Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Kwa nini huyo Dokta toka Kenya asiwepo wakati watakapokuwa wanafanya hiyo Autospy akiwa kama member wa familia ? Pia nilikuwa nauliza jee kama Familia ikiamua kuchukua baadhi ya samples kama tissues for further analysis kwenye private laboratories wanazozijua wao ...jee hilo nalo wataruhusiwa kwa sheria za Tanzania?
 
Sibishani ila nilikuwa najibu swali lako la kwanza na kukupa facts, kama ulikosea kuliuliza kiri kwani muungwana ni vitendo.

Nashukuru.

Kiranja,

Lengo langu pekee la kuchangia ni kuelemishana. Kuwa na ofisi Dar na kuendesha case mahakamani ni vitu viwili tofauti. Kuniambia ana ofisi jengo fulani kwenye hili hoja si issue maana suala tunaloongelea ni kuendesha cases mahakamani.

I hope umeelewa na kama una uhakika na unachosema basi wapelekee chama cha sheria, sijui wanaitwaje ili hao wahusika wachukuliwe hatua.

Hao Wazungu kitu cha kwanza wanachofanya wanapokuja kwetu ni kusoma sheria zetu, wengi wao wanazifuata na kupata vibali hata kama ni kwa rushwa. Usitegemee wakili wa mtu controversial kama Chenge afanye kazi TZ bila kibali.
 
Tatizo kuna nia njema ya kutaka kuujua ukweli kwenye hili? TBC walipaswa sasa na wao kupatwa na wasiwasi kwani wanatumika na hii itamaliza credibility yao ambayo wameanza kujijengea hapa nchini.

Daktari hajapatikana so far ,ila kwa taarifa ni kuwa ujumbe mzito umeelekeza kuwa ni lazima azikwe leo.

Sasa ni nani hasa ambaye ametuma huo ujumbe mzito kwamba ni lazima azikwe leo...

Mbona sasa vichwa vinazidi kuuma?
 
Bongolander,

Mambo ya fire siyajui kwahiyo siwezi ku comment.

Mambo ya accounts hii inafanya kazi dunia nzima. Hata kampuni ya Tanzania inaweza kufanya kazi mahali popote baada ya kutimiza sheria za nchi husika.

Una uhakika gani hao waliochunguza mahesabu ya EPA hawajasajiliwa Tanzania? Kwanza aliyechunguza ni mtanzania na ana ofisi TZ. Huenda E&Y wamesajiliwa TZ pia.

Hata hao madaktari wa macho na magonjwa mengine huwa wanapata vibali kabla ya kuruhusiwa. Huwa hawashuki tu airport na kuanza kutibu watu.

Kuna mambo mengi sana yanafanyika chini chini, huwezi kujua mpaka kama kuna tatizo.

Mara nyingi hata kama kampuni haina usajili ndani ya nchi, ikipata tender, kazi ya kwanza ni kuanza usajili na kupata vibali vingine.

Wote tumelalamikia hapa kuhusu ile kampuni ya Norway kufanya kazi TZ bila usajili. Leo
tunapinga kukatazwa kwa daktari ambaye hajasajiliwa Tanzania.



Nadhani tunahitaji watu waliokuwa na uelewa kama wako ili tuweze kujikwamua hapa tulipo. Tangu nimeanza kufuatilia michango yako hapa JF, mara zote uko makini na haufuati upepo.

Hili ndilo tatizo letu sisi wananchi na viongozi wetu. Ubinafsi, ubinasi, ubinafsi!!
 
Hamuwatendei haki TBC1 hata kidogo... nadhani hata ninyi mnaoandika mnajua hilo.

Kuna mambo yanafanyika na hata baadhi ya wafanyakazi na waandishi wa TBC hawakubaliani nayo na ndio maana wanasemwa kwani wanafanya kazi nje ya proffession yao.....kuna nguvu za ziada ,subiri kidogo utaona mtikisiko mkubwa humo ndani ya TBC1.

Jiulize mkataba wao na Bunge ambao ulikuwa ni kurusha matangazo live.
 
WanaJF

Hiki ni kitu ambacho hakijatokea katika mazishi ya viongozi wa nchi hii-wananchi kutaka uchunguzi zaidi kwa mwakilishi wao. huenda ndio maana TBC wamekipa umuhimu.

Hichi kifo cha wangwe kina utata mno, nawasifu ndugu wa marehemu kutaka uchunguzi zaidi, hili ni fundisho na mwanzo wa mambo mapya katika tawala za kitanzania. Hapa hamna kufunika kombe mwanaharamu apite,mpaka kieleweke.......
 
kumzuwia daktari kutoka kenya ni jambo la haki kwa serikali, lakini kwa nini mwanzo watoe ruhusa kisha waseme haiwezekani? ni upotezaji wa muda wa watu ...hasa kwenye kitu kinachohusisha maiti!

nafikiri TBC1 wanafanya kazi nzuri.........yaani wasingerusha live ingelikuwa wamedharau suala hili nyeti. the only problem ni kuwa TBC1 ina uwezo wa kurusha live kitu kimoja tu. lakini ingelikuwa wanawweza wangerusha bunge live, kisha wakatuunganishia na kwa tarime.
 
Hii serikali imeamua kufanya vita dhidi ya watu wake yenyewe na hii inatupeleka kujiuliza maswali lukuki:
Tutaiaminije tena Serikali yetu?
Serikali yetu ni kwa manufaa ya nani?
Serikali inaficha nini?

Jana usiku saa 2 nimesikiliza taarifa ya habari TBC, ikanishangaza na kunisikitisha sana! Katika Taarifa hiyo ya saa usiku TBC kiaina wameihusihsa CHADEMA na kifo cha Chacha Wange; wamedai kuwa TBC imepata ushahidi wa Makabrasha aliyokuwa nayop Marehemu kuwa alikuwa akienda Dar es Salaam kuifungulia kesi CHADEMA na angefanya Press conference baada ya kufungua kesi hiyo na kuwa kuna taarifa kuwa Viongozi wa CHADEMA walikuwa wanafahamu hilo (Marehemu alikuwa anaenda kuwafungulia kesi).

Kwa kweli walinikwaza sana, badala ya kuhimiza uchunguzi huru kuhusu kifo cha Wangwe TBC (Serikali?) Wanahusisha kifo cha Wangwe na kesi dhidi ya Viongozi wa CHADEMA. Veery Shaaaame kwa chombo cha habari cha Serikali kutangaza kitu cha namana hiyo. AIBU TUPU!

Kuhusu Daktari wa familia kukataliwa kufanya postmortem hapo Serikali inajipalia makaa ya moto ambao itashindwa kuuzima kama ilivyowashindwa Walenchoka na Waanchali wa huko huko Tarime. Hawa jamaa wanaweza kuweka kando tofauti zao na kusimama kidete dhidi ya Serikali.

Ushauri wangu ni kuwa Familia ya Wangwe ichukue maiti wao na kuipeleka Kenya kisha waiombe Serikali itume Daktari wake huko aungane pamoja na DEaktari wa Familia kwa uchuinguzi au vinginevyo Waende Mahakamani ili Mahakama iiamuru Serikali iruhusu Famiilia itafute Daktari wake kuuchunguza mwili wa Marehemu
 
kumzuwia daktari kutoka kenya ni jambo la haki kwa serikali, lakini kwa nini mwanzo watoe ruhusa kisha waseme haiwezekani? ni upotezaji wa muda wa watu ...hasa kwenye kitu kinachohusisha maiti!

nafikiri TBC1 wanafanya kazi nzuri.........yaani wasingerusha live ingelikuwa wamedharau suala hili nyeti. the only problem ni kuwa TBC1 ina uwezo wa kurusha live kitu kimoja tu. lakini ingelikuwa wanawweza wangerusha bunge live, kisha wakatuunganishia na kwa tarime.


Serikali iliridhia uchunguzi huru; la daktari kutoka Kenya, nahisi ni taratibu tu za kawaida ingetakiwa zifuatwe na siyo kukurupuka kama ilivyo sasa.

Hili jambo linakuwa na utata kwa kuwa watu wanaolishughulikia wanazongwa na nguvu pingamizi nyuma yao. Kwa hiyo, siyo kwa matakwa yao, bali ya wengine kabisa.
 
kwa nini nguvu nyingi sana inatumika katika jambo lenye suluhisho rahisi? au ndio njia ya kutupotezea muda kujadili mafisadi and the likes?
 
mmmmmmmmmmmmmmmmmmmh Arufu ya uozo!!!!

Hivi mnamkumbuka kulikuwa na daktari mmoja bingwa pale Muhimbili sasa hivi amestaafu nadhani alikuwa bingwa kwa masuala ya autospy nakumbuka nasikia alikuwa muda mwingi amelewa na Mwalimu JK alimfuata na Jamaa akamchukuaNyerere mpaka chumba cha upasuaji na kuvuta maiti akapasua alafu akachukua andazi akang'ata. (Nadhani hii ilikuwa story tu kama za "K funika kikombe") lakini ninachotaka kusema hapa ni kuwa kama yule Daktari bado yupo atafutwe huyo, yule jamaa nilimwona siku moja anafanya Interview na ITV (2001) alikuwa very good, sijui kwa sasa kama bado anapractice atakuwa msaada sana ni out spoken, akificha leo atakuja sema siku nyingine, haogopi. Nimesahau Jina lake lakini nahisi lazima kuwe na mtu hapa anahabari zake, tafadhari msaada.
 
Wakati Marehemu Chacha Wangwe alipotofautiana na Mwenyekiti wake na hadi kufikia kusimamishwa umakamu Mwenyekiti, wengi wa wachangiaji katika Thread hii tuliyomo mli-mlima sana Wangwe na kufikia hadi kumtakia afe, ikibidi kwa kupigwa risasi.

Leo hii bado mnajitahidi ku-speculate na hata kubadilisha taarifa halisi ya tukio zima lililotokea kule Tarime, kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA alitaka kuvamiwa na watu wenye hasira kali ambao wanamtuhumu juu ya kifo cha Wangwe. Kuna ambao wanajitahidi ku-twist zaidi mtiririko wa thread hii kwa ajili ya manufaa ya mtu binafsi au kundi fulani, si vibaya kwani mnalolifanya mnalielewa vizuri. Lakini mwisho ya yote ni kuwa mnasherehekea ushindi mlioupata wa kuona kuwa sasa Wangwe mlilokuwa mnamtakia limekwishamfika, Sioni sababu ya kutaka KUMSAFISHA MTU ambaye hata kutuhumiwa bado hajatuhumiwa, au kushinikiza yale mnayoyataka ninyi dhidi ya Deus bila ya kujali haki zake za kimsingi na sheria zinazomlinda hadi sasa.

Endeleeni ku-speculate kama mnadhani hiyo ndiyo njia sahihi ya kubadilisha matokeo halisi
 
niliandika jana kuwa kimbelembele cha wanasiasa kutumia msiba kukuza au kujipatia umaarufu kutaligharimu taifa

1 tbc wako musoma kujaribu kupotosha taifa kuwa chadema ndo wauaji wa wangwe kwa mantiki kuwa chadema itasambaratika na ufisadi utarudi kwa kasi

2. kwa kufanya hivyo tayari wananchi wa tarime wana hasira nan chadema na wachagaa, na tayari maduka ya wenzetu hawa tangu jana hayajafunguliwa, manake serikali inachochochea ukabila

3.kam tbc hawafanyi hayo hapo juu, huenda wanalipa fadhila kwa marehemu, fadhila ambazo wao na serikali wanazijua zaidi

hili ni taifa la watu ambao ukifikiri sana, utashangaa vichwa vyao viko chini ya mabega au juu ya mabega.

haiwezekani mtu apigwe risasi halafu gari lake liwe involve kwenye accident fake halafu liumie kiasi kile. labda liwe ni gari feki na wala siyo lile alilokuwamo wangwe

jibu ni rahisi, wangwe alikufa kwenye ajali iliyosababishwa na kuendeshwa na dereva asiye mzoefu bwana mallya
 
pROF. hAJAFA
Hajafa nani? Profesa Shaba? Nimesoma somewhere kuwa ameshakufa. Nilishangaa maana sijawahi sikia hata siku moja. Nilipata habari tu kuwa mwane Hamish amefariki. Baba mtu bado. Hebu eleza zaidi.
 
Kifo cha Wangwe ni tukio halisi na la kusikitisha sana. Japo wote linatugusa kwa namna moja au nyingine ni tuko katika makundi tofauti.
Nashauri kwamba kwa sababu hii si habari ya kufikirika, ni vema tuandike taarifa halisi ili wale tunaofuatilia tupate hizo taarifa badala ya kulibadili kama suala la mjadala wa kuweka hisia zetu na nadharia ambazo hazipo; wakati mwingine tofauti kabisa na ukweli wenyewe.
Napendekeza wale wenye habari/taarifa halisi na za kweli toka Tarime watujulishe. Kama huna taarifa ni vizuri kusoma tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom