kuzabwa kibao na yule dogo, bado alikuwa imara tu na kuendelea na mitikasi kama kawa

Kumbuka kadri miaka inavyosonga mbele kampeni za vyama vingi zinaimarika zaidi tofauti na enzi za serikali ya Mwinyi wakati wa chama kimoja. Katika serikali ya awamu ya tatu ndipo vyama vya upinzani vilizaliwa na kuanza kukukaa,kutambaa na kutembea. sasa siasa inakimbia na KIKWETE lazima akimbie kwenda na wakati. mazingira haya yanachosha. kazi za Rais na kampeni hivi sasa zimeongezeka baada ya wananchi kupewa uhuru wa kusema. Enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa kampeni za mitandao kama ya jamiiforums haikuwepo. Mazingira hayo ukiingia katika Saumu lazima utaangauka. Hivyo sioni ajabu Rais kuwa na uchovu wa kumwangusha.
 
Hii leo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ameanguka mara mbili akihutubia umati wa wana CCM katika kuzindua kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa uchaguzi wa mwaka 2010.

Napenda nieleweke kuwa sina ubaya na kuanguka kwa JK lakini miscalculation ya CCM na JK kwa ujumla. Inaelekea Jangwani wanaidhania ni ile ya Yanga tu.

Inaelekea CCM na watu wake wamesahau kuwa Jangwani ni sehemu iliyobarikiwa na Papa Yahane Paulo II mwaka 1990, na hivyo ni patakatifu zaidi ya hata Ikulu anakokung'ang'ania. Wachawi wengi huanguka pale bila kujua kuwa wanakatiza eneo ambalo si la kuchezea na linalostahili heshima zote. JK kaanguka wakati akiongea maneno ambayo kwangu naweza kukiri ni uwongo, hakuyamalizia na Mungu akaamua kumnyamazisha kwa muda.

Mimi si CHADEMA na wala si CUF, siegemei upande wowote lakini iwe ni angalizo kwa wanasiasa wengine mnaotarajia kupatumia kwa uzinduzi wa kampeni zenu; msiende pale kuwaongopea watanzania yatawakuta makubwa!

Pole JK, lakini usirudie kusema uwongo kwani wanaokushangilia asilimia kubwa ni sababu ya njaa zao tu!
 
CCM kutumia helikopta ktk kampeni ni just a mere coincidence na mkulu kuanguka jukwaani?


Kinana anakwambia (3:45) "siku ambazo tunatakiwa kufanya kampeni ni kuanzia tarehe 22 Oktoba mpaka, 22 kesho mpaka Oktoba, ukisema unaweza kupiga kila mahali si kweli ...."

Hivi hapa kasema nini hasa? Hiyo 22 kesho ni 22 ya mwezi gani? Hiyo "mpaka Oktoba" ni mwanzo wa Oktoba au mwisho wa Oktoba? Au tarehe gani ya Oktoba?

Kura watu wanapiga Oktoba 31, nayo ni Oktoba, mwenyekiti wa kampeni ya CCM anawaambia watu wapige kura mpaka Oktoba bila kufafanua tarehe, maana yake hata siku ya kupiga kura Oktoba 31 kupiga kampeni ruksa kwa mujibu wa Kinana !

Yaani communication skills zero, huyu mtu kaenda kusoma mpaka Harvard, halafu tunawasakama walioishia darasa la saba wakati hata wasomi wetu bado wako shaghalabaghala kama hawajasoma.

Hatujali clarity, hatujali preciseness, sasa kama katika kuongea tu ni hivi vipi katika kupanga mipango ya kiuchumi? Wanasoma small print kweli hawa ?
 
Last edited by a moderator:
Ajabu ni nini? nani hajawahi kuanguka? hata hivyo hakufika chini! Mambo mengi yanaweza kuwa yamechangia... swaumu, nk
Mimi naona ni bahati mbaya tu.
Ni kweli wengi tumewahi kuanguka lakini hatujawahi kuonekana mbele ya Watanzania wengi kama na wala anguko letu haliathiri taifa.
 
Dr Kikwete bado ndie raisi wa nchi ya Tanzania mpaka sasa hadi atakapokabidhi kwa raisi mpya kama hatafanikiwa kutetea kwa ufanisi nafasi yake katika uchaguzi huu. Sisi raia wote, kwa sasa tuzidi kumwombea afya njema na nguvu za kuendelea na shughuli zake raisi wetu. Najuwa kuwa, sisi kama raia tuna itikadi mbalimbli tofauti tulizo nazo, na inawezekana kabisa mtu akawa hampendi Kikwete kiitikadi au kwa sababu 1, 2, 3 ... lakini mimi nafahamu kuwa wa-Kristo wote wanafundishwa katika msahafu wao kuwa adui yako mwombee mambo mema (shibe na afya) na wala usimwombee mabaya yamtokee. Kwa msingi huo washabiki wa itikadi za Dr Slaa na Prof Lipumba nawaomba tumwombee afya tele Dr Kikwete ambae bado ni raisi wa nchi yetu kwa sasa.

Ushindani katika mbio za kuingia ikulu hapana budi unahitaji washindani wenye afya njema ili waweze kuuza sera zao na hatimae sisi wapiga kura tuweze kuchagua kiongozi bora kuongoza taifa letu. Baba yetu wa taifa (RIP) alisema ukishindana na mgonjwa ukamshinda haileti heshima ya ushindani huo. Hivyo tuwaombee wagombea wote Dr Kikwete, Dr Slaa na Prof Ibrahim afya njema kabisa katika campaigns zao hadi mwisho.

Sisi wana JF tuoneshe ukomavu wetu utokanao na elimu, dini zetu, umri wetu na hata exposures kila mtu aliyo nayo kutoa hoja zenye nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu katika mtandao wetu huu. Kama tunataka kusaidia kuwauza wagombea wetu ktk forum ya JF tunaweza kufanya hivyo kwa kutumia lugha nzuri na hoja nzuri badala ya matukano na hoja za jazba ambazo mwisho wa siku zitakuwa zinawaharibia wagombea wetu tunaowashabikia.

Hata hivyo kuhusu afya ya Dr Kikwete kuna maswali mazito. Na mimi sijuwi kama ni busara kutangaza ukweli wa afya ya raisi au kuficha. Sijuwi ni kipi kinalipa katika hayo mambo mawili. Lakini wote tunafahamu ukweli mmoja kuwa.. mfichaficha ugonjwa… matokeo yatamwumbua! Hatuombi mambo mabaya juu ya Mh raisi yatokee, lakini badala yake viongozi wa CCM watumie hekima njema kukabiliana na hali hiyo.

Nafasi yetu kama raia ni kungoja maelezo yao na hatimae kupiga kura ya kumchagua tunayemtaka kuongoza taifa letu. Tusigombane, sisi wote ni wamoja (ndugu) ktk taifa letu. Hivi ndio nionavyo mimi…
Sungura
 
nyumba zetu nyingi zina Tiles mbona hatudondoki kama Dr Slaa. Mgombea Urais atalalaje Guest house????????? maaana ya Guest house unaijua????????? Mwanza kuna Hotel kabao za hadhi ya Rais mtarajiwa
Hoteli wanalala wakubwa wenye nazo. Slaa ni kada yetu, analala guest house, period. Kwani wanaolala guest house si binadamu, au kwa vile unadhani guest house ni sehemu ya kufanyia uzinzi tu? Slaa alikuwa anatafuta wadhamini, hiyo hadhi ya urais aliitoa wapi, sasa hivi ni mgombea, labda anaanza kufikia hiyo hadhi. Lazima kufanya vitu kwa wakati!! ala
 
Nilikuwa naangalia star tv,wakati tukio linatokea,kama binadam nilishtuka sana,rais alianguka lakini alidakwa na mpambe wake kabla hajafika chini.Nilichokinotice tafauti ya 2005 na leo,viongozi wengi(kama sio wote)waliokuwa wamekaa jukwaa kuu hawakuonekana kupanic kama 2005,inaonekana wameshamjua na wameshalizoea hilo tatizo,kilichowatatiza ni jinsi ya kudili na wananchi ambao walionekana wamepigwa na butwaa.Cha msingi kwa sasa ni Mheshimiwa rais kuachana na pilikapilika za kisiasa na kupumzika na familia yake,sababu nilichokiona kwenye nyuso za viongozi kana Dk.Sheini,Mkapa,Makamba ni aibu.

Hassan wa Chadema utamtakia mazuri JK wapi na wapi? kila siku mnaomba na kuota ndoto lolote baya limfike Jakaya Kikwete ili muweze kupata nafasi ya kuongoza nchi. Wasiojua siasa utawajua tu. Tukio hili limewafurahisha sana Chadema na ndio mmejaa humu kuonyesha kwamba hamfai kuongoza nchi. Wafuasi wa chama makini hawawezi kudhihaki afya ya wananchi wenzao. Kazi kwenu watanzania kuchambua pumba na mchele. kwa mtaji huu ni heri CCM wakaendelea kuongoza.
 
Swaumu? Hakuna lolote anatafuta public huruma ya wananchi! Ah siasa kazi kwelikweli!

Whaaat? Rais Na ukamilifu wake ajiangushe kwa ajili ya kuhurumiwa na jamiii???? Haingii akilini kabisa...So cheap trick!!! Hili nakataa haliwezekani!!!!
 
kweli kazi imeanza, hawajampeleka msata kama mwaka ulee?
 
heheh mie nakubaliana na maria roza,
rais arest tu in peace,
mbona wamama kibao wamepoteza maisha wakati wa kujifungua mahospitalini kutokana na huduma mbovu,
afu yeye akiwachekea mafisadi,
na yeye arest in peace huko!:mad2:a

ila hii mada imenichekesha sana
nimesoma na kutokana na michango ya watu hapa.
i belive wengi hapa mnaamini raisi wetu MHESHIMIWA JAKAYA KIKWETE ni MSHIRIKINA...which i found very funny!:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky:
 
Kuna habari au tetesi. Nani kaanguka Jangwani?

Sio tetesi ni kwa uhakika kabsaaaaaaaaaaa. Nimeona TBC live man! Mwanzo mbaya sana. Hata hizi kampeni naona zitakuwa shida sana kwake pamoja na Chama kumwandalia helkopta bado shida iko!
 
Mnaosema Kikwete anaumwa mnadanganyika kweli. Mbona haunguki akiwa safari anatoa hotuba nje ya nchi? Hiyo political strategy kupata huruma ya wapiga kura. JK hana shida wala haumwi. Ni kama MP alivyolia bungeni to drive a point home. Mbona akitoka hapo hatuoni amelazwa kwa hata siku moja? Nyie hamjui siasa kweli.
 
Hahaha hahaha mkuu u made my day, maraisi wetu ni kunenepa matumbo tu! Lakini hii kwa kweli ni kali and strange...................... Hata wakispin vipi bado voters watakonkludi jamaa nni mgonjwa tuj which is a fact.

Daima fisi (Chadema) anasubiri mfupa kudondoka. Mwaka 2005 alipoanguka KIKWETE hapo hapo Jangwani waliomtakia mabaya walijua ndio mwisho wake lakini akapata ushindi wa kishindo zaidi ya asilimia 80. Mwaka huu 2010 pia ni wa CCM. Kwa watanzania makani suala la kuanguka ni dogo. Mbona Clinton alipatikana na hatia ya kufanya mapenzi katika Ikulu ya Wamarekani na akaendelea kuongoza sembuse kuanguka???? haaaaa.
 
Rais ana majukumu mengi huwezi kumfananisha na mfunga saumu yoyote mahali popote. Ni sawa na kuuliza mbona binadamu wote tunaumwa na mbu lakini hatugui kwa pamoja.Unaweza kuumwa na mbu kumi na mwingine akaumwa na mbu wawili tu lakini wa mbu kumi asiugue malaria yule wa wawili akaugua.

Hivi dunia nzima rais anayefunga swaumu ni Kikwete Peke yake?? wafungaji swaumu wako kibao kuanzia waalimu wanaofundisha Hisabati mpaka Makuli wa Kariakoo, mbona hawaanguki hovyohovyo??
 
Daima fisi (Chadema) anasubiri mfupa kudondoka. Mwaka 2005 alipoanguka KIKWETE hapo hapo Jangwani waliomtakia mabaya walijua ndio mwisho wake lakini akapata ushindi wa kishindo zaidi ya asilimia 80. Mwaka huu 2010 pia ni wa CCM. Kwa watanzania makani suala la kuanguka ni dogo. Mbona Clinton alipatikana na hatia ya kufanya mapenzi katika Ikulu ya Wamarekani na akaendelea kuongoza sembuse kuanguka???? haaaaa.

sijui huwa mnalipwa shilling ngapi,kuneutralize mambo hapa...?
JF kuanguka ni dhahiri,ana matunguri :becky::becky::becky::becky::becky: aibu!
usijihangaishe mie sio chadema wala ccm..:becky:😛layball:😛layball:
 
Daima fisi (Chadema) anasubiri mfupa kudondoka. Mwaka 2005 alipoanguka KIKWETE hapo hapo Jangwani waliomtakia mabaya walijua ndio mwisho wake lakini akapata ushindi wa kishindo zaidi ya asilimia 80. Mwaka huu 2010 pia ni wa CCM. Kwa watanzania makani suala la kuanguka ni dogo. Mbona Clinton alipatikana na hatia ya kufanya mapenzi katika Ikulu ya Wamarekani na akaendelea kuongoza sembuse kuanguka???? haaaaa. Mbona Dr Slaa alifumaniwa na mke wake kule Dodoma akiwa na binti Guest bado anagombea Urais.

lakini ukumbuke alipodondoka ndo alikuwa anahitimisha kujinadi kwa wananchi,,, hii ya leo ndo alikuwa anafungua kujinadi kwa chama chake,,na ukumbuke alipodondoka mara ya kwanza walisingizia alikuwa amefunga, na hii ya leo watasema hivyo, kama raia mlipa kodi ambayo ndo anatumi kwanini hawasemi ukweli,,, Naamini jamaa anamatatizo ya kiafya huwezi ukasimama dakina 8 kuongea tu then ukadondoka hilo haliwezekani,,,,,swala la Slaa kufumaniwa huwezi li compare na kudondoka kwa kikwete hata kidogo,

Kwa macho ya kawaida ukimwangalia mgmbea Mwenza na yeye afya mgogoro tuweelewe vipi???
 
Hivi kweli Mkwere angemudu mdahalo na Slaa na Lipumba kama hali yenyewe ndio hii?
 
Back
Top Bottom