GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Come to think of it, sasa naona ni vyema ametolea nje mdahalo maana kama mambo yenyewe ndio haya sidhani kama angeweza kuhimili mashuti ya Slaa na Lipumba.....
 
Kama ameanguka basi ujuwe wizi wa kura upo hakuna kutofautisha na uchaguzi uliopita ,ila mwaka huu wataanguka wengi tu !!
 
nyumba zetu nyingi zina Tiles mbona hatudondoki kama Dr Slaa. Mgombea Urais atalalaje Guest house????????? maaana ya Guest house unaijua????????? Mwanza kuna Hotel kabao za hadhi ya Rais mtarajiwa

unalinganisha CHADEMA na CCM ambao bajeti yao ya ushindi tu tuliyopewa tuifungie mkanda ni bilioni 50????.sintashangaa kusikia mgombea wa upinzani analala guest au anakula gengeni ..serikali lazima iwape huduma nzuri maana wakipata madhara tutafanya uchaguzi wa marudio....mwaka 2005 walitumia karibu bilioni 150!!
 
Kuna tetesi kuwa hiyo ni mbinu mkakati ambao wamefanikiwa kuprove kulingana na masharti ya sangoma. Wakati mnachonga huku ile cc ya ccm inashangilia ushindi wa uchaguzi. Ila kipindi hiki wamenoa
 
Nilikuwa naangalia star tv,wakati tukio linatokea,kama binadam nilishtuka sana,rais alianguka lakini alidakwa na mpambe wake kabla hajafika chini.Nilichokinotice tafauti ya 2005 na leo,viongozi wengi(kama sio wote)waliokuwa wamekaa jukwaa kuu hawakuonekana kupanic kama 2005,inaonekana wameshamjua na wameshalizoea hilo tatizo,kilichowatatiza ni jinsi ya kudili na wananchi ambao walionekana wamepigwa na butwaa.Cha msingi kwa sasa ni Mheshimiwa rais kuachana na pilikapilika za kisiasa na kupumzika na familia yake,sababu nilichokiona kwenye nyuso za viongozi kana Dk.Sheini,Mkapa,Makamba ni aibu.
 
Halafu mbona maraisi wetu hawazeeki haraka wakiwa madarakani? Obama sasa hivi ukimwona keshaanza kuwa kibabu. Lakini hawa wa kwetu ndio kwanza wanazidi kuwiva. Hawafanyi kazi hawa....

Hahaha hahaha mkuu u made my day, maraisi wetu ni kunenepa matumbo tu! Lakini hii kwa kweli ni kali and strange...................... Hata wakispin vipi bado voters watakonkludi jamaa nni mgonjwa tuj which is a fact.
 
Tofautisha kuanguka kwa Slaa na Kikwete, huwezi kusema kuanguka kwa Kikwete ni bahati mbaya mara ngapi anashauriwa apumuzike hataki, tatizo la JK ni ugonjwa ambao unafichwa tofauti na kuanguka kwa Slaa huwezi kusema kuteleza kwa Slaa kulisababishwa na ugonjwa.

Afterall huwezi kutegemea kila siku Slaa ateleze bafuni na kuvunjika mkono lakini hii ya JK ya kuanguka unaweza ukapredict kutokana na record ya afya yake.
.

mbona jibu unalo kwamba ana uchungu na nchi yake ameshauriwa apumzike hataki ili kuwatumikia watanzania basi ndiye Rais bora. Kwa sisi tulio mtaani tunathibitisha kwamba KIKWETE anafanya sana kazi kwa kuangalia shughuli zake kwenye vyombo vya habari mbali na kazi ambazo haziko kwenye vyombo vya habari. Kwa hakika huwezi kujui kikwete analala na kupumzika saa ngapi.

Kuna mzee wa chama nimempigia simu kuuliza vipi Rais ameishiwa nguvu tena? kasema usiku wa kuamkia leo Rais kalala masaa mawili tu akiwa na timu ya wataalamu kupitia ratiba ya kampeni na kuifanyia marekebisho kadhaa.
 
Hahaha hahaha mkuu u made my day, maraisi wetu ni kunenepa matumbo tu! Lakini hii kwa kweli ni kali and strange...................... Hata wakispin vipi bado voters watakonkludi jamaa nni mgonjwa tuj which is a fact.

Ipo siku huyu jamaa ataanguka akiwa kwenye zile roundtable/ panel discussions za Davos......nyi subirini tu

Au kufia (perish the thought) jukwaani kabisa....
 
huyu atakuwa ni kiumbe chenye roho mbili (made by shekhe yahya), moja ya kampeni na nyingine ya kuongozea,
huenda inapotoka ile ya kuongoza inaingia ya kufanyia kampeni,
hivyo pengine humzidi nguvu na kumwangusha pale tendo la roho hizo zinapobadirishana kazi,
 
Presure up, presure down. Kazi anayo!

Asisingizie swaum, kwani ye hajakandamiza daku? Ndio zake huyo kwani Mza nako ilikuwa swaum?

Aachwe apumzike kama alivyomuacha Mzee Mkapa! Kama ni mgonjwa aache wazima wa afya na akili akina Dr Slaa wachukue nchi!
 
Mh. JK rudi kajipange upya vinginevo...............
 
Ebana eeh naona kuna surge ya wanachama wapya mwezi huu....

....aa mbona JF wanaisoma sana ...siummsikia Jk akichonga kuhusu mtandao[JF]....Akasema ..mtandaoni wanachonga sana lakini watanzania hawadanganyiki.....nadhani anajuwa kuwa watanzania wengi hawasomi...!!
 
Aisee, mimi nashauri wakati wa kuchangia-tuchangie kwa kutumia busara zaidi.Acheni matusi kwa viongozi, tunachotakiwa kufanya hapa ni kurekebisha. Mimi namuombea apone haraka aendelee na kampeni zake kama kawaida.

Humu watu wanachangia kwa ushabiki. Ugonjwa ni jamabo la kawaida na inaweza kutokea muda wowote ule,hivyo isionekane kudondoka au kuishiwa nguvu kwa president ni jamabo la ajabu saana as if hamana watu amabao huwa wanadondoka.

Changieni kwa kujenga zaidi. Angekuwa ni baba yako mzazi amedondoka ungechangiaje? Habari ya kuambiwa ugonjwa haituhusu-maana hata ukiambiwa utatoa msaada gani? Huu ni umbea wa kutaka kujua internal matters za watu.
 
Oh yeah...na wala sitashangaa kama na yeye ni mwanachama humu na hupenda kuchangia hasa kwenye lile jukwaa la wakubwa....
 
tatizo ni mgumu kusoma alama za nyakati......ni kama vile haoni maandishi ukutani...hii ni ishara kwamba CCM inaanza kuanguka...
 
Ipo siku huyu jamaa ataanguka akiwa kwenye zile roundtable/ panel discussions za Davos......nyi subirini tu

Au kufia (perish the thought) jukwaani kabisa....

hata mwanawasa aliangukia kwenye mkutano wa AU akafa wakazuga hajafa wajipange wakaenda kumficha FRANCE...lakini angalau mwanawasa alikuwa ameweka wazi afya yake kwa wazambia...
 
nilikuwa naangalia star tv,wakati tukio linatokea,kama binadam nilishtuka sana,rais alianguka lakini alidakwa na mpambe wake kabla hajafika chini.nilichokinotice tafauti ya 2005 na leo,viongozi wengi(kama sio wote)waliokuwa wamekaa jukwaa kuu hawakuonekana kupanic kama 2005,inaonekana wameshamjua na wameshalizoea hilo tatizo,kilichowatatiza ni jinsi ya kudili na wananchi ambao walionekana wamepigwa na butwaa.cha msingi kwa sasa ni mheshimiwa rais kuachana na pilikapilika za kisiasa na kupumzika na familia yake,sababu nilichokiona kwenye nyuso za viongozi kana dk.sheini,mkapa,makamba ni aibu.
mbona kuna mtu kaandika alilamba mchanga? Na wasaidizi hawakufanya kitu?.......tuelezeeni katika hali ya uwazi na ukweli.........!
 
Humu watu wanachangia kwa ushabiki. Ugonjwa ni jamabo la kawaida na inaweza kutokea muda wowote ule,hivyo isionekane kudondoka au kuishiwa nguvu kwa president ni jamabo la ajabu saana as if hamana watu amabao huwa wanadondoka.

Sawa, ugonjwa ni kitu cha kawaida na humkuta mtu yoyote bila kujalisha. Lakini huyu bwana sasa ni mara kadhaa sasa anaanguka hadharani. Je faraghani keshaanguka au kuzimia mara ngapi?

Watu tuna kila sababu ya kuhoji hali yake ya afya. Uraisi si picnic bana. Tena kwa nchi zetu hizi za ulimwengu wa tatu uraisi si kazi ndogo (ingawa wao naona kama vile wanatanua zaidi ya kufanya kazi). Tunataka raisi mwenye akili timamu na afya nzuri ili aweze kufanya kazi kwa bidii na kutusaidia kutondoa katika bahari ya ufukara.
 
Aisee, mimi nashauri wakati wa kuchangia-tuchangie kwa kutumia busara zaidi.Acheni matusi kwa viongozi, tunachotakiwa kufanya hapa ni kurekebisha. Mimi namuombea apone haraka aendelee na kampeni zake kama kawaida.

Humu watu wanachangia kwa ushabiki. Ugonjwa ni jamabo la kawaida na inaweza kutokea muda wowote ule,hivyo isionekane kudondoka au kuishiwa nguvu kwa president ni jamabo la ajabu saana as if hamana watu amabao huwa wanadondoka.

Changieni kwa kujenga zaidi. Angekuwa ni baba yako mzazi amedondoka ungechangiaje? Habari ya kuambiwa ugonjwa haituhusu-maana hata ukiambiwa utatoa msaada gani? Huu ni umbea wa kutaka kujua internal matters za watu.

bora iingekuwa ugonjwa tukajuwa dawa..lakini hapa ni ndumba zimegongana na anazidiwa anaanguka ...sasa tusemeje///?
 
Oh yeah...na wala sitashangaa kama na yeye ni mwanachama humu na hupenda kuchangia hasa kwenye lile jukwaa la wakubwa....
He, jukwa la wakubwa ndiyo living room yake? Nitaanza na mimi kuvinjari huko.
 
Back
Top Bottom