GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Amedhooofu ... kama CCM yake vile. Hakuna cha swaumu wala nini
 
Tabia ya kutojua wapi kuwe na siasa wapi kuwe na ushauri wa kitaalamu kutamponza Jk. Jk anasahau kuwa mgomeba wa uraisi ni kubeba mizigo ya chama.

Waliombebesha wengi wanataka aendelee kuibeba kwa faida yake na zaidi wao. Kama afya hairuhusu kwa nini asiwe mkweli akajipanga kulingana na uwezo wake kwa sasa?

Nasubiri hotuba ya daktari wa raisi itakayotolewa. Tukicheza mpaka uchaguzi ufike tutapokea hotuba kibao za daktari wa rais
 
Kuna wazee UWT waliapa toka 2005 kuwa JK hamalizi vipindi viwili.:confused2:
Kwani UWT ndiyo mwaumbaji hizi ni porojo za mitaani. Maneno hayo kisheria ni uhaini unaweza kushitakiwa kwa kupanga kufupisha maisha ya Rais.
 
Ni vyema wakatuambia anaumwa nini -- kabla hajaendelea na kampeni. Wengi hawatahudhuria kampeni zake kuhofia usumbufu na kupoteza muda -- yaani baada ya dak chache tu jamaa chini!!! Wengine husafiri kutoka mbali sana!
 
Pole JK. Mungu akutie nguvu ili uendelee na campaign. Tunataka tuone mpambano wenu na Dr Slaa hata mwisho. Na mwisho utanoga zaidi hapo Slaa atakapokubwaga kwa asilimia nyingi zaidi yako.
 
Huyu jamaa kweli anatufaaa?? Sijui...apunguze kuchanganya mambo,,,,Pole ndugu yangu
 
Hivi ma bodygurd na wasaidizi wake wanakuwepo karibu kweli au ndo hivyo hawajui majukumu yao. Pamoja na matatizo aliyonayo, hawa wasaidizi wake wanapaswa wawajibishwe kwa kumwacha aanguke bila kumzuia.
 
Be blessed JK, you will regain your strength in the NAME of JESUS CHRIST.
 
...mmm, My dear Roza. Jamaa anatuudhi lakini hii kidogo naona kama imepinda hivi ama we waonaje?

yamkini ndani ya jamiiforums kuna washirikina wasio na utu kama Roza kusema Rest in peace (RIP) kwa Rais kabla hajafa hiyo ni dhambi huna dini?
 
Kuanguka sio yeye tu kumbuka Dr Slaa aliaguka majuzi bafuni Mwanza na kuvunjika mkono,ile ni ajali kama ajali nyingine
usichanganye mchanga na sukari! Slaa ameteleza yaani mabafu ya ma-guset na mahoteli yetu tiles hazina viwango! JK kadondoka kwa afya mbovu! tuseme ukweli
 
..maelezo yatakuwa Raisi alikuwa amezidiwa na swaumu.

..nadhani hii ni calculated move kutafuta kura za huruma za Waislamu.

..nashauri Slaa,Lipumba,..na wagombea wote wa Uraisi wajibwage kwenye majukwaa na kusingizia swaumu.
 
Naomba mambumbumbu wa amani muache kuchochea chuki na hulka ya dharau katika nchi hii iliyojengwa kwa misingi ya heshima na upendo. Ndio maana Dr. Slaa alipodondoka na kuteguka mkono hakuna aliyesema RIP. Badala yake watu wote tulimuombea apone haraka aendelee na kazi za ujenzi wa Taifa. Muwe wastaarabu.
Tofautisha kuanguka kwa Slaa na Kikwete, huwezi kusema kuanguka kwa Kikwete ni bahati mbaya mara ngapi anashauriwa apumuzike hataki, tatizo la JK ni ugonjwa ambao unafichwa tofauti na kuanguka kwa Slaa huwezi kusema kuteleza kwa Slaa kulisababishwa na ugonjwa.

Afterall huwezi kutegemea kila siku Slaa ateleze bafuni na kuvunjika mkono lakini hii ya JK ya kuanguka unaweza ukapredict kutokana na record ya afya yake.
 
hakuanguka jumla mabodyguard wake walimuwahi kabla hajafika chini. Mbona hata Dr Slaa alianguka bafuni huko mwanza hadi kuvunjika mkono. wote wameanguka tofauti mmoja kaanguka bafuni mwingine jukwaani. hii ni bahati mbaya inaweza ikamtokea mtu yoyoye wakati wowote.

Bahati mbaya mara ya tatu? i cant buy it!! hii haijawahi kutokea ata mara moja kwa maraisi watatu waliopita!!
 
good question....

na bila shaka katika group ya waliokuwa jangwani kuna wengi tu wana saumu why yeye tu????

kuhusu ikiwa wanafunga kinafiki au wanakula kwa siri sidhani...bali nadhani kuna unafiki kwa kikwete kusingizia saumu kila anapoanguka..

saumu saumu......good scapegoat eehh!!!!!


Rais ana majukumu mengi huwezi kumfananisha na mfunga saumu yoyote mahali popote.

Ni sawa na kuuliza mbona binadamu wote tunaumwa na mbu lakini hatugui kwa pamoja.Unaweza kuumwa na mbu kumi na mwingine akaumwa na mbu wawili tu lakini wa mbu kumi asiugue malaria yule wa wawili akaugua.
 
Kuyumba si kuanguka. atakuwa kamili tu baada ya muda mfupi. wadau haifai kuandika hovyo

Welcome, leo JF itapata wageni wengi sana, Invisible vipi sever yetu iko imara.

Luiza Gama

Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

Join Date Sat Aug 2010
Posts 1
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power 0
 
Back
Top Bottom