Bongolander,
Mambo ya fire siyajui kwahiyo siwezi ku comment.
Mambo ya accounts hii inafanya kazi dunia nzima. Hata kampuni ya Tanzania inaweza kufanya kazi mahali popote baada ya kutimiza sheria za nchi husika.
Una uhakika gani hao waliochunguza mahesabu ya EPA hawajasajiliwa Tanzania? Kwanza aliyechunguza ni mtanzania na ana ofisi TZ. Huenda E&Y wamesajiliwa TZ pia.
Hata hao madaktari wa macho na magonjwa mengine huwa wanapata vibali kabla ya kuruhusiwa. Huwa hawashuki tu airport na kuanza kutibu watu.
Kuna mambo mengi sana yanafanyika chini chini, huwezi kujua mpaka kama kuna tatizo.
Mara nyingi hata kama kampuni haina usajili ndani ya nchi, ikipata tender, kazi ya kwanza ni kuanza usajili na kupata vibali vingine.
Wote tumelalamikia hapa kuhusu ile kampuni ya Norway kufanya kazi TZ bila usajili. Leo
tunapinga kukatazwa kwa daktari ambaye hajasajiliwa Tanzania.