Kikao cha CCM: RA Atema Cheche "Nitajiuzulu...."

Habari nilizozipata toka ndani ya Kikao cha Tume ya Mapatano na Maridhiano ya CCM na wabunge wake kilichomalizika jana hapa mjini Dodoma, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ametema cheche na kukubali kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama iwapo itaundwa tume huru kuthibitisha yale ya tume ya Mwakiembe.

Miongoni mwa Cheche alizotema, ni pamoja na kumlipua Spika Sitta kana kwamba ni kumkomelea msumari wa mwisho kuthibitisha chuki binafsi za Spika Sitta dhidi ya Edward Lowassa.

RA amesema Kamati ya Mwakiembe ni siasa chafu, ni ubia kati ya Spika Sitta na Mwakiembe dhidi ya Lowassa na Rostam.

RA anadai Six aliomba kwa El kupewa nyumba yenye hadhi yake Dar es Salaam na Dodoma pamoja na ofisi yenye hadhi, Urambo, EL alimtilia ngumu kuwa ni kinyume cha taratibu. Pia aliomba lami toka Urambo-Tabora na Motorcade lakini EL alimgomea, hivyo jamaa akawa na hasira na kutafuta upenyo wa kufanya visasi.

RA alishauri iundwe Public Inquery ikigundua kuhusika kwake, yeye atajiuzulu nyadhifa zake zote.

Hata hivyo, RA hakuzungumzia kabisa issue za Kagoda kama uthibitisho wa dhati kuwa hahusiki aslan.:mad::mad:

Anamtishia nani sasa! kwani bado anahitajika??????? aende zake bana
 
Thank You hakuna sababu ya kutumia mabillioni wakati ukweli upo wazi... AONDOLEWE!

Inaelekea hataki kuondoka labda wamfukuze chama na Kikwete hawezi kuthubutu maana madhambi yake yote ya kampeni za 2005 papa fisadi RA anayajua maana yeye ndiye aliyekuwa sterling wa madudu yale. Duh! Kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu sikuamini kuja kuona kusshuka nidhamu kwa kiasi hiki ndani ya chama na Serikali.
 
The next step wataleta hoja ya ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika; Sitta ataondoshwa (kwani wabunge kadhaa watapangiwa visema kule nje na kura itapigwa). Akiondoshwa atawekwa Spika wao (jina tunalo) ambaye ataridhia maombi ya kina RA na Sofia. Ndipo tume wataiunda wao na kina RA na EL watasafishwa rasmi kwa kutumia utaratibu wa kibunge na hivyo maamuzi kuwa legally binding.

Tayari kwa karibu wiki kadhaa sasa pesa imetembea Dodoma kwa ajili ya jambo hili na kwa ajili ya kupata support ya wabunge. Novemba 7 ni siku muhimu kwa ajili ya hili.

hivi hizo pesa wanazopewa zinakuwa na uwingi gani, mishahara wanayolipwa si haba, nyumba wanazo magari ndiyo hivyo tena, sasa hizi pesa wanachukua hili ziwapeleke wapi, ni lazima wajuwe kwamba hawatukomoi sisi wanajikomoa na wao pia, tunaishi kwenye tanzania moja, kama kigogo umeme hamna,basi kunakofata ni magomeni na mgao unaendelea kwahiyo pesa ya msimu inakufanya uuze utu wako. shame jamani
 
Unguja maana Pemba yao na wakipata Mkuranga, Kilwa, Rufiji zote mbili, Temeke/Kigamboni, Pangani, Mtwara mjini na Tanga mjini tutafika theluthi ya wabunge na hapo ndio ntolee kwa CCM........... mark my words

Mbona huko kote ni predominantly moslem areas?...why not peramiho,vunjo?

So what if they are moslem areas? whatif the moslems have no faith with CCM and realize that CCM is a beast, however the Wakristo of Peramiho and Vunjo are still turning Shavu la Kushoto na Kulia and chant Mpende Adui or is it Mpende Jirani yako?

Your statement shows that Wakristo are great beneficiaries of Matunda na Kazi za CCM!

Otherwise if that was not your intent, then why bring UDINI?
 
Yaani tutumie mamillioni ya kodi kwa ajili ya kutafuta Rostam ajiuzuru! mbona hiki ni kichekesho. dah! Rostam ...

Hiyo tume labda itoke Scotland Yard ndio itaonekana huru hata kama ushahidi uko wazi. Halafu ikishatoa hukumu asiyoitaka Rostam atasema iundwe tume nyingine kuichunguza hiyo tume.
 
Mtanzania,
Mkuu wangu kwanza pole sana.. ndio siasa za Bongo hizo kwani hakuna jimbo lolote unaloweza gombea kwa tiketi ya CCM ukawa salama - HAKUNA..hivyo sii tu kina Sitta na Mwakyembe isipokuwa ni tabia zenu nyote kama chama. Sitta na Mwkayembe wote wamepata upinzani toka vyama vya Upinzani hna sikuona mauaji au kitu kinachokaribia hivyo. Utanisamehe nitakuja strong kidogo kukupa changamoto!

Nina swala, hivi Katika kujisafisha wewe... Je, unaweza kusema wazi EL na RA ni Mafisadi?.. au usafi ni wa mwili wako na sii kauli..Hivi Unafiki wa mtu ni usafi au?.. sasa kama wewe unataka kujisafisha nakuomba ulaani vitendo vya kina Lowassa, Rostam na wengine wote kwani usafi wa mtu huanza kwa kufahamu matendo mabaya..Hivi ukiona mtu kaua inabidi usireport hadi wewe utakapo kisafisha na makosa ya uasherati au kuchukua posho mbili!
Tofauti kubwa ya WApiganaji na wengine wote ni kwamba hawa wanatoa report ktk vyombo vya sheria na hao kina RA wanazungumza haya pembeni kazi kuita waandishi wa habari wakidai wapiganai nao sii wasafi...

Mkuu wangu tatizo lako na hao kina Mwakyembe na Sitta mnagombea kipande cha mkate ambacho kila mmoja wenu ndio shibe yake. has no interest in political balance towards social harmony and common good, na ndicho nilichjokiona hapa JF.. Kifupi mkuu wangu utanisamehe lakini usafi ungeuanza hapa JF, kila nilichosoma ktk kuburuzana kwenu nimewasoma kama ni selfintrest zaidi..Kila mmoja wenu anarusha magumi pasipo kukubali kujitazama yeye. It's been wewe hivi wewe vile, mimihivi mimi vile, na hakuna mmoja wenu anayekubali kujitazama na kutambua mapungufu yake..

Mwakyembe na Sitta wanaweza kutokuwa wasafi, but they represent our problem na our needs Kitaifa, hivyo sifa zangu kwa Sitta na Mwakyembe ni ktk maswala yanayolihusu taifa zima.. Hayo ya Kyela nawaachia wana Kyela.

Na kusema kweli nimeshindwa sana kukupa support moja kwa moja kwa sababu Mpiganaji wa kweli hujiunga Upinzani kwa lugha yangu kuwa Conservative kifikra ili upate kuisafisha system ilinayowabeba Mafisadi..Haramu ni Ufisadi, na ndicho kinachotakiwa kupigwa vita.. Usafi wa mtu unaanza na nafsi,uwezo wa kutambua mabaya na ukayakemea.

Kama ndio ingekuwa hivyo tusingekuwa na Mapadre, Masheikh na kadhalika wakitoa mawaidha na kufundisha neno la Mungu..Miyume wenyewe hawakuwa perfect ama niseme wasafi..kwanza hakuna mtu msafi na ndio maana tumeunda sheria, magereza na vyombo vya usalama.. Hiyo ndio kazi yao.. Sitta au Mwakyembe aren't clean wapelekeni ktk vyombo vya sheria..Na kama haiwezekani then system nzima inafail, systema mbayo wewe unataka kujiunga nayo..

Kama unataka kugombea Ubunge kwa sababu huridhiki na hali halisi ya Utawala uliopo na unataka kuleta mabadiliko ktk utawala basi jiunge na Upinzani wa sio kuwaletea wananchi mfumo ule ule wanaoupiga vita..Kyela haikuanza kutawaliwa na Mwakyembe, mapungufu ya Kyela hayakuanza miaka mitano iliyopita isipokuwa ni mlolongo wa viongozi wa CCM waliwakilisha wananchi wa Kyela kushindwa kuwaletea mabadiliko..And I believe wee pia utakuwa katika hesabu ya viongoz hao kwani changes haziletwi na kichwa kimoja isipokuwa policies za chama kinachoongoza.

lakini kama unagombea kwa sababu ya Mwakyembe au malalamiko ya wana Kyela, hapo mkuu wangu usiyachukulie mawazo yangu kwa uzito hivyo kwani all what ai'm for Upinzani wa system nzima iliyopo na sii WATU. Wapiganaji wana represent Upinzani na sii Upinzani wa jina la mtu...
 
Hawa mafisadi wanatuchezea ngoma gani, nchi hii siyo "pori" (wapumbavu) tena, kwani fedha walizonazo si zinatosha wao kuishi na familia zao? kwa nini wanang'ang'ania uongozi wakati wao ni wafanyabiashara? wawaachie nafasi hizo watu wenye sifa kweli za siasa, wapo wengi sana nchi hii, tena wanauchungu na umaskini wetu huu.
 
The man has said yuko tayari achunguzwe na tume huru.

Wangapi miongoni mwa watuhumiwe waliowahi kuwa na nerve ya kutoa challenge ya namna hiyo-almost non.

Munaopinga challenge aliyowapa RA sasa munataka nini, kama kweli munaheshimu sheria na taratibu na muko objective kwa nini mupinge tume huru?
 
The man has said yuko tayari achunguzwe na tume huru.

Wangapi miongoni mwa watuhumiwe waliowahi kuwa na nerve ya kutoa challenge ya namna hiyo-almost non.

Munaopinga challenge aliyowapa RA sasa munataka nini, kama kweli munaheshimu sheria na taratibu na muko objective kwa nini mupinge tume huru?

Nani mwenye mamlaka ya kuunda tume ya kumchunguza RA? Sitta, Kikwete, Makamba, au Hosea? Je ni kwanini wanasubiri mpaka RA awape hiyo unayoiita challenge?
 
RA, ni smart sana sababu watu wengi hapa wameingia mkenge wakidhani anaongelea tume huru inayoshirikisha vyombo na watu mbalimbali, HAPANA TUME anayozungumzia Rostam itaundwa na CC/NEC kupitia Sekretarieti ya CCM ambayo RA anacontrol kwa zaidi ya 90%.

Outcome hapa ni wazi kuwa RA atasemwa kuwa clean.

Angekuwa mkweli, sababu kamati ya Mwakyembe ilikuwa ni kamati ya Bunge, angesema mambo ya tume Bungeni ili wabunge including kina Slaa, Zitto wawe na nafasi ya kuingia kwenye hiyo tume ili tujue ukweli!!
 
Sio kutafuta RA ajiuzulu bali kama Tume ya Mwakiembe ilisema kweli, ilitenda haki na hakua na motives behind mlolongo wa majungu haya yanayoendelea.

Pasco Pasco give us a break. Na hiyo tume itakayoundwa kuichunguza tume ya Mwakyembe nayo tutaiundia tume ya kuichunguza? damn RA damn him again.
RA huhitaji tume nyingine ikuchunguze wewe jiuzulu tu. uchafu wote uliyoifanyia nchi yetu huhitaji microscope kuuona hata kipofu anauona kirahisi sana!!
 
Habari nilizozipata toka ndani ya Kikao cha Tume ya Mapatano na Maridhiano ya CCM na wabunge wake kilichomalizika jana hapa mjini Dodoma, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ametema cheche na kukubali kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama iwapo itaundwa tume huru kuthibitisha yale ya tume ya Mwakiembe.

Miongoni mwa Cheche alizotema, ni pamoja na kumlipua Spika Sitta kana kwamba ni kumkomelea msumari wa mwisho kuthibitisha chuki binafsi za Spika Sitta dhidi ya Edward Lowassa.

RA amesema Kamati ya Mwakiembe ni siasa chafu, ni ubia kati ya Spika Sitta na Mwakiembe dhidi ya Lowassa na Rostam.

RA anadai Six aliomba kwa El kupewa nyumba yenye hadhi yake Dar es Salaam na Dodoma pamoja na ofisi yenye hadhi, Urambo, EL alimtilia ngumu kuwa ni kinyume cha taratibu. Pia aliomba lami toka Urambo-Tabora na Motorcade lakini EL alimgomea, hivyo jamaa akawa na hasira na kutafuta upenyo wa kufanya visasi.

RA alishauri iundwe Public Inquery ikigundua kuhusika kwake, yeye atajiuzulu nyadhifa zake zote.

Hata hivyo, RA hakuzungumzia kabisa issue za Kagoda kama uthibitisho wa dhati kuwa hahusiki aslan.:mad::mad:

Jamani hayo maneno in red si ndio aliyokuja nayo Zitto Kabwe hapa jamvini only 4 months ago, eti iundwe tume huru ya majaji kupata ukweli wa Richmond na wakati bunge ilishatolea maazimio.

Jumlisha na msimamo wake juu ya kununua mitambo chakavu ya Dowans, utaona unavyoweza kuconnect the dots kwa usanii wa Zitto. Defense yake utaskia anaweka maslahi ya taifa mbele, ni kama vile Sofia Sima anavyoweka "maslahi ya taifa" mbele.

It is now becoming increasingly clear that Zitto Kabwe ni mouth piece ya mafisadi. Ameshakua highly compromised huyu kijana amebaki kutaka kuvuruga watu.
 
Huu upumbavu mbona Sitta anastahili hivyo vyote alivyoomba motorcade ni haki yake nyumba Dar ni haki yake na ofisi jimboni kwake ni haki yake mbona hivi ni vitu vidogo jamani? Hivi hii nchi ina njaa kiasi hicho cha kudanganya na visingizio vya kijinga? kama barabara kwenda Urambo kwani ataitumia peke yake au wana Urambo pia?
 
Nani mwenye mamlaka ya kuunda tume ya kumchunguza RA? Sitta, Kikwete, Makamba, au Hosea? Je ni kwanini wanasubiri mpaka RA awape hiyo unayoiita challenge?


Kama wao wanasubiri na wewe hukufanya lolote sasa wa kulaumiwa ni RA ama wewe na wao?

Kama una uhakikia RA ni fisadi kwa nini usipeleke ushahidi kwa wahusika?

Hata huko nyuma RA alishatoa challenge kwa wambea na wadaku wote wanaoamini yeye ni fisadi wapeleke ushahidi kwenye vyombo vya dola.

Sasa afanye nini zaidi ya kukupa changamoto umpeleke mbele ya vyombo vya sheria.

The man is too smart for ordinary Tanzanians. You have to giove him credit for that. RA anaona miaka 10 ahead wakati Mtanzania wa kawaida hata kesho haioni!!!
 
Kama unataka kugombea Ubunge kwa sababu huridhiki na hali halisi ya Utawala uliopo na unataka kuleta mabadiliko ktk utawala basi jiunge na Upinzani wa sio kuwaletea wananchi mfumo ule ule wanaoupiga vita..Kyela haikuanza kutawaliwa na Mwakyembe, mapungufu ya Kyela hayakuanza miaka mitano iliyopita isipokuwa ni mlolongo wa viongozi wa CCM waliwakilisha wananchi wa Kyela kushindwa kuwaletea mabadiliko..And I believe wee pia utakuwa katika hesabu ya viongoz hao kwani changes haziletwi na kichwa kimoja isipokuwa policies za chama za chama kinachoongoza

Mkuu Mkandara,

Hoja yako ndiyo niliipigia sana kelele zama zile za msuguano wa wana-Kyela mara baada ya mwana JF kutangaza nia ya kugombea.

Kwa mazingira yaliyopo ndani ya CCM hivi sasa, kweli mtu ambaye ana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko anaweza kwenda kugombea kupitia CCM? How many times wabunge wa CCM wamefungwa midomo wasiseme maovu ya wenzao ama ya serikali? Tena wengine kwa kutishiwa maisha.

Hivi kweli tuhuma inamhusu Makamba, ama RA au EL, utaingia kwenye vile vikao vya wabunge wa CCM uombe ridhaa ya kuongelea hoja hiyo Bungeni na uruhusiwe? Nape Nnauye isingekuwa huruma ya Muungwana leo hii asingekuwa mwana UVCCM wala mwana CCM, kisa aligusa tuhuma za kigogo wa CCM. Chama kimejaa untouchables (miungu watu) ambao hutakiwi kuwasema wala kwenda kinyume nao vinginevyo unaweza kufungishwa virago.

Hao wanaoitwa wapiganaji wameibuka kuinusuru CCM baada ya kuona chama kinapoteza umaarufu mbele ya wananchi. Baada ya Dr. Slaa kumwaga radhi ya LIST OF SHAME na Zitto kupeleka hoja ya Buzwagi ndipo akina Mama Kilango wakaibuka. Mama Kilango akiwa Bungeni alisema hawezi kukubali akae kimya awaachie akina Slaa na Zitto wapate umaarufu kwa kuibua kashfa na hoja nzito nzito, kisa anaogopa kushughuliwa na Chama ama serikali. Je, leo hii hao wapiganaji wanaitwaje ndani ya CCM? Hata kama una ka-doa kidogo, unaweza kujikuta unatwishwa kashfa ya mwaka 1947 ili kukunyamazisha usiseme. Ukiwauliza walikuwa wapi hawakukushughulikia, hawana jibu la kukupa.

Sasa hivi kamati ya Mzee Mwinyi inatapatapa tu, hawajui watachukua kipi waache kipi. Mama Simba tayari ameishasema ndani ya CCM hakuna aliye msafi, kwa hiyo hata yeye mwenyewe ni mchafu na JK nae ni mchafu. Kauli hiyo ina maana kubwa sana kwa wale wenye nia ya kuingia kwenye siasa.

Nikimsikia kijana anasema anakwenda kugombea Ubunge kupitia CCM ninamuona ni opportunist tu kwa kuwa kama yeye ana nia safi na dhamira njema, hawezi kwenda kujichanganya na waliovunda ama kuoza kabisa. Hivi kweli kama mtu ni msafi anaweza kwenda kukaa jalalani ama kujichanganya na wachafu? Umeambiwa kabisa hili ni jalala, ni sehemu iliyojaa takataka, bado mtu anakwenda kukaa hapo hapo. Hapo lazima ujiulize sana kama kweli mtu huyo ana nia na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi.

Hivi, ili ushinde Ubunge ni lazima upitie CCM? This is the opportune time for young men and women who wish to vie for MP posts kuingia kazini kumwaga sera za kueleweka. Unajua huu uchafu ambao CCM wanapakana sasa hivi utakuja kuwasumbua sana kuusafisha ikifika 2010, labda kwa kuwa ni mafisadi watatumia hela za ufisadi ili washinde. Lakini kama kuna mtu yuko serious na mapambano ya kweli, watanzania wa sasa wanasomesheka vizuri tu na wanaelewa. Ujinga unaoendelea ndani ya CCM ni faida kwa upinzani na wale wanaotaka kuingia kwenye siasa kupitia upinzani.

Mabadiliko ya kweli hayataletwa na hii CCM ya JK, EL na RA. Basically naweza kusema ni CCM ya RA na EL. JK ni boya tu amewekwa pale kama Mwenyekiti, lakini wenye final say ni akina EL na RA. Ndiyo maana hakuna lolote la maana linalofanyika, mikutano yao imekuwa ni kumbi za mipasho utadhani watu wako rusha roho pale Lango la Jiji.

NB: Kumradhi mwana JF ambaye ulitangaza kugombea kupitia CCM. Niliahidi kwamba ukishinda Ubunge nitaendelea kukumbusha mabandiko yako ya hapa ndani, unless na wewe upotee kama akina Dr. James Msekela ambao kwenye TANZANET walionekana wafurukutwa na walipoingia kwenye system wamemezwa na wamekuwa mute kama hawapo.
 
Sasa hivi kamati ya Mzee Mwinyi inatapatapa tu, hawajui watachukua kipi waache kipi. Mama Simba tayari ameishasema ndani ya CCM hakuna aliye msafi, kwa hiyo hata yeye mwenyewe ni mchafu na JK nae ni mchafu. Kauli hiyo ina maana kubwa sana kwa wale wenye nia ya kuingia kwenye siasa.
Maneno hayo pekee yanamwondoa ktk Uongozi.. Sielewi JK anasubiri kitu gani
 
JK alishapata kunukuu "Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi". Kwa hiyo anasubiri 2010 kama kawaida yenu mmpe ushindi wa tsunami amalizie ngwe ya pili na kuendelea kuleta "maisha bora kwa kila mtanzania".
 
Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ametema cheche na kukubali kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama iwapo itaundwa tume huru kuthibitisha yale ya tume ya Mwakiembe.:mad::mad:


Dr. Remmy na Chidumule miaka ya nyuma waliwahi kuimba "Polisi wapo, mahakama zipo, vyombo vya sheria vipo, tume za nini?"
Tunahalalisha wizi ndani ya wizi kwa kuunda tume baada ya tume.
 
Ama kweli mzee Ruksa naye alisema; Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu. Yaani hata mafisadi wanapata power ya kukoroma na kuropoka kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom