GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Kazi ipo!! huo ni woga andthis time lazima tumtoe. dont Joke
 
Pole JK; ila hii ni dalili mbaya sana; huenda inabidi tutafakari kama kweli watanzania wote tu salama na kama kuna wagonjwa wakatibiwe kwanza wakati huo wazima wakiendelea na kazi; na hili ni jambo la kawaida
 
Rais ana majukumu mengi huwezi kumfananisha na mfunga saumu yoyote mahali popote. Ni sawa na kuuliza mbona binadamu wote tunaumwa na mbu lakini hatugui kwa pamoja.Unaweza kuumwa na mbu kumi na mwingine akaumwa na mbu wawili tu lakini wa mbu kumi asiugue malaria yule wa wawili akaugua.

Au Nyerere, Mwinyi na Mkapa walikuwa wavivu katika utendaji wa majukumu yao?kwanini ni Kikwete tu ndiye anayezidiwa na uchovu na kuanguka mbele ya kadamnasi?

Ok..Ata Umaru YarAdua walikuwa wanasema ni mzima wa afya njema mpaka ilipofika point of no return.
 
mkuu hakuna mwenye kumtakia shari.......

swali ni kwanini ukweli hausemwi????????????!!!!!!!!!!

Ukweli upi? kama unaujua sema nasi tujue kwa vile hukubaliani na sababu zilizotolewa na viongozi wa CCM pale jangwani!!!!!!!!
 
Ajabu ni nini? nani hajawahi kuanguka? hata hivyo hakufika chini! Mambo mengi yanaweza kuwa yamechangia... swaumu, nk
Mimi naona ni bahati mbaya tu.
 
Tabia ya kutojua wapi kuwe na siasa wapi kuwe na ushauri wa kitaalamu kutamponza Jk. Jk anasahau kuwa mgomeba wa uraisi ni kubeba mizigo ya chama. Waliombebesha wengi wanataka aendelee kuibeba kwa faida yake na zaidi wao. Kama afya hairuhusu kwa nini asiwe mkweli akajipanga kulingana na uwezo wake kwa sasa? Nasubiri hotuba ya daktari wa raisi itakayotolewa. Tukicheza mpaka uchaguzi ufike tutapokea hotuba kibao za daktari wa rais

saluti mkuu...imeeleweka
 
Mkapa na u-obese wake wote ule sikuwahi kusikia kaangauka hata mara moja...labda awe alikuwa anaangukia ndani na habari hazitoki
 
yamkini ndani ya jamiiforums kuna washirikina wasio na utu kama Roza kusema Rest in peace (RIP) kwa Rais kabla hajafa hiyo ni dhambi huna dini?
Wewe unajua maana ya rest in peace si lazima kuambiwa mtu aliyekufa usichukulie mazoea yakawa ndiyo kweli.
 
Infact ni mara ya nne toka aanze rasmi mbio za urais. awali ilikuwa ni ile ya 2005, then zimewahi kutokea mbili hapa katika katika.

Ni vema sasa tuambie Rais wetu anaumwa nini? Ansbert Ngurumo aliwahi kuandika:

Rais wetu si dhaifu kama wananchi wake ambao wengi wanalalala au kushinda njaa; wanapata mlo mara moja moja (na wenyewe haujakamilika virutubisho); wanafanya kazi nzito na ngumu zinazokula nguvu ya mwili na akili; wana pato duni sana (chini ya shilingi 1000 kwa siku); wanakabiliwa na magonjwa hatari na hawana huduma ya matibabu inayoeleweka na inayoaminika; wanaishi katika mazingira hatari; wanakabiliwa na magonjwa sugu kwa miaka mingi; wanatembea kwa miguu au baiskeli, bajaji au wanasafiri kwa malori na mabasi mabovu; hata kwa wanaosafiri kwa ndege, wanatumia madaraja ya chini yanayochosha; wanalala kwa saa 2 au tatu kila siku; wanasumbuliwa na umaskini wa kutisha kiasi kwamba kila wanapolala hawana tumaini kama wataiona kesho.

Watanzania hawa hawazimii, hawaishiwi nguvu wala hawaanguki, aanguke rais mwenye afya isiyotetereka (kama tulivyoelezwa) na mwenye matunzo ya viwango vya juu?.."


Sasa iweje huyu? Kijua ndio hichi ni vyema Rais akate shauri sasa. kwani kwa hali yoyote, lazima mgombea binafsi ndo aongoze kampeni kwa nguvu zaidi..... na pengine wabunge waliopita bila kupingwa. ile confidence ya kusimama na kuikimbiza kura kwa hali ha hila lazima ipungue...

Ni faida kwa wengine walio katika mbio? historia itatuambia....
 
Kuanguka sio yeye tu kumbuka Dr Slaa aliaguka majuzi bafuni Mwanza na kuvunjika mkono,ile ni ajali kama ajali nyingine

huwezi kufananisha ...sillaaa kuanguka bafuni ...na jk anayeanguka anguka ovyo.....tena mara nyingi tu akiwa na wasaidizi wake na mara nne hadharani...kwa alivyoanguka bafuni silaa ingekuwa jk ..asingetangaza ........angesema lolote....
 
Pole Jk, sijui unatatizo gani jamani, mbona kila mara jangwani kwenye uzinduzi waanguka.

Siyo kila mara Jangwani kwenye uzinduzi.
Mara ya kwanza(2005) alikuwa anafunga kampeni alipoanguka ikabidi Che Nkapa aje atulize umati, yeye Kikwete alikimbizwa sehemu-sehemu.
mara ya pili leo anafungua kampeni, Makamba et al wameshindwa kabisa kuubeba umati na kuutoa katika simanzi.
Hata aliporudi Kikwete mwenyewe na namna aliyokatisha houtuba, maswaali yanazidi kuongezeka.
 
na nadhani kisingizio kisiwe SWAUMU, we won't buy that.... naamini swaumu ya Rais ni tofauti na SWAUMU za siye wengine kwa kuwa DAKU laku ni zito kidogo..... and now I can seriously see the danger of having unpopular running mate...... God bless lakini tuendako ni giza...... Mungu atusaidie
 
Wamtumainiao BWANA ni kama Mlima wa Sayuni, hawatatikisika milelee.....JK mtegeemee na Kumtumainia MUNGU sio mwanadamu...kama vile ambavyo hutegemei kura za wafanyakazi basi vivyo hivyo, usiwategeemee wanadamu pia. MUNGU wang akutie nguvu mtumishi
 
Tujadili kwa unyenyekevu kwani huyu ni rais wetu kwa sasa

Inategemea unasoma kwa staili gani. staili unayotumia inaweza kukupa maana tofauti.

Pili, naye kacheza faulo. Kwasasa nchi inapaswa kuwa chini ya Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Twaweza tukaujadili hata uraisi wake.
 
Back
Top Bottom