Kiingereza cha Mlimani City

Kiingereza cha Mlimani City

Hi!, Hey! Hallo! How are you! ndio salamu za mlimani city. Huwezi sikia mambo, poa! utaonekana ndio umeshuka.
 
nimewai kuitwa "My wangu" pale mlimani city,mtoto nilitoka nae Mwanagati
 
Jamani kwa nini kila mtu akikanyaga tu lango la kuingilia Mlimani City anaanza kuongea kiingereza? Utasikia cha kuungaunga mara IS na WAS kibao. Kwani mkiongea Kiswahili chenu mtakuwaje? Acheni uzuzu, ubitozi na usister duu!

Kama wamewekeza kwenye Kiingereza wana uhuru wa kukitumia bila kuingiliwa na mtu. "After all," ngoja na mimi nichanganye, "Kiingereza ni lugha rasimi Tanzania."
 
Sisi wengine huwa tunapita hapo kupigwa kiyoyozi kabla ya kuendelea na safari ya kurejea makwetu...
Mkuu Nimecheka kwa sauti, kama nakuona hivi unavyozuga kushangaa bidhaa kumbe unakula kiyoyozi.
 
Sanasana wasichana wa vyuo ndo wana hizo swaga za kuongea kiingereza
 
vitu vingine huwa vinashangaza na kuchekesha sana wabongo bwana!!!!!
 
Yesterday kibao na kiingereza chenyewe sasa mwe utasikia SNAKE THIS WAY (nyooka na njia hii) au UR THEIR HIPOPPOTAMUS (Wewe ni kiboko yao) nifollow instagram walking lollipop
 
Last edited by a moderator:
kweli mkuu kuna wengine wanatembea na oxford dictionary
.kaka mi naomba kuuliza hivi mlimani city unaingia na cheti ulichosomea inglish kozi?maana si wengine ni wa umande jumla.hatujui mayai.tunaruhusiwa kuja?
 
Yesterday kibao na kiingereza chenyewe sasa mwe utasikia SNAKE THIS WAY (nyooka na njia hii) au UR THEIR HIPOPPOTAMUS (Wewe ni kiboko yao) nifollow instagram walking lollipop

Hahaha! umenikumbusha mbali kuna siku tulikuwa class form 4 tukiwa darasani nje kulikuwa na hali ya hewa ya mvua jamaa mmoja akaropoka "The rain is coming down" Na darasana kulikuwa na mwalimu du jamaa mbona alichezea za kumtosha!
 
Last edited by a moderator:
Yesterday kibao na kiingereza chenyewe sasa mwe utasikia SNAKE THIS WAY (nyooka na njia hii) au UR THEIR HIPOPPOTAMUS (Wewe ni kiboko yao) nifollow instagram walking lollipop

aaaaaah! mkuu hapo umeua
 
Last edited by a moderator:
.kaka mi naomba kuuliza hivi mlimani city unaingia na cheti ulichosomea inglish kozi?maana si wengine ni wa umande jumla.hatujui mayai.tunaruhusiwa kuja?

mkuu mlimani city unaingia na cheti cha english course,kadi ya kupigia kura,barua ya mjumbe,na pasport size 2
 
Hata Mimi wa nyakitonto kasulu kigoma naweza kupanda hadhi kwa kutema yai doyunoworamsei
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom