Kikao cha CCM: RA Atema Cheche "Nitajiuzulu...."

Mkandara,

Sasa RA na Sophia Simba wanaunguza na kuropoka kile ambacho si Uzushi bali mambo ya unyumba ndnai yao.

Tatizo ni kuwa kina Sitta na Mwakyembe, waliona haya na kuamua kuinusuru Serikali na Chama AIBU na sasa kinawalipukia!

They are practically done unless wanaondoka CCM!

-------------------------------
Narudia tena, UPUUZI wa wapiganaji wa CCM ni kuangalia maslahi yao na si Maslahi ya Taifa na jinsi watakavyoangamia, hakuna atakayeamini kuwa walikuwa wakipigania maslahi ya Taifa.

Mchungaji hivi leo umesali sala ya hasubuhi? naona unachanganya!!
 
Yaani jamani hawa watu wanatufanya sisi matahira sana. Hakuna haja ya kuunda TUME Lowassa alijiudhuru kwasababu aliona amekosa, hakuna haja ya kuendelea na hii mijadala serikali ijipange upya ianze kutupatia maisha bora kwa kila mtanzania.

Rostam anatuona kama vile watanzania hatuna akili kabisaaaaa, aondoke zake huko. Kama kujiudhuru aendelee tu, kwani naye ni FISADI MKUBWAAA, ana bahati uongozi wetu wa leo ni nyanya.

Watanzania tusikubali kuundwa kwa TUME mpya eti kuchunguza iliyosema TUME YA MWAKIEMBE kama ni kweli, uiiiii WIZI MTUPU!!!!, Mbona haikuundwa TUME kuchunguza kwa nini HOSEA alisema uongo?? alibeba mkoba wake kututolea report ya uongo, mbona mpaka leo haijundwa TUME.

Rostam please give us break.
 
RA is still the Don! sitta na wenzake wapo katika hatari kubwa sana ya kuondoshwa kwenye nafasi zao kwenye uchaguzi ujao. sio kama nitajali, kwa sababu sitta hana upiganaji wa mali za mwananchi, ana ganga njaa tu.
 
Rev. Kishoka,

Mkuu twende mbele turudi nyuma kidogo..

Hivi mnawafikiria CCM wajinga kiasi gani vile.. Yaani hawa wapiganaji kama sii lolote sii chochote iweje hili swala la Richmond limewakuna Mafisadi kiasi hicho.. imefikia hata watu kutukanana matusi ya nguoni, kumbuka ugonvi wa mkutano wa Kamati kuu ya chama, lugha zilizotoikea pale..Leo hii wewe mkuu wangu unazungumza LUGHA ya Sophia Simba, wewe mchungaji unakubaliana na kina Sophia kwamba hata kina Sitta ni mafisadi ktk utetezi wa mtu Fisadi..

Mkuu wangu yawezekan Sitta fisadi lakini kesi moja baada ya nyingine, Marekani walikwenda Afghanstan kwa sababu ya 9/11 na dunia tulikuwa nyuma yao, sasa kama tungeanza kusema marekani nao ni Materrorist size yao kweli hali ya maisha yetu Ulaya ingekuwa hivi..Sote kwa ujumla tulilaaani terrorism kwa sababu sote tulikuwa hatarini na kama tungeshangilia hayo matokeo yake kina Osama wangepiga miji yote ya Marekani na nchi zote za Ulaya kwa sababu sisi tumewapa nguvu.

Ndicho mnachokifanya hapa..mnashindwa ku take a stand badala yake mnakumbwa ktk kiza kinene cha mbinu za mafisadi.. Ikiwa Mwakyembe na Sitta ni mafisadi kwa nini kesi zao hazifikishwi bungeni au mahakamani... Kama iliwezekana kuchukuza BoT, EPA, Richmond na mashirika mengine iweje shida kuwafikisha mahakamani watu hawa badala yake zinapigwa simu za kuhoji wabunge na posho zao.

Of all Ufisadi jamani posho imekuwa kitu cha kujibu mapigo!

Mkuu wangu Uhasibu nimeufanya na naelewa wazi kabisa malipo yoyote yale ya serikali yanapitishwa vipi..Mbunge hawezi kuilazimisha wizara kutoa posho isipokuwa serikali yenyewe iliweka posho hizo ktk kifungu cha matumizi toka mwanzo, besides kuchukua posho mbili sioi crime hata kidogo maadam invoice na cheki vimepitishwa kisheria na maofisa wanaotakiwa kupitisha. sana sana mbunge huyoi atatakiwa kurudisha fedha alizopewa zaidi, kama hana atakatwa ktk mshahara au posho zijazo lakini posho mbili sio swala la RUSHWA hata kidogo kwani lipo ktk kifungu cha matumizi ya wizara, shirika au taasisi. Kama kuna kukamata mtu basi yule aliyepitisha matumizi hayo ndiye wa kushinkwa koo..

Pili, hapakuwa na sababu kabisa ya Hosea kwenda Bungeni wakati wa bunge ati kumwona Spika..Mkuu wangu, vita hii isingekuwa kubwa hivi kama kweli hawa wote lao ni moja..
 
Nilifurahia kapata upinzani jimboni kwake kumbe mganga wa kienyeji?

.Huyo ni mpinzani boya, au boshen under the sama pay roll ili kusijetokea serious contender. Katika majimbo yote ya Tabora, ni Igunga peke yake ndio CCM imeshinda kwa asilimia 100 katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Kwa maoni yangu, njaa, dhiki na umasikini uliokithiri, its easy to buy them out.Kitendo cha CCM kushinda kwa asilimia 100% Igunga, ni uthibitisho kuwa ni king maker who is mightier in Tabora, and its you never know what money can do kwa masikini wa Urambo, wasije kuwa kama wale wa Busanda na Biharamulo, msijeshangaa Six akang'oka.
 
The next step wataleta hoja ya ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika; Sitta ataondoshwa (kwani wabunge kadhaa watapangiwa visema kule nje na kura itapigwa). Akiondoshwa atawekwa Spika wao (jina tunalo) ambaye ataridhia maombi ya kina RA na Sofia. Ndipo tume wataiunda wao na kina RA na EL watasafishwa rasmi kwa kutumia utaratibu wa kibunge na hivyo maamuzi kuwa legally binding.

Tayari kwa karibu wiki kadhaa sasa pesa imetembea Dodoma kwa ajili ya jambo hili na kwa ajili ya kupata support ya wabunge. Novemba 7 ni siku muhimu kwa ajili ya hili.
 
Tayari kwa karibu wiki kadhaa sasa pesa imetembea Dodoma kwa ajili ya jambo hili na kwa ajili ya kupata support ya wabunge. Novemba 7 ni siku muhimu kwa ajili ya hili.

Kwa mtaji huu CCM wanako elekea ni kuuza nchi kama pesa ina nguvu kiasi hiki mpaka wabunge walio chaguliwa na wananchi kihalali wanakubali kununuliwa kwa fedha za kifisadi basi tunako elekea tutaanza kuchapata makonde.
 
Mmmh jamani Tanzania tumekuwaje?

Kila kitu mpaka tume,tume juu ya tume. Kila mtu akituhumiwa mpaka tume,hata akiwa na makosa ya wazi mpaka aundiwe tume, jamani! Mbona Mzee Mwinyi mwaka 1976 hakusubiri tume? Kila kitu tume, hata mtoto wa Mwinyi alishindwa kumuiga baba yake kwenye mkasa wamabomu ya mbagara kuwa mpaka tume imhakikishie kuwa kuna uzembe.

Hivi mabomu kulipuka bila kulipuliwa si uzembe? Sasa Rostam nae anataka aundiwe tume, kwani yeye ni nani? Neno uwajibikaji liondolewe kwenye kamusi ya kiswahili au lipewe maana nyingine kabisa si hii tunayoijua.

Mungu atusaidie nchi imeuzwa! Si mmajua msemo wa "ina wenyewe na wenyewe ndio sisi? (mimi na wewe hatumo!)
 
Hawawezi kuubadili UONGOZI wa BUNGE angalau kwa sasa. Uzuri ni mmoja kwenye uongozi wa mhimili huu; SPIKA anachaguliwa, hateuliwi mbali na uteuzi ule wa awali wa chama chake ambao kwa sasa hauwezekani pia kufanyika.
Acheni CCM wanyukane kwanza. Wanayemharibia kwa sasa ni JK. Anaonekana Uraisi hauwezi na Uenyekiti wa chama chake pia umemshinda.
 
Iko siku ambapo Watanzania wataamka na watakuta kwamba Chama cha Mapinduzi hakishiki tena hatamu za uongozi wa nchi, na badala yake Ikulu na Bunge vimechukuliwa na chama kingine. Siku hiyo ambayo haina jina, itakuwa ni siku ambapo Chama cha Mapinduzi kitaanguka kwa kishindo kikuu na sauti ya kuanguka kwake itasikika kila kona ya Tanzania, na mwangwi wa kuporomoka kwake kurindima katika bara letu la Afrika na mabaki ya mtetemo wa kuvunjikavunjika kwake kusimuliwa kama hadithi za Alfu Leyla wa Uleyla kwa vizazi vijavyo vya Watanzania. Kuanguka kwa Chama cha Mapinduzi kutakuwa ni mwanzo wa msemo, na bila ya shaka kutatungiwa methali.

 
Janja yao kusogeza mbele mjadala huu, ili waendelee kutafuna kodi zetu. Kwanza kuhusu chuki binafsi kati ya Six na EL-Unathibitishaje hili? Halafu mmemsoma Sophia Simba kwenye Mwananchi? Yaani, mambo ya uswahiiiiiili!
******************Kweli Tanzania haina viongozi!********************
 
Pale Dodoma wabunge wamemwambia mzee Ruksa na kamati yake kuwa amwambie muungwana kuwa ugomvi wote na mpasuko utaisha mara moja wakiondoka kwenye uongozi/ccm lile gruop of 4, RA, El, VjiCent na Mzee wa Tics. Na wameonyesha ni wakali kweli kwenye hilo, I hope hawatarudi nyuma, maana wakishindwa kwenye hilo, wamejimaliza.
 
kama mahesabu ni ya kumbadili spika, trsut me, wanajiandaa kufail tena kama walivyofanya mara nyingi huko nyuma. mambo yamebadilika sana na move ya aina hiyo itamnufaisha zaidi spika kuliko mahasimu wake.Ila ngoja tuone mambo yataishia wapi. CCM sasa wako katika vita ambavyo ni lazima wema uushinde uovu.Vinginevyo tutaendelea kuongozwa na wababaishaji mpaka mwisho wa safari
 
The next step wataleta hoja ya ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika; Sitta ataondoshwa (kwani wabunge kadhaa watapangiwa visema kule nje na kura itapigwa). Akiondoshwa atawekwa Spika wao (jina tunalo) ambaye ataridhia maombi ya kina RA na Sofia. Ndipo tume wataiunda wao na kina RA na EL watasafishwa rasmi kwa kutumia utaratibu wa kibunge na hivyo maamuzi kuwa legally binding.

Tayari kwa karibu wiki kadhaa sasa pesa imetembea Dodoma kwa ajili ya jambo hili na kwa ajili ya kupata support ya wabunge. Novemba 7 ni siku muhimu kwa ajili ya hili.
Mkjj naona unaililiaa CCM.. Si vibaya kwani wameshika dola kwa sasa.

Sina tatizo lolote na RA, EL, au Sophia Simba kwani hawa wote wanapigania masilahi ya CCM kwa faida yao..

Hilo la Nov 7 natamani na ningeshukuru litimie ili demokrasia mpya ifungukee.
 
The next step wataleta hoja ya ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika; Sitta ataondoshwa (kwani wabunge kadhaa watapangiwa visema kule nje na kura itapigwa). Akiondoshwa atawekwa Spika wao (jina tunalo) ambaye ataridhia maombi ya kina RA na Sofia. Ndipo tume wataiunda wao na kina RA na EL watasafishwa rasmi kwa kutumia utaratibu wa kibunge na hivyo maamuzi kuwa legally binding.

Tayari kwa karibu wiki kadhaa sasa pesa imetembea Dodoma kwa ajili ya jambo hili na kwa ajili ya kupata support ya wabunge. Novemba 7 ni siku muhimu kwa ajili ya hili.
Mkjj naona unaililiaa CCM.. Si vibaya kwani wameshika dola kwa sasa.

Sina tatizo lolote na RA, EL, au Sophia Simba kwani hawa wote wanapigania masilahi ya CCM kwa faida yao..

Hilo la Nov 7 natamani na ningeshukuru litimie ili demokrasia mpya ifungukee.
 
kazi ipo sololo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mzee six upo mpe maneno magumu huyo mhabeshi kwanza si raia wa tz, ana kivuli cha jeikei huyo lakini nchi ni ya watanzania wote
 
Kwa mtaji huu CCM wanako elekea ni kuuza nchi kama pesa ina nguvu kiasi hiki mpaka wabunge walio chaguliwa na wananchi kihalali wanakubali kununuliwa kwa fedha za kifisadi basi tunako elekea tutaanza kuchapata makonde.

nchi imeshauzwa..ipo mikononi mwa RA na jopo lake, hata Kikwete na tabasamu lake hafurukuti..

wabunge nao waliochaguliwa 'kihalali' ni wachache, wengi wamemwaga pesa ili kufika hapo walipo, ndiyo maana ni rahisi kununuliwa na mafisadi..

kwa hali hii kuchapana makonde huko mbele haitakuwa jambo la kushangaza..
 
Mkandara,

Wakati wa Uchaguzi wa 2005, pesa chafu ya EPA ndio iliyoirudisha CCM Madarakani, ingawa wala hawakuhitaji kuchota.


Uchaguzi wa 2000, pesa za Meremeta na upuuzi mwingine zilitumika vizuri sana maana kulikuwa na kutokuaminiana ndani ya Chama na ngao ya CCM Mwalimu Nyerere alikuwa katutoka

Uchaguzi wa 1995, pamoja na pesa zote zilizokwisha chukuliwa kisanii na CCM, ilibidi wamkimbilie Nyerere ambaye single handedly aliwaangusha Mrema na wenzake wa Muungano na kutumia fimbo ya matakoni kumrudisha Salmin.

CCM ni chama si cha kuaminiwa na wewe unalijua hilo. KInachotokea sasa hivi ni ugomvi wa nani ashike hatamu na kula utamu kwa kutumia CCM na wala si kuhusiana na maslahi ya Taifa.

Waziri wa Usalama wa Taifa anapota kauli kuwa kila mtu ni safi kuhusu RICHMOND na RADA, je unafikiri ni nani aliyetoa baraka kwa kauli kama hiyo kutolewa?

Lowassa, Rostam, Sitta, Mwakyembe na wengineo wana madhambi yao, na tatizo limekuja sasa hivi ni mapiku!

Kama kina Sitta na Wapiganaji wangesikiliza lile tulilowaambia la kutetea maslahi ya Taifa na kufanya kazi kwa manufaa ya Taifa, fedheha kama hii isingetokea na kina Lowassa, Rostam na Sophia wasingediriki kufanya wanalolifanya leo hii!

Kwa miaka mitatu tumekaa tukizungumzia tuhuma kuhusu Rostam na Lowassa, je wameshakalishwa kitako ndani ya Chama au Serikalini na wakachukuliwa hatua?

Je Chenge naye ambaye ni mkuu wa Maadili ndani ya Chama ni lini amekalishwa kitako akaambiwa ajieleze?

Juzi suala la Richmond limegeuzwa kuwa ZeComedy, kina Sitta wanabanwa Golori zao kuttokana na kupenda posho, kina Ngwiliza wanafunuliwa kwa kupata pensheni mbili mbili, huku Richmond, Kagoda, EPA, Rada na sasa Kilimo Kwanza wanapeta na tunadanganywa kuwa ni kukua kwa Demokrasia ndani ya Chama!

Huu ni uhaini wa hali ya juu, na Watanzania tunachezewa akili, tunafujiwa hazina yetu na tunafanywa wapumbavu!

Nilihoji kwa nini Wapiganaji hawajiondoi na UCCM na kupigania mambo ya Taifa? Kwa nini wanaendelea kuogopa panga na rungu la Chama kwa kuendelea kuimba CCM mbele, Tanzania nyuma kam Wakristo wanavyoimba Msalaba Mbele Dunia nyuma?

Kwao Wapiganaji wa CCM, wokovu wao(binafsi) ni kupitia CCM na si kupitia Taifa la Tanzania!

Ni upuuzi kuendelea kuwasikiliza! Kwanza afadhali na tunajua kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni Mafisadi na hilo kila Mtanzania analijua na usishangae kuwa mwakani, viti vyote vya Ubunge Dar vitakwenda CCM na zaidi CCM inaweza kupunguza nusu ya viti vya Upinzani hasa Bara.

Lakini kwa kuwa ni jadi ya kuoneana aibu ndani ya Chama, kina Sitta wamepoteza nafasi moja kubwa sana, walipoleta ripoti ya Richmond wakadai kuna mambo mengine hawatayazungumza ili kuifichia aibu Serikali, hapo ndipo walipouza utu wao na wakapoteza sifa ya kuwa wapiganaji na hata maana ya kuwa na tume.

Kuondoka kwa Lowassa hakukutosha, ilipaswa ripoti ilete mabadiliko ya kweli si ya watu kujiuzulu tuu!

Kama wasingeficha baadhi ya mambo eti kuionea aibu Serikali, leo hii kila lililoovu lingeanza kuweweseka na kuogopa. Lakini midhali waliamua kufukia maovu na uzembe mwingine kwa kuonea huruma na aibu Chama na Serikali, basi ni vigumu sana kwa mabadiliko na vita dhhidi ya uhujumu, uzembe na kutofuata kanuni kufanikiwa.

Lakini swali langu na lile la Mwanakijiji linarudi, Wapiganaji wanapigania nini na wanampigania nani?

Ukiona Sophia na Rostam wanatamba kama walivyofanya sasa hivi, jiulize Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo wapi na yupo upande gani?
 
Posho ya Mzee Mwinyi, Msekwa na Kinana ni kiasi gani kwa siku kwa kazi hii ambayo haitakuwa na TIJA? Ni nini ambacho CCM hawakijui kinachotafutwa hapa? Ruzuku inayochotwa na CCM kutoka hazina yetu ndio inayogharamia ujinga huu?
 
Back
Top Bottom