GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Mkapa na u-obese wake wote ule sikuwahi kusikia kaangauka hata mara moja...labda awe alikuwa anaangukia ndani na habari hazitoki

Mkuu hata Mwinyi ambaye naamini pia alikuwa anafunga sana tu, sina taarifa kama aliwahi kuanguka. Nakumbuka pamoja na kuzabwa kibao na yule dogo, bado alikuwa imara tu na kuendelea na mitikasi kama kawa
 
Slaa alipolazwa Muhimbili kwa ajili ya kutolewa POP magazeti yalitangaza yuko ICU, sasa kesho magazeti yakitangaza JK amelazwa ICU sijui itakuwaje.

Halafu give me a break kesho anatakiwa awe Mwanza itakuwaje wandugu daktari wake atamruhusu aende, basi akianguka tena tusiambiwe ni ajari.
 
Ni kweli ameanguka -- hii ni mara ya 3 sasa anadondoka kwenye majukwaa in 5 years. Tatizo kubwa ni kwamba wananchi hatuambiwi kinagaubaga anaumwa kitu gani. Leo tumeambiwa ni kwa sababu ya swaumu ya Ramadhani -- yaani anashindwa kumudu swaumu?

Mwaka 2005 hapo hapo Jangwani alidondoka na baadaye tukaambiwa ni kutokana na kufunga (haikuwa mwezi wa Ramadhani). Kuna uvumi kwamba ana kisukari cha kushuka. Kama ni hivyo kwani kisukari ni ugonjwa wa siri? Si waseme tu, wanaficha nini?

Kikwete ana ugonjwa wa nervous system jamani tuambizane ukweli, kashaanguka mara 3 publicly sasa. Huko Ikulu watu wanajua kwamba kashaanguka zaidi ya mara hizo privately. Hakuna rais wa Tanzania aliyewahi kudodoka kabla.

Tuambizane ukweli tu kwamba rais mgonjwa, mficha ugonjwa (ashakum) mauti humuumbua.
 
Siyo kila mara Jangwani kwenye uzinduzi.
Mara ya kwanza(2005) alikuwa anafunga kampeni alipoanguka ikabidi Che Nkapa aje atulize umati, yeye Kikwete alikimbizwa sehemu-sehemu.
mara ya pili leo anafungua kampeni, Makamba et al wameshindwa kabisa kuubeba umati na kuutoa katika simanzi.
Hata aliporudi Kikwete mwenyewe na namna aliyokatisha houtuba, maswaali yanazidi kuongezeka.

...Wewe umeona kama mimi. Ukweli ni kwamba hta aliporudi kuhutubia tena usoni alionekana dhahiri kuwa hakuwa katika hali ya kawaida. Ilifurahisha/ilisikitisha jinsi viongozi wa ngazi za juu wa ccm walivyobaki wamepigwa bumbuazi hawajui wafanyeje zaidi ya YMakamba kuhimiza TOT waendelee kutumbuiza! Nyuso za wanachi wengi zilizovutwa kwenye screen za TV zilionyesha kutaharuki.

Na vituo Vyetu vya TV na waandishi wake navyo vikafeli mno katika hili. Ghafla vyote vikaacha kutangaza na kutuachia picha tu bila kutueleza kinachoendelea. Star TV wao ndio kabisa wakaharakisha kuweka tangazo na baadae kidogo ndio wakalitoa. Na hata watangazaji walipoanza kutangaza hakuna ambaye aligusia tukio lile. Ni kama vile halikutokea kabisa!!

Na usishangae kesho taarifa ya kuanguka raisi jukwaani haitaandikwa kwa mapana na marefu yake kwa mfano kuhoji viongozi wengine kama tukio lile litaathiri kampeni za chama, kumohiji dakitari wake, kumhoji hata mama Salma kwamba mzee alikuwaje toka asubuhi. Sio vyombo vyetu hivi.
 
......kikwete ameshaanguka mara 4[nne] hadharani...yaani mara mbili jangwani na mara mbili kirumba mwanza [ikiwemo aliyoanguka kwenye shughuli ya kanisa la AIC-hakuwa amefunga ].....na pia amewahi kuzirai mara kadhaa akiwa ndani,.....according to insiders.......

there is a problem ...!

pia nime note kwenye hutuba yake kuwa anasoma sana mitandao....ametoa moja " siku hizi tanzania kuna mitandao ...kwenye mitandao wanaandika sana sana ...lakini nawaambia kuwa ..watanzania hawadanganyiki..."

Hajaanguka mara nne kama unavyodai bali ameishiwa nguvu mara 3 na mara moja alivamiwa jukwaani kule Mwanza.

Hao insiders wanaotoa habari za Rais au za ndugu yao unaona wana akili timamu au maamuma? Wewe umewahi kutoa siri za mkeo, mzazi au ndugu wa karibu na watu wakakushangilia? Tutajuaje kama mtoa habari wako hamtakii mema Rais hata akakupa habari za uongo?

Ni makosa makubwa kufikiri kwamba Rais haugui. Kumbuka Rais Mkapa aliugua mguu na kulazwa Uholanzi kwa muda watu wakasema kagombana na mkewe wakati ukweli kwa umri wake tatizo la nyonga n jambo la kawaida
 
..Kuna mwanajamii ameishasema. Ghafla kutakuwa na michango kibao kuhusu hili kutoka kwa wanachama wapya wa JF wenye posts kati ya 4 hadi 10 na wote wanatetea kutokea kwa tukio hilo. Poor We.
 
Iwe ameanguka mara tatu au mara nne, the difference is the same. Na huu ni mwanzo wa kampeni. Atahimili kweli mikikimikiki ya joto la kampeni hadi Oktoba? Tuwe wawazi na wakweli.
 
Pili, naye kacheza faulo. Kwasasa nchi inapaswa kuwa chini ya Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wewe ndio mbumbumbu la kihistoria, kaanze darasa la kwanza kijijini kwenu, Katiba gani unaongelea? ya kupikia maandazi yako hapo chini ya mti unakokunywa kahawa bila kufanya kazi yoyote? Kwa taarifa yako Katiba inasema wazi nchi haiwezi kuwa bila Rais hata sekunde moja, kasome mbumbumbu nambari wani wewe.
 
Hajaanguka mara nne kama unavyodai bali ameishiwa nguvu mara 3 na mara moja alivamiwa jukwaani kule Mwanza.

Hao insiders wanaotoa habari za Rais au za ndugu yao unaona wana akili timamu au maamuma? Wewe umewahi kutoa siri za mkeo, mzazi au ndugu wa karibu na watu wakakushangilia? Tutajuaje kama mtoa habari wako hamtakii mema Rais hata akakupa habari za uongo?

Ni makosa makubwa kufikiri kwamba Rais haugui. Kumbuka Rais Mkapa aliugua mguu na kulazwa Uholanzi kwa muda watu wakasema kagombana na mkewe wakati ukweli kwa umri wake tatizo la nyonga n jambo la kawaida

Ohoo dear... eti aliishiwa na nguvu ila hakuanguka.....ohooo dear
 
..Kuna mwanajamii ameishasema. Ghafla kutakuwa na michango kibao kuhusu hili kutoka kwa wanachama wapya wa JF wenye posts kati ya 4 hadi 10 na wote wanatetea kutokea kwa tukio hilo. Poor We.
.

kama wana hoja tatizo liko wapi? jukwaa letu ni hoja mbele haijalishi upya, uzee mtandaoni au uzoefu.
 
Pili, naye kacheza faulo. Kwasasa nchi inapaswa kuwa chini ya Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wewe ndio mbumbumbu la kihistoria, kaanze darasa la kwanza kijijini kwenu, Katiba gani unaongelea? ya kupikia maandazi yako hapo chini ya mti unakokunywa kahawa bila kufanya kazi yoyote? Kwa taarifa yako Katiba inasema wazi nchi haiwezi kuwa bila Rais hata sekunde moja, kasome mbumbumbu nambari wani wewe.
Buure mnatoana macho.... rais awepo rais asiwepo yote sawa.... hamna tofauti..
 
Mimi nasubiri spin ya wapambe (w)akiwemo (ma)daktari wake.

Ila kama ana matatizo ya kiafya sioni ulazima wa yeye kuendelea na kazi ya uraisi. Tayari keshakuwa raisi na itakuwa hivyo kwenye vitabu vya historia milele na milele na atatunzwa na serikali mpaka siku yake ya mwisho. Sasa sielewi sababu ya yeye kutaka kuendelea kuwa raisi ilhali hali yake ya kiafya si njema.

Mtu mwenye afya njema hawezi kuanguka anguka kama huyu jamaa. Kibaya au kizuri, ugonjwa haufichiki. Unaweza kujaribu kuuficha lakini ipo siku utakuumbua tu.

Halafu mbona maraisi wetu hawazeeki haraka wakiwa madarakani? Obama sasa hivi ukimwona keshaanza kuwa kibabu. Lakini hawa wa kwetu ndio kwanza wanazidi kuwiva. Hawafanyi kazi hawa....
 
  • Thanks
Reactions: 911
Jamani nimepata taarifa eti Kikwete kadodoka jukwaani wakati anahutubia kwenye viwanja vya Jangwani mwenye uhakika atupe.........
kumbe haupo nchini???

blah blah blah
 
usichanganye mchanga na sukari! Slaa ameteleza yaani mabafu ya ma-guset na mahoteli yetu tiles hazina viwango! JK kadondoka kwa afya mbovu! tuseme ukweli

nyumba zetu nyingi zina Tiles mbona hatudondoki kama Dr Slaa. Mgombea Urais atalalaje Guest house????????? maaana ya Guest house unaijua????????? Mwanza kuna Hotel kabao za hadhi ya Rais mtarajiwa
 
Hajaanguka mara nne kama unavyodai bali ameishiwa nguvu mara 3 na mara moja alivamiwa jukwaani kule mwanza. Hao insiders wanaotoa habari za Rais au za ndugu yao unaona wana akili timamu au maamuma? wewe umewahi kutoa siri za mkeo, mzazi au ndugu wa karibu na watu wakakushangilia? tutajuaje kama mtoa habari wako hamtakii mema Rais hata akakupa habari za uongo? Ni makosa makubwa kufikiri kwamba Rais haugui. Kumbuka Rais Mkapa aliugua mguu na kulazwa Uholanzi kwa muda watu wakasema kagombana na mkewe wakati ukweli kwa umri wake tatizo la nyonga n jambo la kawaida

.....aah ...simply ameshaanguka mara nyingi ,maana nyingi inaanzia mbili..

unaongeelea insiders .....si hao wenzeu ...mliowapa kazi kwa kujuana....vichwa vya pazi ...wakipewa bia mbili tu pale mzelendo wanaanza kuropoka ....hawana ethics.....hadi tunaona aibu...kama kweli hawa ndio waliomzunguka ...wale wazoefu mmewatupa wapi?????..au kwakuwa hawakuwa mtandawo!!!

...alafu point of information....mkapa hakulazwa netherlands alilazwa ...switzerland...!!..alikuwa ansumbuliwa na kifundo cha kiuno ....that was made publicly and script zake akiwa hospitali na kwenye physiotherapy hazikuwa siri....

kama ni kufunga mzee mwinyi anafunga hata saa akiwa na miaka 85 ..haanguki!
 
Back
Top Bottom