Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Mchongoma,
Kumbe Prof. Ameshafariki? Nilikuwa sijapata hizi habari. RIP Prof.Shaba. Nafikiri kifo chake kweli kilichangiwa na vitu vingi si pombe tu. Kwanza nasikia alilia sana kwenye msiba wa prof. Makene akisema wazi kabisa "Wamemuacha peke yake, wote rafiki zake wametangulia..". Ilikuwa inaonekana kabisa kama Mzee kakata tamaa kuwa na yeye inabidi awafuate RAFIKI ZAKE. Na sijui msiba wa mwanae Dr. aliuhimili vipi. Au ni baba alitangulia? Kwa mtoto na mwanae ilikuwa pengo kubwa kwa taifa.

...Ohooo, kumradhi yakhe, isijekuwa nami nishachanganya madawa hapa, ...mwanae gani unamzungumzia, Hamish? ..will be back with an accurate info.
 
Ni wakili gani wa Chenge anayetoka nje ya TZ ambaye anamwakilisha Chenge TZ?

Ni daktari gani wa nje ambaye anatibu wagonjwa TZ bila kusajiliwa?

Ni Engineer gani wa nje ambaye anajenga nyumba TZ bila kusajiliwa?

Kama kuna yeyote anafanya hayo hapo juu, anavunja sheria, unaweza kumpeleka polisi.

Cases za majanga zinashughulikiwa na sheria tofauti. Hata red cross wana wanasheria wao wanaowasaidia juu ya namna ya ku operate kwenye nchi mbalimbali.

Mwanasheria wa Chenge anatoka Marekani na anaitwa John Lewisy Madorsky, anapatikana jengo la kitega uchumi floor ya Tano.
 
Tatizo kuna nia njema ya kutaka kuujua ukweli kwenye hili? TBC walipaswa sasa na wao kupatwa na wasiwasi kwani wanatumika na hii itamaliza credibility yao ambayo wameanza kujijengea hapa nchini.

Daktari hajapatikana so far ,ila kwa taarifa ni kuwa ujumbe mzito umeelekeza kuwa ni lazima azikwe leo.
 
Mwanasheria wa Chenge anatoka Marekani na anaitwa John Lewisy Madorsky, anapatikana jengo la kitega uchumi floor ya Tano.

Mkuu,

Si kweli, huyo mwansheria ana partners Watanzania ambao ndio wanaenda mahakamani kuendesha case, yeye anaweza tu akawa anawashauri. Huwezi kwenda kuendesha case
kwenye mahakama za TZ kama hajasajiliwa hapo nyumbani.

Aidha, mpaka sasa Chenge hana case yoyote Tanzania, huyo mwansheria wake anamwakilisha huku nje kule alikoficha vijisenti vyake. Huyo lawyer mwenyewe alitamba kwamba amesajiliwa kufanya kazi kwenye hiyo nchi.
 
...Ohooo, kumradhi yakhe, isijekuwa nami nishachanganya madawa hapa, ...mwanae gani unamzungumzia, Hamish? ..will be back with an accurate info.

Usikute na mimi nimechanganya.Alikuwa mzungu siyo?maana haya majina yana utata!
 
Kichuguu,

Vifo mahali popote ni very controversial hasa vitokanavyo na ajali. Ndio maana anayetakiwa kutoa maamuzi juu ya kifo kimetokana na nini lazima awe na authority fulani kwenye nchi husika.

Ukiruhusu mtu yeyote, ataletwa dr. kutoka sehemu na kusema jambo ambalo si ajabu halina ukweli. Kasheshe itakayotokea hapo hakuna anayejua. Baada ya hapo utamkuta wapi huyo daktari mpaka umshitaki kwa kuzua? Imagine ile case ya Diana angekuja daktari mwingine toka nje akasema dereva hakulewa? Kasheshe ambayo ingetokea hapo, hakuna anayejua.

Daktari waliosajiliwa kwenye nchi, wanabanwa na sheria za nchi. Kama ametoa uchunguzi fake, hushitakiwa na mabaraza ya madaktari na pia vyombo vya dola. Huyo Mkenya Tanzania tutaenda kumkuta wapi kama amevurunda kwenye taarifa yake?

Hiyo sheria ina make sense na ndio maana karibu kila nchi inayo. Hivi kweli madaktari wote wa TZ hatuwezi kupata daktari ambaye anaweza kuchunguza na kusema ukweli? Mbona kifo cha risasi ni rahisi mno kugundua?

Mtanzania, ilikuwaje fire departement toka uingereza walikuja kufanya uchunguzi wa ajali ya moto shauritanga, ilikuwaje wakaguzi wa hesabu kutoka nje wakaja kukagua mahesabu ya Tanzania, kwani hawa hawakuwa na uwezo wa kuleta habari za uongo na kutimua? Kama hicho ni kisingizio cha kuficha ukweli hakifai.
I am sure at the end damu ya Wangwe itakwenda na maji, itasemwa for the sake of something we do not know let us put this aside. Nadhani kuna thread moja nili-predict kuwa tusubiri series ya vifo vya watu and that is where we are.
 
Tanzania huwa wanapata madaktari kutoka nje kuja kufanya clinics hapa nchini. Kwa mfano eye clinics na nadhani pia walwahi kuja heart specailists kufanya operations/matibabu THI. Pia Maj Gen Kombe alifanyiwa indepedent post mortem na Dr toka nje. (alikuwa raia wa Tanzania)
 
Swali la kujiuliza ni kwa nini wananchi hawana tena imani na vyombo vyetu kuanzia polisi na sasa hadi madaktari? Kuna precedence hapa. Sokoine alikufa katika mazingira ya kutatanisha yakapita hivihivi hadi leo umebaki uvumi, na hatutaki kufanya uchunguzi.

Kifo cha Amina, Mbatia vyote vilikuwa na maswali mengi na hadi leo tumebaki na maswali yetu. Sasa na hiki ni hivyohivyo, utata upo wazi, tumebaki tunafanya siasa na itaisha hivihivi.

Inawezekana kabisa wenye malengo yao wakafanikiwa kutumia msiba huu kuidhoofisha chadema, lakini kwa vyovyote vile haitatusaidia katika kujibu maswali tuliyo nayo, zaidi ya kuzidisha hofu miongoni mwa wananchi, na wala kuidhoofisha chadema kwa njia chafu za kutumia msiba huu haisaidii kutatua matatizo ya wananchi yaliyosababisha wawe na chuki na serikali yao. Chacha amefariki, na inawezekana wakafanikiwa kuizima chadema kama walivyopania, lakini kwa hakika hawatazima msisimko wa mabadiliko ambao unachemka nchini. Ataibuka Chacha mwingine na itazaliwa chadema ingine.

Kinachonipa shida kuliko vyote mimi ni imekuwaje vyombo vyote muhimu kama polisi na sasa madaktari vimefika mahala vinakubali kutumikia wanasiasa badala ya kutumikia utaalamu wao? Tumefikaje hapa na tutajitoaje?
 
Mkuu,

Si kweli, huyo mwansheria ana partners Watanzania ambao ndio wanaenda mahakamani kuendesha case, yeye anaweza tu akawa anawashauri. Huwezi kwenda kuendesha case
kwenye mahakama za TZ kama hajasajiliwa hapo nyumbani.

Aidha, mpaka sasa Chenge hana case yoyote Tanzania, huyo mwansheria wake anamwakilisha huku nje kule alikoficha vijisenti vyake. Huyo lawyer mwenyewe alitamba kwamba amesajiliwa kufanya kazi kwenye hiyo nchi.

Mkuu hakuna uongo hapo ,anapatikana jengo la kitega uchumi floor ya tano, na jina lake ndio hilo.Mbona Mkono anaenda kuendesha kesi nje ya Nchi?

Unawajua wanasheria wa Barrick? Je? wa City water mbona walikuwa kwenye kesi hapa nchini kabla ya kuzipeleka nje?

Unawajua wanasheria wa Lowassa ambao wanapatikana pale RECS ATTONEY? NI wazungu ,sasa sikuelewi unamaanisha kitu gani kusema hawawezi kwenda mahakamani hapa Bongo.
 
Sasa hapo mbona hali inazidi kuwa Tata, na Serikali sasa ndio inaanza kufanya jambo zima lionekane gumu. Na hawaoni aibu kumleta daktari ambaye alifanya uchunguzi mara ya kwanza ambao wanandugu wameona kwamba una walakini? Kwani Prof. Wangwe alipoongea jana alisema kwamba wanataka kurekebisha makosa ya Uchunguzi uliopita.

Sidhani kama hili jambo litaisha kwa urahisi namna hii... Ndio kwanza kunakucha...
 
Hii ndiyo Tanzania yetu, mimi bado najiuliza kama wamemuua ni akina nani hao na ni kwa kosa gani kubwa alilofanya mpaka wamuue?

Kama ni CCM je madaraka ya kuchukua jimbo la Tarime ndilo limtoe uhai mtu? Kwani ukikaa bila kuwa mbunge utakuaje. Yaani madaraka ni bora kuliko uhai wa mtu? Shetani wakuwa hawa.

Na kama ni chadema uenyekiti ni bora kuliko uhai wa mtu jamani kweli? Hivi unapokwenda kunadi sera za chama si unamwomba Mungu akusaidie watu wakuelewe na wajiunge na chama? sasa wamejiunga tena uwe wa kwanza kuwaua. Tumieni busara ya Mungu kwamba hata ukikosa Yeye anakuvumilia na ukitubu anakusamehe.

Na kama ni maadui wengine bado utu wa mtu ni bora kuliko chochote (pesam nyumba, mradi, mke, demu, n,k)

Ni kweli sheria ya kuleta daktari kutoka nje kufanya kawi hii bila kusajiriwa na chombo cha madaktari nchini ipo ila sasa hizi sheria zetu zisitumike tu kama mtego kwa kuangalia maslahi furani.
 
What? is Shaba gone? Wale Madaktari wa makerere in the 60s wameisha jamani! r u sure he' dead? Kuna pathologist mjerumani mwanamke kaolewa na mmachame wamjaribu hacorruptiki. Prof shao vipi?ruksa?
 
Kitila, Inatisha sana hii hali. Hasa ukizingatia wasomi na waelewa wa mambo kama wewe na wengine wengi tunafika mahali hatujui kule nchi inaelekea. Wale ndugu zetu ambao hawakupata vidato na kutolewa tongotongo la elimu wana hali gani? Mishangao yao ikoje? Tuna toafuti gani nao leo hii katika kufumbua vitendawilii hivi vigumu? Viongozi wetu hivi huwa wanawaza nini? Maisha bora kwa kila mtanzania? It is Pathetic!
 
Mtanzania, ilikuwaje fire departement walikuja kufanya uchunguzi wa ajali ya moto shauritanga, ilikuwaje wakaguzi wa hesabu kutoka nje wakaja kukagua mahesabu ya Tanzania, kwani hawa hawakuwa na uwezo wa kuleta habari za uongo na kutimua? Kama hicho ni kisingizio cha kuficha ukweli hakifai.
I am sure at the end damu ya Wangwe itakwenda na maji, itasemwa for the sake of something we do not know let us put this aside. Nadhani kuna thread moja nili-predict kuwa tusubiri series ya vifo vya watu and that is where we are.

Bongolander,

Mambo ya fire siyajui kwahiyo siwezi ku comment.

Mambo ya accounts hii inafanya kazi dunia nzima. Hata kampuni ya Tanzania inaweza kufanya kazi mahali popote baada ya kutimiza sheria za nchi husika.

Una uhakika gani hao waliochunguza mahesabu ya EPA hawajasajiliwa Tanzania? Kwanza aliyechunguza ni mtanzania na ana ofisi TZ. Huenda E&Y wamesajiliwa TZ pia.

Hata hao madaktari wa macho na magonjwa mengine huwa wanapata vibali kabla ya kuruhusiwa. Huwa hawashuki tu airport na kuanza kutibu watu.

Kuna mambo mengi sana yanafanyika chini chini, huwezi kujua mpaka kama kuna tatizo.

Mara nyingi hata kama kampuni haina usajili ndani ya nchi, ikipata tender, kazi ya kwanza ni kuanza usajili na kupata vibali vingine.

Wote tumelalamikia hapa kuhusu ile kampuni ya Norway kufanya kazi TZ bila usajili. Leo
tunapinga kukatazwa kwa daktari ambaye hajasajiliwa Tanzania.
 
Mkuu hakuna uongo hapo ,anapatikana jengo la kitega uchumi floor ya tano, na jina lake ndio hilo.Mbona Mkono anaenda kuendesha kesi nje ya Nchi?

Unawajua wanasheria wa Barrick? Je? wa City water mbona walikuwa kwenye kesi hapa nchini kabla ya kuzipeleka nje?

Unawajua wanasheria wa Lowassa ambao wanapatikana pale RECS ATTONEY? NI wazungu ,sasa sikuelewi unamaanisha kitu gani kusema hawawezi kwenda mahakamani hapa Bongo.

Kiranja,

Tusibishane bila facts, niambie huyu mzungu wa Chenge anaendeshe case gani na mahakama ipi?

Una uhakika gani hao unaowasema kwamba hawana usajili wa kuendesha case Tanzania?

Suala sio uzungu au weusi, suala ni kusajiliwa. Tuna wanasheria wengi hapa labda wanaweza kutusaidia.

Mtu ambaye anaendesha case bila kusajiliwa anavunja sheria. Kama unamjua mmoja, waambie hicho chama cha sheria na watamshughulikia mara moja.
 
Huyo daktari ni mwanaume kweli kweli. Kwenye msiba uliojaa siasa kama huu, wanaweza kuingia waliomo na wasiokuwemo. Ni bora ashirikishe watu wengine wengi kama waangalizi
ili akisema tofauti na kile wanachotaka wananchi, yasije yakampata mabaya.

Namwonea huruma na kumwombea pia huyo daktari.

MTANZANIA....

Ni kweli inahitaji ujasiri kidogo.labda nisaidie kidogo nahojua kuhusu Postmortem;kwa kawaida hufanywa kwenye tukio lolote la kifo chenye kuonekana sio cha kawaida,polisi hufanya hivi ili kuweka taarifa sahihi za kifo incase baadae akatokea mtu kufungua kesi au shauri juu ya chanzo/muhusika wa kifo.hapa order huwa inatolewa na hakimu(kama sijakosea),pili ndugu za mfiwa wanaweza kuomba postmortem endapo wana mashaka juu ya chanzo cha kifo.
Now wakati wa postmortem zinakuwapo pande tatu,daktari,polisi na ndugu wa maiti.Kabla ya kuanza ndugu atauliza na polisi anamtambua aliyekufa na wanauhusiano gani.je ndie huyu aliyelala hapa?akishatoa maelezo hayo,daktari atafanya postmortem na kuandika ripoti ambayo daktari hubaki na nakala moja kwa ajili ya kumbukumbu ya hospitali.

Kuhusu Dk.kutoka kenya ni sahihi kumzuia,kwani hana leseni ya kupractice hapa,lazima competence yake ithibitishwe na ndipo asajiliwe.
 
Kitila, Inatisha sana hii hali. Hasa ukizingatia wasomi na waelewa wa mambo kama wewe na wengine wengi tunafika mahali hatujui kule nchi inaelekea. Wale ndugu zetu ambao hawakupata vidato na kutolewa tongotongo la elimu wana hali gani? Mishangao yao ikoje? Tuna toafuti gani nao leo hii katika kufumbua vitendawilii hivi vigumu? Viongozi wetu hivi huwa wanawaza nini? Maisha bora kwa kila mtanzania? It is Pathetic!

Nakubaliana na wewe moja kwa moja. Ni kama vile nchi iko kwenye ndoto ya kutisha! Na muda wowote ukiamka unaweza kuambiwa nchi imetekwa! Viongozi wawaze nini, kwani wanajua wanachokifanya?
 
Anaweza akawa ni mwenye maelekezo maalum wenye taarifa wafuatilie na kutuambia katoka wapi huyu?

Pia kuna haja ya kujua kuna kitu gani hapa kinachofichwa kuhusiana na kumkataa huyu wa Kenya ? si wangempa tu kibali maalum kwani kufanya hivyo kungewafanya wananchi waamini kuwa serikali wala watawala hawahusiki na msiba huu?

Kiranja maelezo mengine yatafuata .............hivi punde
 
Ni wakili gani wa Chenge anayetoka nje ya TZ ambaye anamwakilisha Chenge TZ?

Ni daktari gani wa nje ambaye anatibu wagonjwa TZ bila kusajiliwa?

Ni Engineer gani wa nje ambaye anajenga nyumba TZ bila kusajiliwa?

Kama kuna yeyote anafanya hayo hapo juu, anavunja sheria, unaweza kumpeleka polisi.

Cases za majanga zinashughulikiwa na sheria tofauti. Hata red cross wana wanasheria wao wanaowasaidia juu ya namna ya ku operate kwenye nchi mbalimbali.

Sibishani ila nilikuwa najibu swali lako la kwanza na kukupa facts, kama ulikosea kuliuliza kiri kwani muungwana ni vitendo.

Nashukuru.
 
Swali la kujiuliza ni kwa nini wananchi hawana tena imani na vyombo vyetu kuanzia polisi na sasa hadi madaktari? Kuna precedence hapa. Sokoine alikufa katika mazingira ya kutatanisha yakapita hivihivi hadi leo umebaki uvumi, na hatutaki kufanya uchunguzi.

Kifo cha Amina, Mbatia vyote vilikuwa na maswali mengi na hadi leo tumebaki na maswali yetu. Sasa na hiki ni hivyohivyo, utata upo wazi, tumebaki tunafanya siasa na itaisha hivihivi.

Inawezekana kabisa wenye malengo yao wakafanikiwa kutumia msiba huu kuidhoofisha chadema, lakini kwa vyovyote vile haitatusaidia katika kujibu maswali tuliyo nayo, zaidi ya kuzidisha hofu miongoni mwa wananchi, na wala kuidhoofisha chadema kwa njia chafu za kutumia msiba huu haisaidii kutatua matatizo ya wananchi yaliyosababisha wawe na chuki na serikali yao. Chacha amefariki, na inawezekana wakafanikiwa kuizima chadema kama walivyopania, lakini kwa hakika hawatazima msisimko wa mabadiliko ambao unachemka nchini. Ataibuka Chacha mwingine na itazaliwa chadema ingine.

Kinachonipa shida kuliko vyote mimi ni imekuwaje vyombo vyote muhimu kama polisi na sasa madaktari vimefika mahala vinakubali kutumikia wanasiasa badala ya kutumikia utaalamu wao? Tumefikaje hapa na tutajitoaje?

Kitila,

Hayo ni matatizo ya serikali zinazoendesha mambo kwa mabavu mabavu. Dawa ya rumours ni ukweli 110%.

Kitu pekee ambacho mimi siungi mkono ni kuvunja sheria. Ila ni mwumini wa ukweli na naamini serikali inayojali matakwa ya wananchi wake lazima iwe tayari kwenda extra mile katika kuutafuta ukweli. Kuna njia nyingi za kupata ukweli bila kuvunja sheria.

Serikali ya CCM si mwumini wa ukweli na wanatuficha mambo mengi ndio maana hata sisi wananchi tunashindwa kuwaamini.

Wa kulaumiwa hapo ni serikali yenyewe ambayo imetufikisha hapa ambapo sasa hatuamini kitu kinachotoka kwenye midomo ya serikali.

Kunahitajika juhudi kubwa kuweza kurudisha imani ya wananchi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom