Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
I am shocked with these news! Mungu ailaze roho ya marehemu CZW mahala pema peponi, Amina!
 
Sipendi kusisitizia lakini surely... viongozi wetu wangetumia gari ambazo kidogo ziko salama zaidi... although hakuna 100% security/safety.

Na raia wa kawaida ndio watumie yasiyo salama?

Kasheshe unachemka!
 
Poleni sana wote mnaohusika na msiba huu mkubwa!
Kuweni na subira na uvumilivu katika wakati huu mgumu!
Mola Mwenyezi amlipe kwa kadiri ya wema wake na awabariki nyote! Amiin
 
hapo Ndipo Watanzania Wanaponishangaza ...wakinunua Hayo Mashangingi Mnalalamika ...wakiendesha Corola Na Kupata Ajali Mnataka Wanunuliwe Mashangingi...kweli Siasa Ya Nji Hii Anaiweza Lyatonga Tu....

Hapana Mkuu, Kama M/kiti Anasafiri Kwa Helcopter,why Makamu Atembelee Corolla Tena Hata Haina Airbag!!!!

Wanaosema Serikali Ijiondoe Ktk Magari Ya Enzi Za Benja Ni Wendawazimu Tu, Ulalamishi Umetujaa Sana Sisi Wa Tz, Watu Hmataki Ndege Ya Rais Iwe Mpya !!!!!

Bado Tuna Safari Ndefu Sisi Wa Tz Ili Tuweze Kuwa Wakweli Mbele Ya Mtu Yeyote.
Kwa Sasa Mtu Anaweka Msimamo Just Bcoz Hampendi Fulani Na Si Un Yeti Wa Issue.
 
Kwa mujibu gazeti la The Citizen la leo, tairi lilipita pancha 2 na Mallya alikuwa amekaa kiti cha nyuma na wala si cha mbele pamoja na dereva. Taarifa tete kama hizi ndio huwa zinazaa utata kama ule uliotokana na Hayati Sokoine kukaa upande ambao hakutakiwa kukaa ndani ya gari. Pamoja na hayo yote tuzingatie masuala muhimu kwanza, nayo ni kuipatia faraja familia ya marehemu na kuisaidia kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu.
 
RIP Chacha,Poleni ndugu, marafiki na wana tarime na watanzania.
Pia watu humu tupunguze uzushi, hivi kila bunge likianza wakaenda car dealers na wabunge kuchagua magari hatutasema? mara ngaoi tunawalaumu na kuwanyoshea vidole eti wanaendesha mashangingi bila kujali wapiga kura wao? Tusiwe na double standards.
Chacha kaondoka na bila hiyana ndani ya kikolola chake not even a rav 4. Hakuwa ndani ya gari ya kifisadi.
Hivi mbowe na kambi yake wataenda kwenye mazishi baada ya majungu yote waliomfanyia?

??????????????????
 
Hapana Mkuu, Kama M/kiti Anasafiri Kwa Helcopter,why Makamu Atembelee Corolla Tena Hata Haina Airbag!!!!

Wanaosema Serikali Ijiondoe Ktk Magari Ya Enzi Za Benja Ni Wendawazimu Tu, Ulalamishi Umetujaa Sana Sisi Wa Tz, Watu Hmataki Ndege Ya Rais Iwe Mpya !!!!!

Bado Tuna Safari Ndefu Sisi Wa Tz Ili Tuweze Kuwa Wakweli Mbele Ya Mtu Yeyote.
Kwa Sasa Mtu Anaweka Msimamo Just Bcoz Hampendi Fulani Na Si Un Yeti Wa Issue.

kaka umeongea ukweli mtupu...ni kweli sisi watz hatupo real...we are double standard....
ben alinunua ndege wakapiga keleleeee..wabunge kupewa mashangingi wakapigaa kelele...wangwe kaendesha corola wanapiga kelele wanataka gx...
...naomba kutoa hoja binafsi .......tumnunulie rais ndege mpya yenye usalama zaiidi...
 
Pole sana kwa familia, jamaa, ndugu, wabunge, wanachadema,wanatarime na watanzania wote wapenda mabadiliko ya kimaisha kupitia uongozi.

Atakumbukwa kama mpambanaji aliyeweka alama ya mapinduzi katika historia ya demokrasia ya vyama vingi nchini.

AMEN.
 
Jaman Spika amelia sana. na sasa wanakutana katika kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Huduma za Bunge. Kamati ya Uongozi ni kwa ajili ya mambo ya Kibunge na kamati ya huduma ni kwa mambo ya kiutawala

This is what i was about to say.

Spika ameshindwa kuongea leo kabisa wakati ana sitisha bunge, wakati anasoma kanuni ya 149 akawa bado hajatulia hivi, ikafika kipindi mwishoni kabisa akaanza kulia akiwa anaongea, ikabidi azime mic atoke.

Hii inanifanya nihisi kwamba kuna kitu zaidi ambacho sisi hatukijui.
 
Nakubaliana na wewe mkuu!!! kuweka rekodi sawa ni kwamba tairi mbili za upande mmoja... yaani ya mbele na nyuma ndio zilizokuwa zimepasuka.

Ukubwa wa gari pia una kinga fulani... no wonder wamepewa mikopo ya magari kama nissan patrol na toyota landcruiser gx... haya yako salama zaidi kuliko Toyota Corrola...

Sipendi kusisitizia lakini surely... viongozi wetu wangetumia gari ambazo kidogo ziko salama zaidi... although hakuna 100% security/safety.

Kasheshe,

Unachoandika sio sahii kabisa, inaelekea hiyo ni group thinking ya watu wengi Tanzania na ndio maana viongozi wetu wanaongoza kwa kununua shangingi.

Gari kubwa sio kinga ya ajali. Tembelea hata websites tafuta safest cars.

Gari ndogo ni safe kama utalinganisha gari zilizo sawa kwa ubora na vifaa. Taili zikipasuka, matatizo yanatokana na gari kuviringika. Gari kubwa inaweza kuviringika zaidi ya gari ndogo, wote tumesoma center of gravity na jinsi inavyohama kirahisi kwa kitu kirefu.

Ukiachia Afrika na labda USA, viongozi karibu wote duniani wanatumia gari ndogo.

Faida ya gari kubwa ni kwamba ni comfortable kama unaenda safari za mbali na pia kwa watu wengine ni status, unaonekana uko juu ya watu wengine lakini SIO kweli kwamba magari makubwa ni salama kuliko madogo.

Ondoeni mawazo kama hayo ambayo hayaendani na facts zozote za maana, ni group thinking kama ile ya kwamba Saddam ana silaha kubwa, kiasi kwamba hata waliotakiwa kutafuta facts wakawa wanaandika tu bila uchunguzi.

Kama umeona picha mbalimbali za ajali duniani, utakuta gari ndogo imeharibika kabisa lakini baadhi ya watu wamepona, wakati hizo 4WD ni ngumu sana kupona kama impact ya collision ni kubwa.

Tatizo la Tanzania ni uendeshaji mbaya. Kuna watu wanasema barabara ya Dar - Dodoma ni nyembamba sana. Mnataka hiyo barabara iwe na ukubwa gani? Angalieni hata faida kiuchumi, hiyo barabara ukitafuta average ni kwamba gari linapita kila baada ya dakika kama kumi, matumizi yako chini sana ukiachia sehemu chache za mijini. Mnataka kutumia mabilioni ili kuzuia vifo kama 1000 kwa mwaka? Mna ushahidi gani kwamba hata barabara ikipanuliwa ajali hazitatokea shauri ya uendeshaji mbaya pamoja na magari mabovu? Economically unawezaje kuhalalisha kutumia mabilioni hayo kuokoa ajali kama 1000 huku watu malaki wanakufa shauri ya kukosa dawa? huku wakulima vijijini wanahangaika kwa umaskini shauri hakuna barabara za kufikisha mazao yao mijini? Kwa nchi ambayo robo tatu ya nchi haina barabara, utaongeleaje kujenga barabara kubwa zaidi ya iliyopo kwa Dar mpaka Dodoma?

Ukiachia USA ambako wana barabara kama viwanja vya ndege, hata hapa Europe barabara ndogo ziko nyingi tu hasa huko wilayani. Nimeendesha barabara nyingi tu hapa Europe, kwa mfano ukienda Scotland kutokea England, kuna barabara ndogo na magari ni mengi labda zaidi ya mara 20 ya TZ. Sisikii hata siku moja kwamba kule kuna ajali kuliko barabara za kuelekea London ambazo ni kubwa.

Matatizo mengi ya Tanzania ni sisi watu wake, tunashindwa kufuata sheria. Barabara ya 80km/h watu wanaendesha mpaka 150km/h. Watu wanaendesha wamelewa. dereva mmoja anaendesha hata miles zaidi ya 500 bila kupumzika, hakuna alama barabarani, polisi hawafanyi kazi zaidi ya kuchukua rushwa, magari mabovu, hayatakiwi hata kuwa barabarani. barabara nyingi hazitengenezwi, mashimo yanaibuka bila kuzibwa.

Matokeo yake tunajidanganya kwamba tukiendesha shangingi tutasalimika, sio kweli, hata Mbatia alikuwa na shangingi. Kuna mate wangu mmoja, kijana msomi karudi toka nje akajenge taifa, akagongwa na shangingi lake na hakupona. Kwa Tanzania hata unayefuata sheria bado unaweza kuwa victim maana waendeshaji wengine watakufuata hata kule unakoendesha salama au hata kukugonga ukiwa umesimama.

Tutasubiri mpaka watu wangapi wafe kabla ya kuchukua hatua?
 
Napenda kutoa pole sana kwa wana-CHADEMA wote, hasa kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa kuondokewa na mwanamapinduzi mwenzetu Mungu azidi kuwapa nguvu katika wakati huu mgumu wa majonzi. Napenda kuwapa pole pia ndugu zangu wa Musoma kwa kuondkewa na kiongozi shupavu. Poleni sana ndugu zangu.
 
Nimekuwa puzzled muda mrefu kuhusu kifo cha CZW kwa kweli sijaamini lakini imebidi nilazimike kuamini, Mungu amlaze mahali pema peponi, Amina
 
Kipande cha barabara ya Pandambili hadi Gairo - inavyodaiwa na wenyeji - kuna vibwengo vinavyokunywa damu za watu. Katika kipindi cha miezi 3 iliyopita mabasi ya Champion na Happy Nation yalipata ajali maeneo hayo hayo. Na wenyeji hao hao wanakupa uhakika kuwa ukitaka kumfanyizia mtu, sehemu hiyo huwa muafaka sana.

Hizo Imani za Uchenge inabidi watanzania tuzikatae kwa nguvu zote.

RIP Wangwe, umetutangulia ndugu yetu na kila nafsi itaonja mauti! umemaliza zamu yako bado yetu!
 
Natoa Pole Kwa Wana Chadema Kwa Kumpoteza Mtu Shupavu Sana Na Mpigania Haki, Mungu Awape Nguvu Na Ujasiri Ndugu Jamaa Na Marafiki Wa Marehemu Wangwe. Sisi Tuilimpenda Sana Lakini Mungu Amempenda Zaidi. Mungu Aiweke Roho Ya Marehemu Wangwe Mahali Peme Peponi, Amen
 
Pamoja na ukweli kuwa kila mtu ana ubaya na uzuri wake, Lazima tukubali kuwa wanamageuzi tumempoteza mwenzetu.

Chacha Wangwe atakumbuka kwakuwa ameingia kwenye historia ya kuwa mwanamapinduzi wa nchi hii.

Vizazi vijavyo vitasimuliwa kuwa aliwahi kuishi Chacha.Kuondolewa umakamu mwenyekiti hakukumwondolea sifa na nafasi yake ndani ya CHADEMA.

Nenda Chacha, nenda kwa amani kapumzike!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom