Kikao cha CCM: RA Atema Cheche "Nitajiuzulu...."

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Habari nilizozipata toka ndani ya Kikao cha Tume ya Mapatano na Maridhiano ya CCM na wabunge wake kilichomalizika jana hapa mjini Dodoma, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ametema cheche na kukubali kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama iwapo itaundwa tume huru kuthibitisha yale ya tume ya Mwakiembe.

Miongoni mwa Cheche alizotema, ni pamoja na kumlipua Spika Sitta kana kwamba ni kumkomelea msumari wa mwisho kuthibitisha chuki binafsi za Spika Sitta dhidi ya Edward Lowassa.

RA amesema Kamati ya Mwakiembe ni siasa chafu, ni ubia kati ya Spika Sitta na Mwakiembe dhidi ya Lowassa na Rostam.

RA anadai Six aliomba kwa El kupewa nyumba yenye hadhi yake Dar es Salaam na Dodoma pamoja na ofisi yenye hadhi, Urambo, EL alimtilia ngumu kuwa ni kinyume cha taratibu. Pia aliomba lami toka Urambo-Tabora na Motorcade lakini EL alimgomea, hivyo jamaa akawa na hasira na kutafuta upenyo wa kufanya visasi.

RA alishauri iundwe Public Inquery ikigundua kuhusika kwake, yeye atajiuzulu nyadhifa zake zote.

Hata hivyo, RA hakuzungumzia kabisa issue za Kagoda kama uthibitisho wa dhati kuwa hahusiki aslan.:mad::mad:
 
Haya maneno gani lakini jamani.. Huyu RA na Wabunge wote Mafisadi hawafahamu kwamba Spika Sitta is third in line ktk uongozi wa nchi?..
 
Yaani tutumie mamillioni ya kodi kwa ajili ya kutafuta Rostam ajiuzuru! mbona hiki ni kichekesho. dah! Rostam ...
 
Haya maneno gani lakini jamani.. Huyu RA na Wabunge wote Mafisadi hawafahamu kwamba Spika Sitta is third in line ktk uongozi wa nchi?..
.
Kwa vile jamaa ni king maker, hili ombi la tume huru ni zuga ya kujisafisha, he is there to stay to make the 2015 king!.
 
Yaani tutumie mamillioni ya kodi kwa ajili ya kutafuta Rostam ajiuzuru! mbona hiki ni kichekesho. dah! Rostam ...

Sio kutafuta RA ajiuzulu bali kama Tume ya Mwakiembe ilisema kweli, ilitenda haki na hakua na motives behind mlolongo wa majungu haya yanayoendelea.
 
Haya maneno gani lakini jamani.. Huyu RA na Wabunge wote Mafisadi hawafahamu kwamba Spika Sitta is third in line ktk uongozi wa nchi?..

So? kila mtu si ana uhuru wa kusema yake! kama vipi sitta anaweza kufuata sheria...
There is probably some truth in this! U can never know. For i personally dont believe sitta na mwakyembe ni 'wapiganaji'. Hakuna mpiganaji ndani ya CCM. Yote ni changa la macho...
 
.
Kwa vile jamaa ni king maker, hili ombi la tume huru ni zuga ya kujisafisha, he is there to stay to make the 2015 king!.
I don't think so.. JK hawezi kabisa kumsogelea Rostam sasa hivi watakutana faragha na sio kumtumia mtu huyu tena..Ndio maana nikasema Rostam hahitaji kuwa mbunge isipokuwa member wa NEC tu inamtosha..tena he so powerful kiasi kwamba anaweza kuwa pembeni na mambo yakajipaga..
Mfano mzuri, Chande na Apson, manji, Patel na wengineo wengi wenye mivunda ya uhakika.
 
Sio kutafuta RA ajiuzulu bali kama Tume ya Mwakiembe ilisema kweli, ilitenda haki na hakua na motives behind mlolongo wa majungu haya yanayoendelea.

Kwa hiyo iundwe tume nyingine kwa ajili ya Richmond? Oops lini tutaacha kutumia pesa zetu vibaya? lini tutaachana na richmonduli na tukaelekeza nguvu ktk miradi ya maendeleo na matatizo lukuki ya elimu na njaa? By the way lugha ya mwakani ni uchaguzi. Tutaondoka lini kwenye bonde hili?
 
So? kila mtu si ana uhuru wa kusema yake! kama vipi sitta anaweza kufuata sheria...
There is probably some truth in this! U can never know. For i personally dont believe sitta na mwakyembe ni 'wapiganaji'. Hakuna mpiganaji ndani ya CCM. Yote ni changa la macho...
CCM bado ina viongozi wachache ambao ni wasafi crystal clear, na pia miongoni wa wapiganaji, wako baadhi ni wapiganaji wa kweli, wengine ni wapiganaji kutimiza malengo yao ya agenda zao, na wengine ni njaa zao tuu kazi yao kulishwa maneno na mfadhili wao mkuu na kuja kuyatapika bungeni.
 
mfano....
 
I don't think so.. JK hawezi kabisa kumsogelea Rostam sasa hivi watakutana faragha na sio kumtumia mtu huyu tena..Ndio maana nikasema Rostam hahitaji kuwa mbunge isipokuwa member wa NEC tu inamtosha..tena he so powerful kiasi kwamba anaweza kuwa pembeni na mambo yakajipaga..
Mfano mzuri, Chande na Apson, manji, Patel na wengineo wengi wenye mivunda ya uhakika.
.
Mkandara, King Maker ameshantengeneza King JK, its done. His job is to make the next king. Hivyo hayo yote sio for 2010, ni for 2015. Amini nawaambie whoever who will be king in 2015, must side with the King Maker na kina Sitta wanatengeneza aliance out of King Maker, mwisho wa siku, ni mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama, if you ncant beat them, you have to join them.
 
Haya ni maneno ya mfa maji,mbona tuhuma hizi hawakuzileta mapema.

Rostam anatwambia nini watanzania kuhusu kashfa ya Kagoda.

Si tashangaa kama kuna baadhi yetu tutaamini maneno yake na kumwona kama ana kitu cha kusema maana "miafrika/watanzania ndivyo tulivyo"

Jambo la pili ni kwamba Mafisadi hayana wasiwasi wowote maana wanajua watanzania sisi ni wazuri wa kuchonga mdomo tu inapofika vitendo tunaingia mitini aidha kwa kununuliwa kwa gharama ndogo sana.

Ukombozi wa dhati utapatikana endapo wananchi wanaonunuliwa kwa bei ya kutupwa watakapo elimishwa ili wasibweteke na vijizawadi ambavyo vinawaghalimu kwa takribani miaka mitano.

Yale ambayo tunayapata na kutukereketa humu mtandaoni je yanawafikia hasa wale walio vijijini ambao ndo mtaji mkubwa wa mafisadi maana kwa kutokuelewa wananunuliwa kilahisi ndo maana mafisadi hawana pressure yoyote wanajua sisi humu tunapiga kelele za chura ambazo hazitawakataza kuchota maji.
 
Mkandara,

Wote RA na Sitta ni wanafiki na wapuuzi.

Hili suala la Sitta kulilia ving'ora lilikuja alipoingia Bungeni 2006 kama Spika na alipotunisha msuli akakalishwa kikao cha Kichama akabanwa gololi!

Sasa RA na Sophia Simba wanaunguza na kuropoka kile ambacho si Uzushi bali mambo ya unyumba ndnai yao.

Tatizo ni kuwa kina Sitta na Mwakyembe, waliona haya na kuamua kuinusuru Serikali na Chama AIBU na sasa kinawalipukia!

They are practically done unless wanaondoka CCM!
 
Pasco,

Kina Sitta hawawezi kupukutika kwa maana wao walishanunuliwa na kunyeshewa tarkima chafu kutoka kwa RA na their usefulness kwa RA and crew is over, they are not needed any more na ndio maana unayasikia aliyosema Sophia Simba na hili la RA leo.

Narudia tena, UPUUZI wa wapiganaji wa CCM ni kuangalia maslahi yao na si Maslahi ya Taifa na jinsi watakavyoangamia, hakuna atakayeamini kuwa walikuwa wakipigania maslahi ya Taifa.

Mfano hili la Posho, was an opportunity kwa Sitta and camp to clean the party and Serikali and show that they care about MWananchi. Lakini siasa ni mapiku, sasa wao wamegeuzwa msamba juu, huku walichokijua na walipaswa kukifanyia kazi kw aKunkoma Nyani Giladi, wakadai wanainusuru Serikali na wakaanza kutongozana na Serikali!

Sasa hivi Richmond, Kagoda, EPA and all other cases ambazo ziliihusisha CCM na Serikali iwe ni Lowassa, JK au Mkapa zimeshafutika machoni mwa Serikali, tusubiri tume ya usuluhishi miaka 30 ijayo CCM itakapoondolewa madarakani ndipo tuje kujua Meremeta alimnufaisha nani na ni nani kweli alikuwa Kagoda.

By that time, wahusika wote wakuu watakuwa ni ama hayati au marehemu!
 
Nilifurahia kapata upinzani jimboni kwake kumbe mganga wa kienyeji?

Licha ya Huyo mganga wa kienyeji na Mwanamazingira anayeishi D'salaam (Bw.Bakari Nyarobi),Pia kuna Taarifa zenye Uthibitisho kwamba Dr.Peter Kafumu - Kamishna wa Madini wizara ya Madini na Nishati anatarajia kutupa karata yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Igunga katika uchaguzi wa mwakani (2010).
 
hakuna chochote hapa........kwanzaRostam Aziz alistahili awe gerezani hivi tunavoongea. Edward Lowasa huyu ingekuwa ni China angekwisha nyongwa zamani. Wasituchefue....hivi wabunge hawaruhusiwi kuingia mkutanoni na bastora zao??? kuna watu wananstahili kuuliwa kwa sababu ya matamshi yao......chenge, sofia paka ni miongoni mwao.
 
Back
Top Bottom