Kikao cha CCM: RA Atema Cheche "Nitajiuzulu...."

The next step wataleta hoja ya ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika; Sitta ataondoshwa (kwani wabunge kadhaa watapangiwa visema kule nje na kura itapigwa). Akiondoshwa atawekwa Spika wao (jina tunalo) ambaye ataridhia maombi ya kina RA na Sofia. Ndipo tume wataiunda wao na kina RA na EL watasafishwa rasmi kwa kutumia utaratibu wa kibunge na hivyo maamuzi kuwa legally binding.

Tayari kwa karibu wiki kadhaa sasa pesa imetembea Dodoma kwa ajili ya jambo hili na kwa ajili ya kupata support ya wabunge. Novemba 7 ni siku muhimu kwa ajili ya hili.

ntafurahi ikiwa haya yatatokea...naamini ni blessing in disguise.....
 
Hi,

Yanayoendelea ndani ya CCM ni aibu tupu,watu wanajadili mambo ambayo hayana msingi wameacha kutekeleza sera za chama chao,wanaendeleza malumbano ya watu binafsi,ambayo haya wasaidii watanzania.Angekuwapo Mwalimu wange koma,

Na Huyu mwenyekiti wa CCM hana memo ya kung'atia?

Elisante
wa DSM
 
Habari nilizozipata toka ndani ya Kikao cha Tume ya Mapatano na Maridhiano ya CCM na wabunge wake kilichomalizika jana hapa mjini Dodoma, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ametema cheche na kukubali kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama iwapo itaundwa tume huru kuthibitisha yale ya tume ya Mwakiembe.

.........
RA alishauri iundwe Public Inquery ikigundua kuhusika kwake, yeye atajiuzulu nyadhifa zake zote.

Hata hivyo, RA hakuzungumzia kabisa issue za Kagoda kama uthibitisho wa dhati kuwa hahusiki aslan.:mad::mad:

Upapa mwingine huu. Eti tume huru iundwe akibainika atajiuzulu! Aendelee na nyazifa zake, sasa autafute hata nafasi ya mwenyekiti wa ccm taifa au ukatibu mkuu. Who cares! Zaidi ya miaka 40 nchi imeendelea kuwa duni, sasa jipu lipombioni kupasuka. NAWASHAURI CCM WAENDELEE KUMKUMBATIA NA KUMPA NAFASI ZOTE ZA KICHAMA ILI KUJIIMARISHA NA KUWAJENGA WATAWALA WA TANZANIA. Ukistajabu ya Musa utaona ya firausi! ama kweli, RA anaamini kuwa ataendelea kuwa mashine ya kutoa viongozi wa Tanzania!
 
Mimi nashngaa sana kuona mtu kama RA bado anaendelea kuwa na madaraka ndani ya Chama, Sasa GOV itaendela na tume tume mpaka lini Hela za wananchi mnazitumbua sawa sawa kwa ajili ya hizo tume sasa Jambo la Msingi M/Kiti wa chama Meno unayo toa kauli moja ya kueleweka kwani wewe ulishapitia Ujeda sasa kumvutia subra unasiri nini? au huyu ni swaiba wako anajitamba sana ... eti iundwe tume. yanini? Toa Maamuzi kwani mpaka sasa tunapokwenda Chama Chako Kipo Recycle bin Nasema Tumechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa na ukimya wako TUNAHITAJI MABADILIKO JAMANI aHHHHHH!!
 
Hapana. Chaguzi za mitaa mwaka 1999 na mwaka 2004 zilikuwa mbaya zaidi na tukapata viti hivyo tulivyopata Bungeni.

Kumbuka mwaka 2004 CUF walipata mitaa takribani yote Mbagala lakini hawakupata kiti hata kimoja cha udiwani. Kigoma CHADEMA ilikuwa na vijiji 2 tu mwaka 2004 lakini nilishinda ubunge na madiwani 4 katika ya 10.

Uchaguzi Mkuu utaamuliwa na ajenda za mwaka kesho na aina ya wagombea ubunge tutakaoweka. Ninaamini tutapa si chini ya 25% ya kura za wabunge nchi nzima na si chini ya wabunge 50. CUF wakipata vizuri zaidi Unguja maana Pemba yao na wakipata Mkuranga, Kilwa, Rufiji zote mbili, Temeke/Kigamboni, Pangani, Mtwara mjini na Tanga mjini tutafika theluthi ya wabunge na hapo ndio ntolee kwa CCM........... mark my words
Zitto,
Nakuheshimu kwa kutokata tamaa hata kama mgonjwa aliye mbele yako dalili zote zinaonyesha hatapona! CUF hawawezi kupata MBUNGE huku Bara labda Lipumba agombee huko kwao.

Nilikushauri wakati fulani humu mkajipange upya kwenye vyama vyenu. Hilo halikufanyika.

Msitarajie miujiza. Angalia rafiki zenu wa CONSERVATIVE kule kwa MAMA walivyokuwa wakijipanga upya kila wanapoanguka. Mara hii watafanikiwa sana tu.
 
Unguja maana Pemba yao na wakipata Mkuranga, Kilwa, Rufiji zote mbili, Temeke/Kigamboni, Pangani, Mtwara mjini na Tanga mjini tutafika theluthi ya wabunge na hapo ndio ntolee kwa CCM........... mark my words

Mbona huko kote ni predominantly moslem areas?...why not peramiho,vunjo?
 
CCM CCM CCM eeeh CCM inatuchosha na imetuchosa hata kuitamka na uozo wake
Kidumu chama cha mapinduzi
sijui kama wamekuwa mabubu ,viziwi ,vipofu ..
 
Mkuu Zitto,

Yaani RA naye ana line up towards 2015? Naomba mwenyezi Mungu asiniache hai kushuhudia matusi haya yakitokea!!!!

Tiba


Unaona sasa Uongo wa watanzania ......., kama ni kweli ungekuwa umeshajinyonga mwenyewe kwa yanayotokea Tanzania,

Ndugu, tema mate chini,
 
RA amepewa tenders kibao za kujenga barabara ili kurudisha fedha alizomkopesha JK wakati wa kampeni za uchaguzi. Hayo wanayokoromeana ni viini macho. Wote wanatakiwa waondoke ije damu nyingine yenye uchungu na nchi yao
 
Hivi wanataka kutumia pesa za walipa kodi ili kusafishana? mimi naona pesa hizo zingetumiwa kujenga zahanati vijijini badala ya kusafisha mafisadi, labda watumie pesa za chama chao lakini sio pesa za wavuja jasho wa tanzania.
 
Hapana. Chaguzi za mitaa mwaka 1999 na mwaka 2004 zilikuwa mbaya zaidi na tukapata viti hivyo tulivyopata Bungeni.

Kumbuka mwaka 2004 CUF walipata mitaa takribani yote Mbagala lakini hawakupata kiti hata kimoja cha udiwani. Kigoma CHADEMA ilikuwa na vijiji 2 tu mwaka 2004 lakini nilishinda ubunge na madiwani 4 katika ya 10.

Uchaguzi Mkuu utaamuliwa na ajenda za mwaka kesho na aina ya wagombea ubunge tutakaoweka. Ninaamini tutapa si chini ya 25% ya kura za wabunge nchi nzima na si chini ya wabunge 50. CUF wakipata vizuri zaidi Unguja maana Pemba yao na wakipata Mkuranga, Kilwa, Rufiji zote mbili, Temeke/Kigamboni, Pangani, Mtwara mjini na Tanga mjini tutafika theluthi ya wabunge na hapo ndio ntolee kwa CCM........... mark my words

Kwa hili Zitto, nimekukubali unajua nia yako kama mpinzani bungeni...achana kabisa na wanaowakatisha tamaa wapinzani, mara nyingi wala si wapiga kura. Wao maneno mengi na bora liende. Kaza buti kaka it might be difficult for others to see the light at the end of the tunel, lakini uionayo ndio hasa. Na macho yako hayakudanganyi
 
Ukiona Sophia na Rostam wanatamba kama walivyofanya sasa hivi, jiulize Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo wapi na yupo upande gani?

yupo upande wa mafisadi...si unakumbuka alisemaje pale diamond jubilee kuhusu EL....ile ni ajali ya kisiasa tu...
 
Zitto,
Nakuheshimu kwa kutokata tamaa hata kama mgonjwa aliye mbele yako dalili zote zinaonyesha hatapona! CUF hawawezi kupata MBUNGE huku Bara labda Lipumba agombee huko kwao.
Nilikushauri wakati fulani humu mkajipange upya kwenye vyama vyenu. Hilo halikufanyika. Msitarajie miujiza. Angalia rafiki zenu wa CONSERVATIVE kule kwa MAMA walivyokuwa wakijipanga upya kila wanapoanguka. Mara hii watafanikiwa sana tu.
Conservative wanapigana siasa katika nnchi ambayo mfumo wake hauna zegwe wala uchafu kama huu, siasa za Nyumbani Afrka, zinapiganwa katika mazingira mazito, vitisho ,nogwa na kuchukiana, urafi wa siasa ni mwingi hebu angalia yanayotokea Kenya, Zimbabwe na serikali zetu za mpito, pamoja na yote hawa kina Zito wanafanya siasa katika mazingira ya hatari, vitisho vya usalama wa taifa, na upuuzi mwingine kama huo.
 
Kifuatacho ni kuundwa kwa tume ya kuchunguza tume ya tume ya bunge kama imefanya kazi yake au la,
 
Mbona anachelewa kutangaza kujiuzulu,aondoke ,kwani tayari mbadala wake mgaganga wa jadi kisha jitokeza.kupingana na Dr. Kibuyu-makubwa haya???
 
Mkuu Mkandara,

Hao Mwakyembe na Sitta wako tayari kutumia greda kukwangua chochote kinachozuia ambitions zao.

Hata siku moja huwezi kuwa mpiganaji wa wananchi huku unatafuna wananchi hao hao.

Wengine tumeonja joto ya jiwe ya mbinu na siasa chafu za hao wapiganaji wenu.

Leo hii Mkandara ukiamua hata kwa kujaribu kugombea jimbo la Sita au yule Sendeka, utaipata joto ya jiwe ya hao wapiganaji wenu. Ghafla utakuwa umetumwa na Lowassa hata kama maishani mwako hujawahi kuonana na Lowassa. Ghafla utakuwa umepewa bilioni moja hata kama mfukoni unahangaika hata kupata laki moja ya kumsaidia campain manager wako.

Mtu anayeweza kukaa na kupanga jaribio la kuuawa na kuudanganya umma mzima huku anajua ni uongo, ni mtu wa kumwogopa sana maana akiwa na nafasi sidhani kama ataogopa kukuweka ndani au kukumalizia mbali ili kusafisha njia yake.

Mtu ambaye yuko tayari kuangamiza wapinzani wake kwa njia zozote zile haramu hata siku moja hawezi kuwa mpiganaji wa wananchi.

Mimi naamini usafi lazima uanzie kwangu; lazima nijisafishe mimi kwanza kabla hata ya kujaribu kumsafisha mkandara.

Usipoamini katika sheria na uongozi wa haki, hata siku moja usitegemee utaweza kuwa polisi wa kusimamia sheria na haki nyumbani kwa mtu mwingine.

Haya yanayotokea sasa ni vizuri yatokee ili kila mtu aone CCM ilipofikia na aina ya watu walioko huko ndani. Kizuri zaidi inaonyesha mahali ambapo Watanzania tumefikia na bila kubadilika tusigemee maendeleo yoyote ya maana.

Kundi la Sitta walimpata Lowassa na kundi lake kwenye Richmond na mimi naamini ilikuwa nafasi nzuri ya kuisafisha serikali. Lakini kilichowaponza ni furaha ya kupata nafasi ya kumdhuru mbaya wao, wakasahau kuwa waangalifu na kuhakikisha katika hiyo assasination wanakuwa fair na wanawapa nafasi ya kutosha hao watuhumiwa kuweza kujitetea. Kila mtu anajua Karadzicz kule Serbia aliua wabaya wake lakini dunia inampa kila nafasi ya kujitetea hata kama ni obvious kwa kila mtu kwamba jamaa hawezi kushinda case. Wahandisi tunasema garbage in garbage out. Ukiharibu process ya kitu chochote, mwisho wake unapata madudu.

Hata wananchi wa vijijini tayari wanaanza kuelewa nani anasema ukweli, nani ana nia ya dhati kutetea maslahi yao, nani wanaimba ngonjera na wote tutajua ukweli hapo 2010.



Rev. Kishoka,

Mkuu twende mbele turudi nyuma kidogo..

Hivi mnawafikiria CCM wajinga kiasi gani vile.. Yaani hawa wapiganaji kama sii lolote sii chochote iweje hili swala la Richmond limewakuna Mafisadi kiasi hicho.. imefikia hata watu kutukanana matusi ya nguoni, kumbuka ugonvi wa mkutano wa Kamati kuu ya chama, lugha zilizotoikea pale..Leo hii wewe mkuu wangu unazungumza LUGHA ya Sophia Simba, wewe mchungaji unakubaliana na kina Sophia kwamba hata kina Sitta ni mafisadi ktk utetezi wa mtu Fisadi..

Mkuu wangu yawezekan Sitta fisadi lakini kesi moja baada ya nyingine, Marekani walikwenda Afghanstan kwa sababu ya 9/11 na dunia tulikuwa nyuma yao, sasa kama tungeanza kusema marekani nao ni Materrorist size yao kweli hali ya maisha yetu Ulaya ingekuwa hivi..Sote kwa ujumla tulilaaani terrorism kwa sababu sote tulikuwa hatarini na kama tungeshangilia hayo matokeo yake kina Osama wangepiga miji yote ya Marekani na nchi zote za Ulaya kwa sababu sisi tumewapa nguvu.

Ndicho mnachokifanya hapa..mnashindwa ku take a stand badala yake mnakumbwa ktk kiza kinene cha mbinu za mafisadi.. Ikiwa Mwakyembe na Sitta ni mafisadi kwa nini kesi zao hazifikishwi bungeni au mahakamani... Kama iliwezekana kuchukuza BoT, EPA, Richmond na mashirika mengine iweje shida kuwafikisha mahakamani watu hawa badala yake zinapigwa simu za kuhoji wabunge na posho zao.

Of all Ufisadi jamani posho imekuwa kitu cha kujibu mapigo!

Mkuu wangu Uhasibu nimeufanya na naelewa wazi kabisa malipo yoyote yale ya serikali yanapitishwa vipi..Mbunge hawezi kuilazimisha wizara kutoa posho isipokuwa serikali yenyewe iliweka posho hizo ktk kifungu cha matumizi toka mwanzo, besides kuchukua posho mbili sioi crime hata kidogo maadam invoice na cheki vimepitishwa kisheria na maofisa wanaotakiwa kupitisha. sana sana mbunge huyoi atatakiwa kurudisha fedha alizopewa zaidi, kama hana atakatwa ktk mshahara au posho zijazo lakini posho mbili sio swala la RUSHWA hata kidogo kwani lipo ktk kifungu cha matumizi ya wizara, shirika au taasisi. Kama kuna kukamata mtu basi yule aliyepitisha matumizi hayo ndiye wa kushinkwa koo..

Pili, hapakuwa na sababu kabisa ya Hosea kwenda Bungeni wakati wa bunge ati kumwona Spika..Mkuu wangu, vita hii isingekuwa kubwa hivi kama kweli hawa wote lao ni moja..
 
.
Kwa vile jamaa ni king maker, hili ombi la tume huru ni zuga ya kujisafisha, he is there to stay to make the 2015 king!.

Rostam is a cornered cat! A cornered cat a very dangerous animal! What he wants is almost impossible as it would create havoc. But He is being clever by half by trying to wood wink his party into something very foolish so to speak.

By suggesting that another probe team be tasked to prove the veracity of the Mwakyembe probe report and once proved to be correct then he will throw in the towel is being very insincere. The least he could have done is to suggest that he resigns first and let the party look into the matter again and once found clean of the Richmond misconduct the party could consider exonerating him.

But again with all that influence and machinations RA commands in CCM, the outcome of the said probe committee would be a foregone conclusion. I hope this time around the CCM top leadership will see through all these calculated diversionary tactics and call a spade a spade. It is time to draw the curtain on RA & EL theatrical antics!
 
Ha haha hahahh. Tayari kuna viraka juu ya viraka ingawa ni katiba changa kabisa.

Mwakani Februari tunaweka viaraka vingine katika nafasi za wabunge ili kuongeza wabunge kufikia 360 kama kikomo na kuongeza wabunge wa viti maalumu kutoka 75 mpaka 116.

Badala ya kuwa ngangali iandikwe katiba mpya mnafurahia kuweka viraka vya kuongeza vilemba ukumbini!! MUNGU atawalaani mtapukutika wote!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom